Mcheza Mpira Victor Wanyama, apewa jina la mtaa jiji Dar, Meya atoa ufafanuzi

Mkuu soma basi barua kabla ya kububujikwa povu,umeona mkono wa Chadema hapo,angalia hata nakala za barua zilikoenda,barua imeandikwa na CCM na imenakiliwa kwa CCM,hata meya hajanakiliwa,unatulaumuje sisi
Sijaona palipoandikwa CCM isipokuwa barua inatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo huku ikiwa imesainiwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa na Mwenyekiti wa Mtaa!!

Sasa tuanzie hapo: Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inaongozwa na CCM au CHADEMA?
Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC anatoka CCM au CHADEMA?

NOTE: Ni serikali za mitaa ndizo hutoa majina ya mitaa. Huyo Afisa Mtendaji amesaini kwa sababu tu yeye ndie mwakilishi wa serikalii kwenye mtaa husika!!!
 
Ni kwa heshima ya kwenda Ndondo Cup, Kinesi! Mbona tuna Sam Nujoma roads, Kenyatta Drive etc?? Povu la nini??
Ina hufahamu umuhimu Sam Nujoma na Kenyatta kwa siasa za Afrika?! Mbona hata nje ya Tanzania ipo mitaa yenye majina ya viongozi wa Tanzania kutokana na umuhimu wao kwenye siasa za Afrika!!!

Sasa kama umuhimu wa Victor Wanyama kwenye soka la Tanzania ni kutembelea Ndondo Cup basi kazi ipo!!!
 
Nimejaribu kusoma maoni hapa lakini bado sijaona tatizo au logic ya kupinga, labda kwakuwa ni Meya wa chadema aliyefanikisha hilo kama hilo ndo tatizo, lakini ni jambo la kawaida sana, wapo mnaosema apewe diamond, lunyamila, na wengineo, hivi kwanini apewe diamond kwa kipi hasa alichoifanyia Tanzania kizidi wengine? Na huo mtaa uitwe diamond au Nasaib? Diamond anaimba kitu gani hasa cha kuelimisha jamii hadi kizazi chetu na cha baadae kiige na kuhamasika? Lunyamila na wenzie walifanya kazi kubwa sana kwa wakati wao, kama kuna kitu exceptional wamewahi fanya, watatambuliwa kwa wakati wao, na kwanini iwe lunyamila na isiwe Peter Manyika?? Jamani hawapewi eti kwakua wewe unawapenda, ila kwa kuthamini mchango wao. Kwanini VICTOR WANYAMA amepewa?
1. Itasaidia kumotivate vikana wadogo wawe na kiu ya kufika na kicheza EPL
2. Itamuongezea credit Wanyama na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi ambayo yeye atakua kama ambassador wa vijana kutoka Tanzania
3. Itaitangaza Tanzania kimataifa
4. Itadumisha ushirikiano wa kimichezo kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Mwisho, hilo ni jina tu na heshima yake kukubali kuja Tanzania ku encourage our young people, so he deserves!

Sio tukampe mtaa mtu anayetuharibia watoto wetu kuimba mapenzi tu, mara msambwanda sijui nini, what do they learn from diamond? Kuvaa macheni, hereni, mikufu, au zile suruali zake za kubana? Kama anataka mtaa aombe uongozi wa kule madale aweke jina lake, Shyrose ameweka jina lake mtaani kwake huko mbweni na yeye afanye if that the case!!!
 
Mbona kuna mtaa unaitwa Ngoma

Acheni roho za kwann

Wenye mtaa wamekubali nyie povu za nini

Kwani mmekatazwa kuita mitaa yenu majina ya kibadeni ,kizota ,samatta? Ruksa yaiteni waacheni raia wa kinesi wajiamulie

33aac9218d6ab3224d2b09ab927039ed.jpg
Kuna akina Ngoma wangapi Tanzania?! Kwanini unajaribu kuaminisha kwamba ni Donald Ngoma wakati wamendika Ngoma? Unaweza kutuambia huo mtaa upo wapi kama hatujaona mlengwa hasa ni nani?!
 
Ina hufahamu umuhimu Sam Nujoma na Kenyatta kwa siasa za Afrika?! Mbona hata nje ya Tanzania ipo mitaa yenye majina ya viongozi wa Tanzania kutokana na umuhimu wao kwenye siasa za Afrika!!!

Sasa kama umuhimu wa Victor Wanyama kwenye soka la Tanzania ni kutembelea Ndondo Cup basi kazi ipo!!!
Vizuri, na upande wa michezo tunatambua mtu wa kwanza toka E.A kucheza ulaya na kutamba, ni motivation!
 
Kwangu mimi huo ni upumbavu wa akili!! Who's Victor Wanyama kwenye soka la Tanzania?!

Nani bora kati ya Victor Wanyama na vijana wanaojitoa muhanga uwanjani kupigania taifa lao ambalo hata haliwajali?!

Ni leo tu hapa tumemshuhudia Mwakyembe akimtembelea Nahodha wa Serengeti Boys ambae ameumia lakini TFF imemtelekeza!!

Shame on You CHADEMA!!

I am sure upumbavu kama huo ungefanywa kwenye halmashauri zinazoongozwa na CCM hivi sasa ingekuwa mnamwaga mapovu hapa!!!
Punguza upenzi wa vyama usiwe mfia vyama unaweza ukawa una point nzuri ukiingaza siasa unaiharibu point yako mkuu
 
SI JAMBO LA AJABU MTAA FULANI KUITWA KWA JINA LA MTU FULANI TENA HUKU AFRIKA KUNA MAJINA YA WATU MBALIMBALI KUTOKA AFRIKA NA SEHEMU MBALIMBALI KUTWA KWA MAJINA YA WATU FILANI.

MF, KENYATTA ROAD HAPA TANZANIA,NYERERE ROAD KULE KENYA.
 
Huu ni upuuzi tena wa kiwango cha juu.Ndio shida ya kuwapa uongo watu wasio jua mji vizuri. Mtu ambaye amekuja kwa safari yake binafsi unakurupuka kumpa heshima jina la mtaa. Hivi katika hilo eneo hakuna wazee au watu waliochangia maendeleo mpaka apewe mtu aliyekwenda kuangalia mechi ya ndondo?

Ni ukosefu maamuzi ya busara.
Mkuu nahisi hiyo ni mipango ilishapangwa hicho kitu hakiwezi kuwa cha siku moja
 
Sijaona palipoandikwa CCM isipokuwa barua inatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo huku ikiwa imesainiwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa na Mwenyekiti wa Mtaa!!

Sasa tuanzie hapo: Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inaongozwa na CCM au CHADEMA?
Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC anatoka CCM au CHADEMA?

NOTE: Ni serikali za mitaa ndizo hutoa majina ya mitaa. Huyo Afisa Mtendaji amesaini kwa sababu tu yeye ndie mwakilishi wa serikalii kwenye mtaa husika!!!

Bwana eeeeh na nyinyi mtaa wenu upeni jina la Ally Yanga
 
b978b528c0054b17f3506e6faf0ca897.jpg
Kutokana na heshima aliyo onyesha na nia ya dhati katika kushiriki kuibua Vipaji vya mtaa, manispaa ya Ubungo kupitia Meya Mh, Boniphace jacob imeamua kumpa mtaa, ukiwa legho hotel kama unatokea sinza mkono wa kushoto kama unaenda uwanja wa kinesi ndio huo mtaa aliopewa victor wanyama
 
Back
Top Bottom