Mchezaji gani aliyestafu ungependa arudi uwanjani

Mkuu flying dutchman alikua ni Mack Overmass, kama niko sahihi
Uko sahihi kiongozi. Bergkamp pamoja na ufundi wake alikuwa anaogopa kupanda ndege.

Ila lile bao lake dhidi ya Argentina kwenye World Cup ya mwaka 1998 pale Ufaransa limebaki kwenye historia ya magoli bora kuwahi kufungwa kwenye WC.

Commentator anakwambia, " Three touches, Control, Turn and Finish " alimwacha Beki Roberto Ayala akishindwa kugeuka.
 
Uko sahihi kiongozi. Bergkamp pamoja na ufundi wake alikuwa anaogopa kupanda ndege.

Ila lile bao lake dhidi ya Argentina kwenye World Cup ya mwaka 1998 pale Ufaransa limebaki kwenye historia ya magoli bora kuwahi kufungwa kwenye WC.

Commentator anakwambia, " Three touches, Control, Turn and Finish " alimwacha Beki Roberto Ayala akishindwa kugeuka.
Lile lilikua kiboko mno kwenye world cup, lakini goli langu bora ni lile alilowapiga New Castle kwenye epl
 
Ricardo Kaká huyu namwangalia anachipukia hadi anakuja kuvuruga kutransfer to madrid
akiwa mdogo kaka anamanage kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu akiwa na nguli wenye umri mkubwa kama carlos, maldin, Cafu, Crespo, Schevichenko, Nedved, na wengineo vijana wa siku hizi hichi kitu kinawashinda
Mchezaji wangu Bora wa muda wote Ricardo Kaka

96deb62abfa008fb2e8270da9a08c217.jpg

Anaitwa Ricardo Izecson dos Santos Leite alimaarufu kama KAKA.

Moja wapo ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu kabisa kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa soka.

Katika timu zote alizochezea amecheza kama kiungo mshambuliaji na mchango wake ulionekana sana, nakumbuka UCL ya 2005 second half, midfield ya Ac millan yote ilipotea ila yeye pekee tu ndio alionekana kuwa hai na isingekuwa schevichenko kupoteza pasi zake mbili za mwisho kwenye extra time yeye ndio angekuwa man of the match wa siku hiyo.

Kwenye fainali ya confederation cup 2009 mimi ni mmoja wapo ya watu waliompa KAKA cheo cha ubrigedia generali wa mpira wa miguu.
 
El phenomenon. Ronaldo orijino alipiga goli 47 katka mechi 48 akiwa na Barca msimu mmoja tu.

Pia alipokuwa PSV Eindhoven msimu wake wa kwanza kabla hajapata injury alipiga goli 12 kati ya game 13, vile vile aliporudi msimu wa pili akiwa fiti alifunga goli 54 kati ya mechi 58 alizocheza msimu mzima.

Hata alipochukua tuzo ya pichich akiwa na barca alifunga goli 34 kati ya mechi 37 alizocheze za laliga.

Timu ya Taifa ya brazil ana goli 62 kati ya mechi 98 alizochezea.

Ebana kuna watu walizaliwa kufunga acha tu, sio akina geroud wanaocheza dakika 700+ alafu goli 5 tu.
 
Mkuu huyo davo suker alipata tu kiki ile world cup na kuwa top scorrer yani ni kama man fongo na haina ushemeji.

Apart from ile world cup ya 2002 kama sikosei sidhani kama alisikika tena. Huyu ni kama James Rodriguez alivyopata ngekewa world cup 2014 but sa hivi kapotea pale madrid
Umenena mkuu, lakini Davo suker aliwahi kuingia kwenye shortlist ya Fifa player of the year mwaka 2000 nafikiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom