Mchina anyongwa ndani ya gari Dar!

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Mfanyabiashara raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,Uwazi linakupasha.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi maeneo aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyozidi kulitilia shaka maana hakukuwa na mtu aliyetoka ama kuingia.

Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.
Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.

“Huyu marehemu inaonekana alikuwa akitoka casino na uchunguzi wa awali unaonesha aliuawa sehemu nyingine na akutupwa hapo.Tunaendelea na uchunguzi kuwasaka watu aliokuwa nao casino kwa mara ya mwisho,” alisema Kamanda Fuime aliyefafanua kuwa mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

11.jpg

22.jpg

33.jpg

44.jpg


Habari kutoka Globalpublishers
 
Back
Top Bottom