Mchina Aoa Mrembo wa Ethiopia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchina Aoa Mrembo wa Ethiopia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chinese boy, Jun 20, 2009.

 1. Chinese boy

  Chinese boy Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Januari Tarehe 21,2009 Kulikuwa na Shamra Shamra za Kusisimua pale sehemu moja ya jiji la Wuhan Pale ambapo wachina wameshuhudia moja ya matukio machache sana ambapo kijana wao amejitosa na kuopoa mrembo wa Ki Ethiopia.Huyu Jamaa amekutana na binti akiwa kule Ethiopia
  katika huduma ya Utabibu.Na binti hajui Kichina haha!
  Kwa Wachina hii case ni very rare,maana mara nyingi wameshuhudia tu vijana wa ki'Afrika wakioa mabinti zao.Ukizingatia kuwa Nchini China wanawake ni wachache kulinganisha na idadi ya Wanaume,Wanaume wengi wa Kichina wamejenga chuki kiaina na Waafrika wanaochukua mabinti zao kama girlfriends au wake.Lakini tukio hili limeonekana kuwa ni furaha sana kwao na kwa haraka hakuna aliyeonekana kupinga,maana wengi hawapendezwi pale Mwafrika anapooa binti wa kichina.
  Nafikiri matukio kama haya yatawapa faraja wachina wanaume wengi ambapo wamekuwa hawana Confidence ya kuwa wanaweza kuwa na mabinti wa Kiafrika.
  Najua pale Arusha kuna binti mmoja kaoana na Mchina Actect fulani
  Ila sikufanikiwa kupata Story yake vizuri.Kama kuna cases nyingine naomba wadau mnipe data.
  Angalia Link Hii Hapa ambapo TV moja iliamua kulifuatilia hili jambo vilivyo.
  http://www.56.com/u75/v_NDE1MDE4MzI.html
  Ingekuwa ni matukio ya Waafrica kuoa mabinti wa Kichina najua wangeshindwa chagua wa oneshe ndoa ipi maana ni nyingi sana,lakini
  katika hili kulikuwa na Special Excitment kwa Watazamaji...
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hongera kwa new couple. Wafanye fastafasta kutuletea vi-nephew..
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Vinaweza kuwa feki kwa kweli...siwaamini hawa hata kidogo.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Jikusoma mazee..yaani kitu gani ni feki hapo? ndoa? au vi-nephew?
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...labda wakaishi nje ya U china, sheria ya mtoto mmoja (计划生育政策) si bado inaendelea?
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wakitaka watoto zaidi ya mmoja basi wakaishi nje ya city - huko unaweza kuzaa zaidi.Ukiishi ndani ya city utakoma maana sera na sheria za huduma zitakukomesha.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Tutaona matokeo ya mwingiliano wa wanaume wa kichina na wanawake wa kitanzania katika miaka ijayo ... thanks to projects mbalimbali - ujenzi wa Uwanja wa Taifa, ujenzi wa barabara, majengo n.k.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  He he he..Hii kesi ya huyu mdada wa kiethiopia ni tofauti na kadhia za wadada wetu 'wapiganaji' wanaohangaika kutafuta faranga na wachina. Huyu mdada na mumewe wanaonekana wametokea mbali hawajakurupuka na hata mtoto pundamilia akipatikana anakuwa kweli anajitambua na kujiheshimu tofauti na dizaini za kontrakta wa kichina na dada 'mpiganaji'.

  Kiukweli napenda watoto 'pundamilia' waliolelewa vyema ..wanakuwa very unique na wanaleta kitu tofauti ktk jamii yeyote ile.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  LOL!
  Umenichekesha sana Abdulhalim!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  teh teh teh..u r welcome..
   
 11. Chinese boy

  Chinese boy Member

  #11
  Jun 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchini kwao pia unaweza zaa watoto wawili kama baba na mama wote
  wametoka familia za kichina zenye mtoto mmoja.Pia wale wa makabila madogo wanaruhusiwa kuzaa wawili.Pia kama una pesa ya kutosha ukikutwa umezaa wa pili unaweza pewa adhabu ya kulipa pesa fulani then inakuwa imetoka.Kwa kijijini ukweli ni kuwa inakuwa ngumu sana ku manage.Lakini ukifanikiwa kukutwa umezaa tayari na huna pesa ya kulipa
  wanaweza zoa vitu vyako vyote vya nyumbani kama furniture.Ila ukifumaniwa mjamzito hujazaa hapo pagumu,kwa hiyo ufanye ujanja wako
  uzae.
  Pia kuna jamaa wajanja hao wenye pesa zao,Wanaoa binti na wakisha zaa naye wana tafuta mbinu za kumpa talaka,then wakioa mwingine wanaruhusiwa zaa,Kwa hiyo naamini hili ni tatizo kubwa maana akina mama wazee wengi wameachwa na waume zao.
  Kwa hilo la jamaa kuoa binti wa nchi nyingine nitatafuta jibu sahihi na kulileta hapa JF.
  Ila ukweli ni kuwa hawa jamaa wamesambaa sana duniani na sasa wengi wamekuwa na uwezo mkubwa kifedha na hivyo naamini kuna Waafrika mabinti wengi hapo baadaye watajikuta wameolewa nao
  na hivyo kuondoa fikra ambayo wengi wao walikuwa wanaona haiwezekani.Hata wazungu pia idadi ya watakaolewa na hawa jamaa itaongezeka maana kila siku wazungu wanazidi jaa kwenye
  nchi hii kutafuta maisha na hivyo wengine wataona kurahisisha mambo heri waolewe nao.
  Ninachofurahi ni kuona hadi sasa jamaa wanajiona wako Chini sana kwa Mzungu kifedha,Yaani hata jamaa Tajiri sana akimwona
  Mzungu anajiona maskini hata kama Mzungu hana chochote,Haha!
  Basi inawapa mori wa kupiga mzigo kusonga mbele!!!
  Cheers!!!!
   
Loading...