Mchezo wa Mieleka nchini Tanzania

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,581
1,069
Wadau,

Nakumbuka kwenye miaka ya themanini mchezo wa mieleka ulitokea kuwa maarufu sana hapa bongo. Kulikuwa na wababe kama Power Bernado, Power Vuru Mroma, Power TX Chaka, Power Bukuku na wengineo.

Kuna yeyote mwenye taarifa za magwiji hawa waliishia wapi?
 
Tehe namkumbuka power mabula alikuja 1980 nikiwa sumbawanga, basi alipasua jiwe kifuani, akavuta gari kwa meno, akazuia pikipiki mbili zisiende kwa mkono wake halafu kwa mbwembwe akafungua fanta akapiga pafu moja akasukutua akatema, duh uwanja mzima watu ayaaaaaa maana wakati ule hiyo fanta kuipata ilikuwa adimu sanaa. TX Chaka nishamuona akipambana na vuru mroma ila sijui wameishia wapi hawa jamaaa.
 
Nakumbuka magazeti yalivyokuwa yanatangaza mapambano yao huku jamaa wakichimbana mikwara sio mchezo. Power Bernado alikuwa anatesa zaidi enzi hizo.
 
IMG-20170815-WA0020.jpg

Huyu ni power nani wahenga wenzangu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom