Mchezo wa mieleka tz

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Wadau,

Nakumbuka kwenye miaka ya themanini mchezo wa mieleka ulitokea kuwa maarufu sana hapa bongo. Kulikuwa na wababe kama Power Bernado, Power Vuru Mroma, Power TX Chaka, Power Bukuku na wengineo.

Kuna yeyote mwenye taarifa za magwiji hawa waliishia wapi?
 

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,590
2,000
tehe namkumbuka power mabula alikuja 1980 nikiwa sumbawanga, basi alipasua jiwe kifuani, akavuta gari kwa meno, akazuia pikipiki mbili zisiende kwa mkono wake halafu kwa mbwembwe akafungua fanta akapiga pafu moja akasukutua akatema, duh uwanja mzima watu ayaaaaaa maana wakati ule hiyo fanta kuipata ilikuwa adimu sanaa. tx chaka nishamuona akipambana na vuru mroma ila sijui wameishia wapi hawa jamaaa.
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Nakumbuka magazeti yalivyokuwa yanatangaza mapambano yao huku jamaa wakichimbana mikwara sio mchezo. Power Bernado alikuwa anatesa zaidi enzi hizo...
 

mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
10,494
2,000
IMG-20170815-WA0020.jpg

Huyu ni power nani wahenga wenzangu?
 

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
2,558
2,000
Wadau,

Nakumbuka kwenye miaka ya themanini mchezo wa mieleka ulitokea kuwa maarufu sana hapa bongo. Kulikuwa na wababe kama Power Bernado, Power Vuru Mroma, Power TX Chaka, Power Bukuku na wengineo.

Kuna yeyote mwenye taarifa za magwiji hawa waliishia wapi?
Mkuu, hiyo michezo nayo ni MIELEKA?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom