Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Zana Oumar Coulibaly, wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast amewasili nchini Tanzania kukamilisha taratibu za mwisho za kujiunga na Simba SC
Coulibaly ambaye ni beki mwenye uwezo uwanjani msimu uliopita alitumikia ASEC Mimosas katika michuano Kombe la Shirikisho Afrika, punde tu baada ya kuwasili nchini alikwenda uwanja wa Taifa kushuhudia Simba ikitakata kwa ushindi mnono wa mbao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows katika mchezo wa ligi ya mabingwa.
Zana Coulibaly, anacheza nafasi ya ulinzi upande wa kulia anakuja kuziba nafasi ya Shomari Kapombe ambaye amepata majeraha ya kuumia mguu akiwa kambini Afrika Kusini wakati timu ya Tanzania Taifa Stars ikijiandaa kupapana na timu ya Taifa ya Lesotho.
=====
Mchezaji Zana Coulibaly raia wa Burkina Faso, aliyekuwa akichezea ASEC Mimosas, amesajiliwa na klabu ya Simba baada kukamilika kwa vipimo vya afya Jana.
Leo, Novemba 30, 2018 Zana amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba mbele ya Mkurugenzi Mkuu (CEO) Crescentius Magori, huku akikabidhiwa jezi namba 21.