mchezo mchafu wa Kufoji barua yenye nembo ya Chadema, makada wa CCM hautasaidia Arumeru East !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mchezo mchafu wa Kufoji barua yenye nembo ya Chadema, makada wa CCM hautasaidia Arumeru East !!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by JOB SEEKER, Mar 24, 2012.

 1. JOB SEEKER

  JOB SEEKER Senior Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alilalamikia kile alichodai kuwa ni kuchezewa mchezo mchafu na makada wa CCM.

  Malalamiko ya Dk Slaa yanatokana na kusambazwa barua yenye nembo ya Chadema ambayo ina maneno ya kashfa dhidi ya Meneja Mwenza wa kampeni wa chama hicho, Vincent Nyerere.

  Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Nkoanekoli, Kata ya Nkoaranga, Kikwe na Akheri, Dk Slaa alisema amesikitishwa na barua hiyo iliyosambazwa usiku wa manane maeneo ya Tengeru na Leganga.

  “Barua hii inaonyesha kama imeandikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe lakini cha ajabu jina langu limekosewa limeandikwa Silaha wakati siitwi hivyo na imeghushiwa nembo na kumbukumbu ya chama changu. Huu ni wizi ambao haukubaliki hata kisheria,” alisema Dk Slaa.

  Akinukuu barua hiyo, Dk Slaa alisema maneno yake yanamshauri kuachana na Vicent Nyerere kwa sababu amemchafua Mkapa, anayeheshimika Meru na nchi nzima, hivyo hali hiyo itasababisha kukosa kura Meru.

  “Sisi tumechukua barua hizi na nakala tumepeleka polisi na namtaka Isaya Mngulu amtafute mhusika wa barua hii ili ashughulikiwe kwa sababu kughushi nembo ni kosa kisheria na njia za kumpata ni rahisi sababu anatafutwa hata kwa njia ya kompyuta,” alisema.

  Dk Slaa alisema kuwa ugomvi wake siyo kukosewa jina lake wala kumchafua Nyerere, sababu watake wasitake Nyerere ni mtoto wa baba mkubwa wa marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakuna uhusiano na uchaguzi huo.

  Alisema ugomvi wake ni kughushi nembo hiyo ya chama na amegundua imeghushiwa baada ya kuwasiliana na Zitto ambaye alikana kuandika barua hiyo wala kuifahamu.

  Zitto akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana pia alikana kuitambua barua hiyo.

  SOURCE : Mwananchi
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  CCM ni sawa na mfa maji. lazima atajikanyaga sana
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Waliofoji hiyo document wameharibu, hilo ni kosa baya sana, shauri yao.
   
 4. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mfa maji haishi kutapatapa.
   
 5. Non stop

  Non stop Senior Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Magamba maji yamewafika shingoni mpaka wanaanza kutumia njia chafu na haramu.
  Huu ni mwanzo tu tutasikia mengine mengi tu.
   
 6. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  magamba watahangaika sana, vipi ile ya tindikali naona imewa-cost sana wameamua kubadili style, mpaka leo bado wanamlipia gharama za matibabu yule jamaa na wameona wameshtukiwa kuwa walimwagia wenyewe na cyo chadema. kweli ccm wauwaji
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  copy lazima iende tume ya uchaguzi, Mkapa ajadharirishwa bali amejidhalilisha mwenyewe kwa kuongea uongo hadharani na hivyo kuumbuliwa.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Na wewe umeliona hilo?. CCM ya sasa imekuwa kama genge la wavuta bangi. Wanafanya mambo bila kufikiria madhara yake kwao na Taifa kwa ujumla. Hivi hawa vijana hawajui maana ya public trust?, je ikitokea in the future wakaoneshwa jinsi gani wanavyobadili taaruma ya kuiba kwa kushushi walikokuzoea katika siasa watakuwa na hoja?.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwani ni siri kwamba alichokifanya Vicent hakikubaliki kwa watu wuangwana wote bila kujali ni CHADEMA. CHADEMA bwana wajanja sana wameamua kujiandikia barua hiyo ili kuwasingizia watu wengine wakiwa na lengo la kummaliza ZITTO ambaye anayeonekana kuwa tishio katika CHADEMA. kwa nini akimbilie kutambua kuwa kuwa jina lake limekosewa? Tutajuaje kama yeye mwenyewe ndiye amelifanyia editting jina hilo? kuhusu technolojia ya Computer kweli SLAA ni mweupe na pengine anachojua zaidi ni kusoma e-mail yake pekee. Hivi kama bauara hiyo mtu kaichapa kwenye computer yake na kui-print kwenye printer yake mwenyewe tena ambayo siyo networked , Polisi watampataje? teh teh teh teh au anataka kujenga mazingira ya kutaka kuwaeleza POLISI kuwa anajua sehemu ilipochapishwa wakati kumbe mhusika mkuu ni yeye mwenyewe. ZITTO taka a note, SLAA na MBOWE hawakutakii mema.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mimi naona bora maghamba, CHADEMA sasa wanabadilishwa kuwa MAGOME kwa sababu hata jambo ambalo VIONGOZI wa CHADEMA wenyewe wanasigishana wanaliona ni bora na kusema ni Maghamba, hii i ahuweni sana kwa Maghamba kwani mwisho wake ni CDM kufia mbali kwa sababu cdm WENYEWE wanajuana kuwa hawpikiki chungu kimoja jambo ambalo siku itakapotimia ukweli utawekwa wazi na wao wenyewe.
   
