Mchezo wa Simba na Yanga kuchezwa tena, Mashabiki kurudishiwa tiketi zao

Hivi unaweza kutaja mkuu baadhi ya hukumu tunazoweza kupewa na Fifa na namna zitakavyoikomoa Tff?
Hukumu moja wapo Tanzania inaweza kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa muda na hukumu hiyo itatutia akili sisi Watanzania na itapelekea wadau wa soka nchini kuibadilisha kabisa safu yote ya uongozi pale TFF.
 
Hivi mbona wanakwepa sana kusema ni nini kilisababisha kughairi huu mchezo?

Kwanini hatuambiwi tatizo lilikuwa nini?
Mkuu hili ndo suala la msingi,sidhani kama hata mashabiki wana haja kurudishiwa chochote ,kwanza kwa mifumo yetu ni ngumu kumrudishia mtu hela yake
 
Wale wapumbavu waliokuwa wanasema serikali HAIUSIKI Na TFF mmeona?.
Chanzo hakisemwi, lakini kinajulikana, ni siasa, kuuza sura kwenye tv, kuendesha nchi bila kuzingatia sheria. Mtoa maagizo aliona avunje pambano ili watu waangalie uzinduzi wa kitabu na kupeana zawadi ya gari. Madhara yaliyojitokeza ni makubwa kuliko matarajio ya kisiasa.
 
Na huyo huyo ndo ametoa tamko.
Mechi ichezwe UPYA.
basi Sawa.
Yanga wanatakiwa wagomee na hyo tarehe mpya

Mpira wa bongo una visa.

Eti msimamizi wa soka na vilabu kwa ujumla haelewani na kilabu kimoja kiasi kwamba waziri anaitisha kikao.
Tff na bodi ya ligi wanaweza kuwa mbuzi wa kafara, lakini mhusika mkuu ni serikali.
 
Serikali imeishatoa maagizo kwa TFF na klabu zote mbili mpira utachezwa ila ujumbe wa Yanga kwa TFF na Serikali umefika
 
Na huyo huyo ndo ametoa tamko.
Mechi ichezwe UPYA.
basi Sawa.
Yanga wanatakiwa wagomee na hyo tarehe mpya
Ni matamko mepesi kwa swala zito. Nini sababu?, kasababisha nani?, kuna sheria imevunjwa? Amewajibishwa? Gharama ya kiingilio ni sehemu ndogo ya hasara kwa wahusika, lakini serikali inaona ndio gharama ya msingi. Kuna watu wametumia nauli, malazi nk.
 
Hukumu moja wapo Tanzania inaweza kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa muda na hukumu hiyo itatutia akili sisi Watanzania na itapelekea wadau wa soka nchini kuibadilisha kabisa safu yote ya uongozi pale TFF.
TFF unawaonea bure, hao ni mbuzi wa kafara.
 
Utopolo alivyofanikiwa kusepa kipigo piga ua hatothubutu kutia mguu tena kwa Mkapa. Atatafuta tu sababu ya kugoma jumla pamoja na kuwekwa kikao na wahusika!!
 
Kanuni ya FIFA inakataza serikali kuingilia masuala ya michezo. Sasa kama serikali inatoa maelekezo, ina maana mpaka sasa kweli wanoko hawajatuma taarifa FIFA?

Kuna hati hati ya kufungiwa na FIFA mwaka huu! Kwa sababu Dunia ni kijiji. Ila tukifungiwa hata mwaka mmoja labda ndiyo tu akili itatukaa sawa.
 
Hukumu moja wapo Tanzania inaweza kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa muda na hukumu hiyo itatutia akili sisi Watanzania na itapelekea wadau wa soka nchini kuibadilisha kabisa safu yote ya uongozi pale TFF.
Tff hii ambayo viongozi wake wanapigiwa kura na vyama vya mikoa sahau kuhusu mtu kushindwa uchaguziii akiwa pale tff .......labda sijaelewa kuwaondoa kwa njia gani?
 
Hapa sasa...

Screenshot_20210517-210136.png
 
Back
Top Bottom