Mchina anayesafiri kutoka China hadi Afrika Kusini kwa baiskeli aingia Tanzania

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,960
4,208
Wadau,

Leo nimekutana na Mchina Mr. Lee Jian Bo ambaye ameamua kufanya safari kutoka China mpaka South Africa kwa kutumia baiskeli. Mr.Lee ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika Biolojia(Bachelor of Science in Biology) kutoka Hubei University.

Alianza safari yake mwezi April 2013 na kwa sasa ameingia Tanzania na nimekutana naye na kufanya naye mazungumzo machache ili kuweza kufahamu zaidi kwa nini ameamua kufanya safari hii ndefu tena kwa baiskeli.

Mpaka sasa amekuwa safarini kwa miezi 13 yaani mwaka mmoja na miezi miwili.

Alianza safari katika jimbo la Wuhan - China na amepita nchi zifuatazo kwa mtiririko Vietnam - Cambodia - Thailand - Sri Lanka - Iran - Armenia - Jordan - Misri - Sudan - Ethiopia - Kenya - na sasa yupo Tanzania.

Hakuweza kupita India kwa sababu alikosa visa, lakini pia hakupita Somalia kwa sababu ya hali ya kiusalama.

Kwa muda huo hajawahi kulala hotelini, mara nyingi amekuwa akilala kwenye makanisa, vituo vya mabasi, shule au kwenye majengo ya vyuo na majengo mengine ya kijamii.

Nilipoangalia baiskeli yake ana vifaa mbalimbali kama turubahi (tent), vifaa kwa ajili ya matengenezo ya baiskeli yake, begi dogo la nguo na mfuko wa vitabu.

Safari yake inaendelea, akitoka Tanzania - Zambia - Namibia - Afrika Kusini.

Atakapofika Afrika Kusini atarudi China kwa kutumia ndege.

Nilishawishika kujua kwa nini ameamua kufanya safari ndefu kiasi hiki tena kwa kutumia baiskeli

Alinijibu, ninafanya hivi kwa sababu nataka kujifunza mambo mbalimbali duniani.

Lakini pia nilimuuliza mpaka sasa ametumia pesa kiasi gani?

Alinijibu kuwa mpaka sasa ametumia dola za kimarekani 2,000/= Jumla ya bajeti yake mpaka atakapofika Afrika kusini ni dola 3, 000/-

Changamoto; safari ndefu namna hii haikosi changamoto.....

Amekutana na changamoto mbalimbali

Moja, upatikanaji wa visa katika nchi mbalimbali hii imemfanya kutumia muda mwingi zaidi kusubiri visa na hivyo kuongeza muda mrefu zaidi wa safari yake.

Mbili, vikundi vya waasi, kwa kuwa anasafari kwa baiskeli amkekutana na vikundi vya waasi katika nchi ya Sudan kwa bahati nzuri hawakumfanya chochote baada ya kugundua kuwa hakuwa na silaha yoyote.

Tatu, baiskeli kuharibika mara kwa mara, amekuwa akiharibikiwa na baiskeli yake ambayo ndio usafiri wake mara kwa mara.
Unaweza kuangalia baadhi ya picha zake na baiskeli anayoitumia kwa safari hii ndefu.

View attachment 161726

Bado nina mazungumzo naye marefu na kwa kuwa atakuwa hapa kwa siku mbili zijazo basi nitawajuza zaidi.

Hapa unaweza kuona picha nyingi zaidi alipokuwa katika nchi mbalimbali.
https://www.couchsurfing.org/image_gallery.html?id=5H11IRR60
 
ebooo hivi vitu vingine hata mtu unashindwa kufikiria vinatokeaje tokeaje :der:
 
Binadamu wengine jamani ....... Hivi kweli kabisa anafanya yoote hayo ...why,for who,for what...nimechoka je Mimi,ahsante kwa kunijuza ili nalo .
 
Mambo mengine hayaleti sense, inamaana kutoka China hadi bara Africa amevuka bahari kwa baiskeli
 
Mambo mengine hayaleti sense, inamaana kutoka China hadi bara Africa amevuka bahari kwa baiskeli

Unashindwa kujiongeza? Akifika maeneo ya bahari anapanda meli, then akishavuka anachochea baiskeli!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nimeipenda hiyo! kamfunika yule mfuasi wa ccm frm geita to dsm(magogoni) kwa baiskel tena anita aina ya phoennex!
cc bnyanya mzee wa minyoo na safari yake ya kwenda ghana!
 
Last edited by a moderator:
Bora pikipiki, sijui hali ya ko.ro.da.ni zake itakuwaje, kwa jinsi alivyokuwa anachochea ni kuua mashine
 
amepita kote,mshaur kuhusiana na wanyama wa mikumi atapokuwa akielekea mbeya njian kwenda zambia.Pia akikutana na waasi wa mbugan ,wazee wa meno ya tembo apite tu kama awakuwaona

Hao wanyama sio ishu ila hao watu wa meno noma
 
Back
Top Bottom