 11. p

  politiki JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwenye red hakikubaliki kwa watu waungwana hao unaosema ni wakina nani hao ?? vipi kitendo cha BWM kumdharirisha vicent kinakubalika??

  kuhusu technology slaa siyo mjinga bali WEWE(THATHA)ndio mjinga ni kwamba printer zote zina serial number unapokwenda kutoa photocopy au ku print kitu mashine zinaacha serial number amabayo wataalam wa uchunguzi wanaweza kuyaona maandishi hayo kwenye karatasi hiyo ingawa huwezi kuyaona kwa kutumia macho ya kawaida ha hiyo ilibidi ifanyike hivyohuko nchi za ulaya na usa kwa ajili ya kuwapata watu waliokuwa wakiandika barua za vitisho au kufoji documents kama wanavyofanya CCM. na pia kwenye computer aliyotumia lazima kuna info. atakuwa ameziacha kwenye hard drive kama vile alipokuwa aki copy nembo ya chadema lazima atakuwa aliingia kwenye internet hivyo ni rahisi kuvuta mafaili yote aliyotembelea kwa ajili ya ku engineer plan yake.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nina uhakika POLISI wakitulia katika uchunguzi wao, huo utakuwa mwisho wa CHADEMA kwani wataumbuka ile mbaya.
  Matukio mengi yanaonesha CDMA huwa wanasababisha halafu wanatanguliza kuwaeleza wananchi kuwa ni CCM
  • Walimwagia mtu tindikali kule Igunga wakasema ni CCM;
  • Wamekuwa ni wazuri sana wa kuwaua wapiganaji walioonekana kwenda kinyume na matakwa yao kwa, hayo hawasemi, hapa Tarime na kule Morogoro CHADEMA hawatakaa waeleweke hata siku moja;
  • Wamekuwa ni wezi wazuri tu wakura huku wakitanguliza kusema wamegungua njama za ccm , na kwa nini siku zote SLAA ndiyo anagundua chama? yeye ni Padre? Katibu Mkuu wa CDM ? au ni Mpelelezi? propaganda hizo na wananchi tumezishtukia.
  • Wamekuwa wazuri sana wa kutanguliza kauli za kutotambua matokeo kabla hata kura hazijapigwa, kwa nini wanaingia kwenye king'ang'anyiro kama hawako tayari kutambua matokeo?
  • Wamekuwa wa kwanza kupeleka vijana kupiga kura hata kama siyo wa jimbo husika kama walivyofanya Igunga na ndiyo maana wamekuwa wakipigia upatu watu waliopoteza shahada zao waruhusiwe kupiga kura ili na mamluki wao watumie fursa hiyo.
  Hivi wakisuguana wenyewe bila kuhusisha Maghamba malengo yao hayatatimia? Mbona maghamba wao ni wao kwa wao na hawamtafuti mchawi toka CDM, CUF au NCCR?. Mimi naamini CHADEMA inastahili vijana kama ambavyo wapenzi wake ni Vijana, Lazima wakubali ZITTO, MNYIKA, MDEE na wengine ndo washike hatamu badala ya kuwaachia SLAA na MBOWE ambao siasa zao ni za maji taka na ndiko walikokulia. Narudia , haiwezeani kila njama zinazogunduliwa za kutaka kukihujumu CDM lazima zidunguliwe na SLAA kwani hakuna wengine? hizi ni siasa za maji taka na sababun kubwa ya hili ni uzee na ndiyo maana anasema POLISI wanaweza kumpata mtu aliyeandika barua anaweza kupatikana kwa njia ya Computer. Uwezo kwa kuchanganua mambo sasa unakuwa bounded na Umri.
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumekucha cdm, vita ya urais mmeisha anza kutafunana wenyewe kwa wenyewe, waacheni wafu wawazike wafu wenzao, ngoja sie tucheze ndombolo km hivi:lock1:
   
