Mchezo wa African Lyon vs Simba kupigwa Taifa badala ya Sheikh Amri Abeid Arusha

Luvanga1

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,777
2,000
Klabu ya African Lyon imeiandikia barua bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) kuomba mchezo wao namba 271 dhidi ya Simba SC uhamishiwe Dar es Salaam.

Lyon wamefikia maamuzi hayo ambapo awali walikuwa wanatumia Uwanja Sheikh Amri Abeid Arusha kwa mechi za nyumbani.

Mwanzoni Lyon waliandika Barua kuomba mechi zao za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe Sheikh Amri Abeid Arusha na Bodi ya ligi ilibariki maabadiliko hayo.

Taarifa imesema kuwa Lyon inadai mchezo dhidi ya Yanga ambao ulifanyika mkoani Arusha katika dimba la Sheikh Abeid Arusha December 20 na Lyon kufungwa kwa goli moja kwa bila (1-0) walipata hasara kutokana na gharama za kambi.

Ukiachana na kambi, gharama za usafiri na pia makato mbalimbali ilikuwa hasara kwao ndiyo maana wameomba mchezo wao dhidi ya Simba ambao utachezwa February 19 ufanyike katika dimba la Taifa, Dar es Salaam.

Source: Saleh Jembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,121
2,000
Walitaka yanga apoteze mchezo mkoani na hilo halikutimia, wampeleke na mnyama akahangaike. Walipokuwa wanaomba hawakujua kuwa lazima ghalama hizo zitakuwepo? Ombi lao litupiliwe mbali mpaka ligi iishe.

Barafu la moto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom