Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,984
MABULA (KULIA) AKIPAMBANA NA IDDI MOSHI WA YANGA KATIKA MICHUANO YA TUSKER KWENYE UWANJA WA TAIFA (SASA UHURU) MWAKA 2000).
Taarifa ya msiba, inaeleza beki wa zamani wa Shinyanga Shooting na Mtibwa Sugar, John Mabula amefariki dunia.
Inaelezwa Mabula aliyekuwa mtaratibu sana ameuwawa kwa kuchomwa kisu katika eneo la Kitunda jijini Dar es Salaam na muuaji wake amekimbia, sasa anasakwa na polisi.
Taarifa kutoka kwa jirani yake zinaeleza, mshambuliaji huyo amemuua Mabula ambaye alikwenda kuamua shemeji yake asishambuliwe.
Lakini baadaye akamuua na shemeji yake huyo kabla ya kumshambulia mkewe na kukimbia kusikojulikana.
Mabula alichipukia kisoka mkoani Shinyanga akiichezea Majengo kabla ya kujulikana hadi kuchukuliwa na Mtibwa Sugar aliyoichezea kwa ufanisi mkubwa.
Bado tunaendelea kufuatilia na tutawaletea taarifa zaidi.