Mchezaji alimwa red card huko America ya Kusini kwa kumjambia Refarii!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Katika hali ya kushangaza kabisa ambayo imewaacha Watu hoi jana katika moja ya mechi za Ndondo huko nchini Colombia mchezaji mmoja alishindwa kujizuia na katika harakati za kutaka kuuzuia mpira gambani ( kifuani ) akajikuta anajamba hali ambayo ilimkawaza sana Mwamuzi ( Refarii ) na kumtoa nje kwa kumpa Kadi nyekundu.

Alipohojiwa mara baada ya kumalizika kwa huo mchezo Mwamuzi huyo alisema kuwa aliamua kumpa kadi nyekundu ( red card ) huyo mchezaji hasa hasa kwa kitendo chake cha kujamba kwa sauti kubwa. " Najua kuwa hali ya kujamba muda mwingine huwa inakuja bila hodi au kukusudia ila kwa huyu Mchezaji siamini kama kweli ilikuwa ni bahati mbaya kwani hata aliponijambia mbele yangu hakuonekana kujali na badala yake alikuwa anacheka tu ndipo nikaona nimpe kadi nyekundu ili akamalizie vizuri huko kujamba kwake jukwaani kwani hewa ilibadilika kabisa pale uwanjani hadi nikawa nashindwa kupumua na kupuliza filimbi vizuri " alisema huyo Refarii.

Je Marefarii wetu akina Israel Nkongo, Chang'walu na Othman Kazi na wao huwa labda wanakumbana na kadhia hii kutoka kwa Wachezaji wetu wa Kibongo ambao hata vyakula vyao tu vingi wanavyokula ni " mitambo " au " vichocheo " tosha vya kujamba.

Nitashukuru na itapendeza kama na wao wakitoa hapa ushuhuda wao ila mwenzao wa nchini Colombia uvumilivu wa kujambiwa ulimshinda na akampa mtu " umeme ".
 
Hahahaaa leo nimecheka aisee..mi navyojua wazungu huwa wanapenda kuona mtu akijamba kuliko kubezuka au sio ivo?
 
Back
Top Bottom