Mchezo mchafu unaofanywa na benki kuwapora wateja pesa zao

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
111
500
Habari zenu ndugu zangu
Naomba kushea na nyie jambo hili

Leo nilikuwa Mahakamani kwa ajili ya shughuli zangu nikakutana na mama mmoja anafuatilia mirathi ya mumewe. Katika mazungumzo yetu akanidokeza jambo moja ambalo nimeshangaa sana.

Anasema baada ya shauri la mirathi kuisha alipewa barua inayomtambulisha kua msimamizi ili akafatilie pesa na mambo mengine

Mumewe alikuwa ni mfanyakazi wa umoja wa mataifa UN.

Alianza na benki aliokuwa anachukulia mshahara mumewe.

Alivyofika baada ya kuwaonesha document walimwambia angoje kidogo wafanyie kazi.

Baada ya muda kidogo wakamuita na kumpa bank statement ambayo alitakiwa apeleke Mahakamani

Bank statement ilionesha account ilikuwa na laki moja na sent kiasi
Akaondoka mpaka Mahakamani na kukabidhi bank statement kwa karani
Anasema karani hakuwa na imani na kiasi cha pesa kilichopo kwenye account ya marehemu kwa sababu document zilionesha alikuwa analipwa milioni 2 kwa mwezi

Karani wa mahakama ikabidi apige simu benki na kuhoji maswali kadhaa kuhusu utata huo
Benki walimjibu kwamba walikosea na kwamba taarifa sahihi account ina milioni mbili na point

Inavyoonekana huu mchezo benki wanaucheza sana.

Fikiria wangapi wamedhulumiwa kwa mtindo kama huu
😡
 
mputa

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
1,170
2,000
Mimi ilinitokea, nilipekeka 300,000/= kwenye a/c yangu, iligongwa mihuri yote na sahihi ya mpokeaji( huyo dada namfahamu kwa sura, kwa kua nina mazoea ya kwenda hiyo bank. Cha ajabu siku nakwenda ku withdraw pesaATM inanimbi insufficient fund, nikaangalia bal nikakuta wameniwekea 30,000/ nilifuatilia kwa branch manager, yule dada aliitwa (aliyezipokea) nikaambiwa baada ya nusu saa niangalie bal nitakuta imerekebishwa, na kweli ikawa hivyo. Wizi upo sana kwenye bank
 
Aisee huu usanii sijui unazibitikaje hawa watu wana umiza sana
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,132
2,000
Mimi ilinitokea, nilipekeka 300,000/= kwenye a/c yangu, iligongwa mihuri yote na sahihi ya mpokeaji( huyo dada namfahamu kwa sura, kwa kua nina mazoea ya kwenda hiyo bank. Cha ajabu siku nakwenda ku withdraw pesaATM inanimbi insufficient fund, nikaangalia bal nikakuta wameniwekea 30,000/ nilifuatilia kwa branch manager, yule dada aliitwa (aliyezipokea) nikaambiwa baada ya nusu saa niangalie bal nitakuta imerekebishwa, na kweli ikawa hivyo. Wizi upo sana kwenye bank
Hii nilikutana nayo nilikuwa Kila nikipeleka pesa Bank naandika na slip natunza kwenye faili Sasa nikapiga hasabu nikataka Sasa nikadraw kiasi kingi nafika bank wananiambia salio halitoshi ,nikawaambia Basi tusitishe ,nikarudi ofisini nikachukua silp zote na kitabu kwenda moja kwa moja kwa branch manager tukapiga naye hesabu
 
Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
17,116
2,000
Huko kwenye dollar asikwambie mtu wanafyeka utazani anayeziweka humo huwa wanamsaidia, mie mpaka nilikuwa nawauliza mbona nilipotoa nyingine ilibaki balance ambayo nyingine ikiingia nisikatwe pesa nyingi? Wanakupiga Kiswahili hicho, sahizi hata Card yao sijui iko wapi!
 
Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
8,197
2,000
Hii nilikutana nayo nilikuwa Kila nikipeleka pesa Bank naandika na slip natunza kwenye faili Sasa nikapiga hasabu nikataka Sasa nikadraw kiasi kingi nafika bank wananiambia salio halitoshi ,nikawaambia Basi tusitishe ,nikarudi ofisini nikachukua silp zote na kitabu kwenda moja kwa moja kwa branch manager tukapiga naye hesabu
Bank wahuni sana. Mwaka jana mwanzoni nilienda kuweka 1.3M kwenye account yangu ya NMB. Tukahesabu fresh, then baada ya kumaliza nikasepa.

Baadae yule teller wakati anafunga mahesabu, akawa inapelea laki 1. Kila akijaribu kuangalia ile loss inatokea wapi, hapati jibu. Mwisho wa siku akapitisha wazo kuwa mimi hela niliyopeleka ilikuwa 1.2M na sio 1.3M. Akajaribu kunipigia simu, sikuwa hewani. Kwavile alikuwa anataka kufunga hesabu, akaandika slip mpya, inayoonesha nimeweka 1.2M then akafoji sahihi yangu. Kwakifupi akatoa laki moja kwenye account yangu.

Nilipopata ujumbe baada ya kuwasha simu kuwa alinitafuta , ikabidi kesho yake mapema niende.Kufika pale ananipa slip aliyojaza yeye akisema tulikosea kuhesabu. Nikamwambia labda ukosee wewe, zile hela nilihesabu kabla sijatoka home. Tukabishana sana hadi kwenda kwa Manager. Yule teller anakomaa kuwa hata kwenye camera zimeonesha kuwa mimi na yeye tulikosea kuhesabu. Vutana sana pale, baadae kuna mmama mmoja nae ni mfanyakazi pale ndio akamuita ndani. Yule mama akamuonesha kosa lilipotokea, kumbe baada ya mimi kuondoka, kuna mtu alikuja na kutoa elfu 50, ila yeye akamuandakia kaweka elfu 50, it means loss ikajidouble.

Baada ya hapo jamaa akaniomba sana msamaha, mpaka natoka getini jamaa yupo ananiomba msamaha tu. Siku hiyo ndio nikajua kumbe bank inaweza kutoa hela kwenye account yako na usiletewe ujumbe.

Wezi sana.
 
Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
111
500
Duu

Du Aisee ulikomaa mzee sasa sijui huyo maza asingemshtua ingekuaje
 
Nguseroh

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
1,645

Mkuu si unapotezea tu kwani na wewe huibi katika nafasi yako? Huko ofisini hupigi panga? Kila mtu bongo ni mwizi katika nafasi yake. Ukiibiwa potezea tu. Cha kufariji huyo aliyekuubia naye atalizwa na aliyemliza naye atalizwa karma ipo kwa iyo usijali songa mbele
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom