Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Kaka kingereza ni muhimu sana na hauwezi kukikwepa, haswa kwa nchi zetu hizi ambazo tunaagiza hadi sindano. Kwenu hapo mikataba, sheria na stakabadhi nyeti zimeandikwa kwa kingereza. Hivyo mtakiponda kila uchao kwa dhana ya 'sizitaki mbichi' lakini kimewazunguka na kuwalea. Lazima mkubali kuikabili hii lugha ya mabwana zetu Afrika, maana ndio inatumika kuwatafuna kwenye mikataba.
Hilo la nyie kuwa na elimu halina mashiko ni 'neither here nor there' maana elimu hiyo kama hamuitumii kulinda vya kwenu, basi haina umuhimu. Nafuatilia mijadala yenu ya mchanga wa madini hadi nahisi kujificha chini ya meza kwa aibu, kama kweli mumekua mkiliwa miaka yote hii kijinga hivyo pamoja na elimu yenu hiyo ni aibu kubwa Afrika na sio kwenu tu.
Wenye elimu huitumia kwa maslahi ya nchi, wanahoji balaa, na kukatalia chochote kisichoendana na misimamo yao, hata kama watapitia kibano sio kusubiri hadi mtafunwe mifupa ndio mnaanza kukurupuka.
Soma taarifa za profesa Wangari Maathai ndio uelewe nini maana ya elimu.
Wakenya wanajua Kiingereza lkn bado wanaibiwa tu kila siku, kama Viongozi wa Kenya wakianika Mikataba wanayosaini na Wageni, kutatokea Mapinduzi kesho, siajabu Kenya yote imeshauzwa kwa Mzungu/Mchina si ajabu hata Mombasa siyo Mali ya Kenya, ...