- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Thomas Lungu Sweswe ni mchezaji wa zamani wa Zimbabwe, beki wa kati anadaiwa kushikiria rekodi ya kucheza dakika 90 dhidi ya Keiza Chiefs bila kugusa mpira.
- Tunachokijua
- Kwa mujibu wa Mwandishi Oladele Emmanuel wa nigfooty.com anaeleza kuwa alifanya jitihada za kumtafuta mchezaji huo na kufanya naye mahojiano ili kupata ukweli wa madai ya yeye kucheza dakika 90 bila kugusa mpira.
Beki huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 38 aliiambia nigfooty.com kwamba habari hizo si za kweli na zaidi alisema yeyote aliyepika hadithi hiyo ana ajenda yake binafsi ya kumchafua.
Sweswe anasema "huo ni uwongo, hata kama una siku mbaya mchezoni kiasi gani hakuna namna jambo hili linaweza kutokea. Haiwezekani mchezaji yoyote anayecheza soka la ushindani kucheza dakika 90 bila kugusa mpira".
"Aliyekuwa nyuma ya jambo hili ni mtu mwenye ajenda binafsi, sijui kwanini hakutaja jambo hili wakati ule niliocheza mpira na akaja na hadithi hiyo wakati huu. Siku zote mimi hucheka wakati watu wengi hunitumia ujumbe wakiuliza ikiwa ni kweli nilicheza dakika 90 zote bila kugusa mpira.
Sasa nimerejea nyumbani Zimbabwe nikifanya kazi kama Katibu Mkuu wa Muungano wa Wanasoka wa Zimbabwe" Thomas Langu Sweswe aliongeza.
Zaidi ya hayo, JamiiForums imefanya mawasiliano na Sweswe ili kuthibitisha habari hii ambapo Sweswe alieleza
"Taarifa hizo ni za Uzushi zinaenezwa na mtu mwenye ajenda binafsi, mwenye nia ya kunichafua. Ukitazama habari hiyo na tarehe inayodaiwa nilicheza bila kugusa mpira nilikuwa tayari nimeshastafu kucheza soka. Pia taarifa hiyo haielezi mechi hiyo nilicheza dhidi ya timu gani na ilikuwa kiwanja gani."
Hivyo, kutokana na ufafanuzi huu kutoka kwa Thomas Sweswe na kukosekana ushahidi wa jambo hili JamiiForums inapata shaka ya rekodi hii kuwa na ukweli.