Mchezo mchafu wa CCM uandikishaji wapiga kura Magadirisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchezo mchafu wa CCM uandikishaji wapiga kura Magadirisho

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Emashilla, Oct 22, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la kushangaza lilikuwa ni kulazimisha vijana wasijiandikishe kwa visingizio vya umri kama vile CCM ndio mama na baba wa Vijana wa Magadirisho. Mama mmoja amelalamikia kitendo cha Kada mmoja wa CCM kumsumbua kijana wake mwenye umri wa miaka 18. Alimtaja kada huyu kwa jian la mama Happy. Kijana aliandikishwa lakini jambo hili limechochea moto wa vijana na wazee kuikataa CCM na kusikika wakisema, "CCM INABAGUA WATU" Hii ilitokea siku ya pili ya uandikishaji.
  Pia,Askari mgambo watumiwa na CCM kuvuruga taratibu za uandikishaji wapiga kura katika kituo C hapa ,Jumamosi 20/10/2012,. Makamanda wa Chadema waliwafukuza mgambo baada ya mabishano ya muda mrefu wa kisheria na uhalali wa askari mgambo kutishia wakazi wanaotaka kujiandikisha. Viongozi wa CCM tawi la Magadirisho waliwaweka mgambo wa tatu ambao wengine waliwapa cheo cha mabalozi wa nyumba kumi(CCM). Watu hawa walikuwa wakiwalazimisha Vijana na watu waliokuja kujiandikisha kutaja majina matatu ya mabalozi wa CCM na walioshindwa walizuiliwa kujiandikisha kuwa wapiga kura.Wengine walilatakiwa kumuona wakala wa CCM ambaye alikuwa na karatasi yenye majina ya mabalozi wa CCM na kupangiwa au kupewa jina la balozi wake. Mbali na hilo walikuwa wakiwataka watu kutii amri zao kabla ya kumuona mwandikishaji wapiga kura. Chadema Magadirishoa ilichukuwa hatua ya kuwafukuza maharamia hawa wa demokrasia na mafisadi na kupeleka taarifa kwa wasimamizi wa uchaguzi. Baada ya sekeseke hilo lililotokea siku ya Jumamosi kwa muda. Lakini uandikishaji haukuendelea kwa muda mrefu kwa sababu waandikishaji walitakiwa kwenda semina na kuapishwa katika ofisi ya mamlaka ya mji mdogo wa Usa-River iliyopo hapa Magadirisho.
  Vituo vya uandikishaji kwa eneo hili ni kama ifuatavyo:
  (1) Ofisi ya Mamlaka ya Mji Mdogo Usa-River;
  (2) Shule ya Msingi Usa-River;
  (3) Tumaini Children's Foundation Centre , barabara ya Dik Dik;
  (4) Kituo cha Kuosha Magari{Car Wash}, Kwa Tarimo barabara
  ya Momella;
  (5) Kwa Waree, Karibu na kanisa katoliki Magadirisho, na
  (6) Ofisi ya Kitongoji

  MUDA WA KUJIANDIKISHA UMEONGEZWA HADI ALHAMISI

  Zoezi la uandikishaji liliaendelea jana na pia muda wa uandikishaji umeongezwa hadi Alhamisi tarehe 25 Oktoba,2012.
  Siku zimeongezwa baada ya Chadema na wananchi wa kata ya Usa-River kuomba muda uongezwe ili kutoa fursa ya watu wengi kujiandikisha. Ombi hili lilikuja baada ya zoezi la uandikishaji kuanza saa nane mchana siku ya kwanza(yaani 17/10/2012) badala ya muda wa saa moja nanusu kama ilivyopangwa. Vituo vingine vilishindwa kuanza kazi kutokana na kutokuwa na vifaa au waandikishaji wapiga kura kutokuwepo na vituo vingine havikuwepo kabisa. Vile vile Jumamosi mchana majira ya saa sita mchana uandikishaji uliahirishwa hadi siku inayofuata kama ilivyoelezwa hapo awali.
   
 2. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hivi nyinyiem bado hawajui kuwa hawahitajiki, wala hawakubaliki hata kidogo? Kukubalika kwa jiwe > kukubalika kwa nyinyiem
   
 3. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wananchi sasa hivi naona wanajua umuhimu wa kupiga kura,CCM na ghiriba zao itabidi waje na mbinu mpya sijui ipi itakayokubaliwa na wananchi
   
 4. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yaani umenichefua na hiyo thread yako,yani unatuletea mambo ya kufikirika kama ulishindwa ni wewe hukohuko nonsense.pusiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
   
 5. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unahitaji matibabu maalum. Hapa hakuna kufikirika bali ni ukweli mtupu kuhusu Chama chenye rushwa kila kona wala si kingine bali ni CCM. Hujachefuka vizuri kwani huu ni wakati wa kutapika. Hakuna aliyeshindwa bali wameabika hao rafiki zako wa hukuhuku.
   
Loading...