Mchina adakwa akifanya UDUKUZI siri za Marekani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
160324054347_f-22_fighter_jet_640x360_getty-620x308.jpg


MTU mmoja raia wa China aliyefahamika kwa jina la Su Bin amekiri kuhusika katika njama za kuiba siri za mifumo ya ndege za kijeshi za Marekani,

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) limeeleza kuwa, Su Bin aliyekamatwa nchini Canada tayari amekiri kufanya kazi na watu wawili kutoka China kati ya Oktoba 28 na Machi 2014 kudukua mifumo ya Kompyuta ya Marekani ikiwemo Kompyuta ya Boeing inayotumiwa na Jeshi la Marekani kuunda ndege zake.

Hata hivyo Su Bin (50) anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba taarifa za kuhusu ndege za kubeba mizigo na silaha.

Amedaiwa kuwa na kampuni ya teknolojia ya uchukuzi wa ndege nchini Canada ambaye tangu mwaka 2014 amekuwa akitafuta uraia wa Canada bila mafanikio.
 
Wachina wana ndege yao ya abiria wanataka kuiweka sokoni soon.Nadhani kuna technology imewashinda sasa walitaka kuiba KWA boing.Ni vijizi sana si vibunifu kihivyo
hata wamarekani nao wanaiba sema hawajashitukiwa! inshort hakuna nchi ambayo haina maandikizi/spies kwa nchi mahasimu!! usishangae hata sisi tuna wetu huko kwa kagame au kagame ana spies hapa kwetu!! ni kawaida!
 
Wizi nao wahitaji ubunifu km mzembe unatendwa....wachina wana fyt km tukiwaiga tutafika mbali...yaab km ulishawai fanya kaz na hawa jamaa utajua tuu kuwa jamaa wanapiga kazi n balaaa hakuna kulembaaa.....tuache kukenua mimeno humu tu fyt kwa vyetu km chinaa
 
Eheheh mkuu umenichekesha sana, swali la dharau sana hili, ingekuwa hivyo hata Tiss sijui wangekuwa na kazi gani, specila training wanazopewa,ehehe u must be joking
Enlighten me, siri gani tulizonazo? idadi yawake/mahawara wa maraisi? au jeshi lina mabomu mangapi? wenzetu wanadeal na technological secrets sio siri za upatu aisee
 
Wachina wana ndege yao ya abiria wanataka kuiweka sokoni soon.Nadhani kuna technology imewashinda sasa walitaka kuiba KWA boing.Ni vijizi sana si vibunifu kihivyo

Halafu mi CCM inawafagilia, China ni taifa la kipumbavu kabisa, hawajawahi kubuni technology yao, wao kila kitu ni kuiba tu, halafu vinajifanya vina sheria Kali za kunyonga wezi wakati vyenyewe ndo vijizi hatari.
Usijaribu kupanda ndege Made in China, lazima ianguke maana ktk kuiba ni lazima kuna technology wataikosea tu.
 
Back
Top Bottom