Mchezo wa maziwa makuu Magufuli anaujua?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
Ukiacha Kenya, Uganda ,Rwanda na DRC ni nchi ambazo zimekua zikichezeana michezo mibaya sana hadi kufikia kupigana vita kabisa, wanao fuatilia mambo haya wanajua.

M23 imepotea kwa msaada was majeshi toka tz pamoja na kuwa m23 inasemekana inauhusiano na Rwanda,

miaka michache tz na Rwanda tumekua maadui, Leo tumekua marafiki, wiki hii kabila amekutana na kagame pamoja na mseven.

haka kamchezo hakahitaji hasira, mgeni ni magufuli, sijajua atapewa namba gani acheze bila kupewa kadi ya njano kama siyo nyekundu.

Tanzania ina wahutu wengi kuliko watutsi na hao wahutu wanataka madaraka Rwanda.

1471072618025.jpg
 
Yeye mwenyewe ni mzaliwa wa Ukanda huu wa maziwa makuu /kanda ya Ziwa.
Anayetakiwa kufahamu michezo hiyo ni Intergencia ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na yeye kushauriwa tu.
Sidhani mpaka anakuwa Rais wa nchi mambo yote yaliyo na indicators au viashiria fulani fulani na majirani zetu kwamba hafahamu.
Sisi kama watanzania nia na wajibu wetu ni kuwasaidia majirani zetu, wale watakaotuzunguka au kutugeuka kwa maslahi yao binafsi, hakika rungu la Mwenyezi Li juu yao.
 
KYERWA, KAGERA: Watanzania 9 wametekwa kisha kuuawa wakiwa wanavua katika mto Kagera na watu wanaodhaniwa ni askari kutoka Rwanda.
Sidhani kama askari wa Rwanda niwakatili kivile wawakute tu waanze kuwapiga risasi bila hata kuwahoji, inawezekana hawa jamaa walikuwa wanatumika kuvusha magendo kwenda Rwanda au walikuwa ni majambazi.
 
Yawezekana hujui ulisemalo mkuu
 
tatizo refa wa haka kamchezo hayupo east Africa, hata kocha hayupo east Africa, magufuli atafute video za mechi za zamani aone wapi atafiti.
Na kibaya zaidi yeye hataki hata kujua hao marefa na makocha wanaitwa nani. Jambo hilo pengine mbele ya safari linaweza kutuumiza sana. "Hima" guys are not trustiful.
 
Ndio maana tunasema Air Military base ya chato ni muhimu sana kwa usalama wa nchi yetu,
Kwa mfumo wa kijeshi base iliyoko Mwanza inafit kabisa kinachotakiwa ni kuiongezea uwezo. Inaweza Ku cover mipaka yote kuanzia Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi hata mpaka wa DRC.
 
Kwa mfumo wa kijeshi base iliyoko Mwanza inafit kabisa kinachotakiwa ni kuiongezea uwezo. Inaweza Ku cover mipaka yote kuanzia Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi hata mpaka wa DRC.
Mwanza inakuwa international airport, kwa sasa ndege za jeshi na za kiraia zimechanganywa sio salama kiulinzi, ni vyema ndege za jeshi zitafutiwe eneo jingine.
 
Yeye mwenyewe ni mzaliwa wa Ukanda huu wa maziwa makuu /kanda ya Ziwa.
Anayetakiwa kufahamu michezo hiyo ni Intergencia ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na yeye kushauriwa tu.
Sidhani mpaka anakuwa Rais wa nchi mambo yote yaliyo na indicators au viashiria fulani fulani na majirani zetu kwamba hafahamu.
Sisi kama watanzania nia na wajibu wetu ni kuwasaidia majirani zetu, wale watakaotuzunguka au kutugeuka kwa maslahi yao binafsi, hakika rungu la Mwenyezi Li juu yao.
Tatizo ni kwamba sisi si watafutaji. Sisi ni watu wa maneno, ndiyo maana wenzetu wanatucheka umasikini. Kuna jambo moja lililo njiani. Mpambano wa jumuiya ya madola na nchj za francofone
 
Back
Top Bottom