 14. M

  MSEMEA JAMVINI Member

  #14
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nakipenda chadema lakini kuna mambo wanayofanya yanaboa kiukweli, najua kabisa siasa za chadema ngoja muone mwisho ..kama hiyo barua inaukweli na madai yaliyotolewa ni vyema siasa zetu bongo tukazireebisha sio kujitengenezea matatizo halafu kuja kusingizia mtu au watu fulani.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Yaani afadhali hata aliyoyasema SLAA kuliko wewe. Nakwambia wewe ni mweupe sana,,ok sasa umegungua hizo serial naamba na mtu anayo kwake utamtambuaje? eti hata nchi za ulaya wanafanya hivyo, achana na mambo unayosikia kwenye habari nyepesi nyepesi siku ya jumamosi BBC unaanza kutudanganya humu. Unachoweza kufanya ndugu yangu siyo habari ya Seriala namba bali kama hiyo printer ina memory unaweza kupata hiyo document tena endapo tu hazikuwa deleted.
  Zaidi yote uliosema ni utumbo mtupu kama Computer na Printer haziko kwenye network. Suala la hard drive hpa halina nafasi, nina wasi wasi kama unajua hata hard drive nini sasa kama hard drive ni external na anatembea nayo? Kasome vizuri hiyo short course yako ya miezi sita haujaiva, naona sasa umemaliza Somo la Computer part na sasa labda unahamia kwenye Storage devices ndiyo maana unajaribu kujikumbushia kile ulichosoma jana, je umesoma mambo floppy disk, flash disk na storage devices zingine? Kma wewe ndiye msemaji wa CDMA katika masuala ya Computer wamekwisha.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CHADEMA wenyewe hao.
   
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  This remind me kule Igunga, ninaona this time wamejaribu ku-improve strategy.

  Igunga CCM walichoma banda la kuku la mwanachama mwenzao, halafu kwenye banda hilo kukaokotwa karatasi ambao haikungua moto iliyosomeka hivi. SISI CHADEMA NDIYO TUMECHOMA BANDA LAKO.

  To make the STORY more exciting katibu mkuu wa CCM Wilson Mkama ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kufika ktk tukio, na pia hakuna kuku hata mmoja katika banda hilo aliyekufa kwa kuungua.

  Hayo yote yanaashiri nini? CCM imefikia mwisho, I'm sure ukichukua finger prints za hiyo barua utakuta finger prints za Mwigulu Nchemba.
   
 18. y

  yplus Senior Member

  #18
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma koment yako,Naomba nikujulishe kitu.Unavyoona Dr W.Slaa analipua kila mbinu chafu za CCM haimaanishi kwamba yeye ndio mgunduzi.Elewa kwamba ndani ya CCM kuna wana CDM zaidi ya unavyofikiria na wameshika nyadhifa za juu sana.Hao ndio mtaji wa CDM,ukitaka kujua.Dr Slaa ana Research moja nyeti sana kuhusu mitakabari wa CCM,hiyo Report ni confidencial ndani ya CCM na ninauhakikaa sio wana CCM wote wanaijua ila Dr W.Slaa anayo na ameisoma baadhi ya mambo yaliyoandikwa alipokuwa anamuombea kura Kijana Josh Makumira kijijini.
  Unatakiwa kujua kuwa kuna wana CCM na wenye CCM,ila kwa upande wa CDM kuna wana CDM tu,CDM ni chama cha wananchi,hata wana CCM pia CDM ni chama chao ndio maana wanachukua hela CCM wanapeleka CDM...
   
 19. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  siasa mchezo mchafu.
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM asanteni saaaaaaaaaaaana kwa kutusaidia kukitangaza chama chetu CHADEMA kuwa ndicho tishio pekee kwenu nyinyi kampuni ya kifisadi mnaodidimiza maendeleo ya nchi.
   
Loading...