Mcheza Mpira Victor Wanyama, apewa jina la mtaa jiji Dar, Meya atoa ufafanuzi

Swedy mussa

Member
Feb 29, 2016
27
45
Jamani wadau hili swala limekaaje wanyama naona kapewa jina la mtaa V. Wanyama street maeneo ya kinesi shekilango wakati Ma legend wa tanzania hapa sijawai kusikia hili swala Au kwa vile anachezea EPL?

Mimi naona kuna haja ya Mitaa wachezaji wakakumbukwa Lunyamila na wengine wengi sababu ni icon ya nchi yetu

Nini maoni yako kuhusu hili
Victor-Wanyama (1).jpg
Screenshot from 2017-06-25 14-03-51.png
Screenshot from 2017-06-25 14-17-04.png


======

Meya atoa Ufafanuzi

======

Tangu jana kutoka habari ya kumpatia Jina la mtaa VICTOR WANYAMA, kata ya Ubungo na mtaa wa Ubungo N.H.C, nimeona kumekuwa na mijadala juu ya hilo, nimeamua nitoe somo juu ya jambo hilo kuepuka kuposhwa na wachambuzi uchwara.

Sheria namba 8 ya mwaka 1982 (sura namba 288) na sheria namba 6 ya mwaka 1999 ,ndiyo inayotoa mamla kwa serikali za mitaa kutunga na kutoa majina ya barabara za ndani ya halmashauri na barabara za mitaani.

*Soma sheria namba 8 ya mwaka 1982(sasa inaitwa sura 288) kifungu cha 55(1)j-to name or re name,where necessary,all streets(such names to be affixed in conspicuous places),and to cause the buildings in such streets to be numbered;*

*TARATIBU ZA KUTOA MAJINA YA MTAA*

Majina ya mtaa yana ngazi kuu tatu ya upatikanaji na upachikaji wa majina, katika mamlaka za serikali za mtaa, majina huanzia kwenye kamati za mtaa ndani ya serikali ya mtaa kwa mamlaka za miji na majiji kisha mapendekezo hayo huenda kamati ya mipango miji na mazingira ngazi ya wilaya na hutoka na azimio la kukubaliwa kwa jina pendekezwa.

Na baadae baraza la madiwani hupokea na kupitisha taarifa ya kamati ya mipango na mazingira.

*NJIA ZA KUOENDEKEZA MAJINA YA MTAA*

1. kwa viongozi wa kuu wa nchi kuleta mapendekezo ya kubadili au kutunga jina la barabara kama wana mgeni wa kitaifa.

2. Kwa mtu kujitolea kuwa mlezi wa barabara mtaani, ipitike vizuri basi huweza pewa jina lake.

3. kwa njia ya asili ya kufuatisha majina ya watu maarufu katika mtaa, mara nyingi hawa huwa hawaombi bali upendekezwa na wananchi.

4. kwa kikao cha kamati ya mtaa au wananchi kukaa na kupendekeza jina mara baada ya kuona wanasababu zao hapo mtaani kwao.

5. kwa kutoa kwa Heshima ya mgeni aliyetembelea mtaani kwao kama kumbukumbu ya mtaa husika na viongozi wake.

*SWALI*

*kwa nini Victor wanyama na siyo samata?*

*JIBU*

Mimi nilipokea ujumbe wa viongozi wa UBUNGO FOOTBALL ASSOCIATION (UFA) mapendekezo ya kuja mtaani kwangu kata ya ubungo siku ya jumamosi ya tarehe 24 June ya kwamba nitapokea ugeni wa wachezaji wa wili kuja mtaani kwetu, wageni waliotarajiwa kupokelewa ni Mbwana Samata wa Tanzania na Victor Wanyama (Kenya) kwa bahati mbaya alikuja mmoja ambaye ni Victor wanyama,ndiyo maana tukio linaonekana ni yeye tu amekabidhiwa jina la mtaa.

*SWALI*

*Je Mbwana Samata akija ubungo mtampatia jina la mtaa*

*JUBU*

Tayari kamati ya mtaa ubungo N.H.C walisha kaa kikao na kukubali kuwapatia wachezaji hawa wa ulaya barabara mbili tofauti, ya Mbwana Samata zamani ilikuwa BENKI STREET(mita 800) na Victor Wanyama zamani iliitwa VIWANDANI STREET(mita 270) ambapo kwenye kikao chao cha mtaa mimi si mjumbe ila nilipendezwa na Idea ya mtaa wa N.H.C na kuwapa full support.

*SWALI*

*Kwa nini Victor Wanyama tu na siyo wanamichezo wengine maarufu wa zamani*

*JIBU*

Mimi ni kiongozi wa ngazi ya wilaya Ubungo na siyo kiongozi wa Kitaifa au Waziri wa michezo hivyo ninayo mamlaka ya kumsaidia mtu kupatiwa jina la mtaa katika ngazi yangu tu ili hao mnao wataja wapate mtaa huku halmashauri ya Ubungo tunawakaribisha waje wapokee barabara za kuzilea na kuzihudumia kama Victor Wanyama.

Pili tulipendezwa na swala la victor kuja mtaani kwetu kutia hamasa vijana wetu wanaochezea ligi ya Ndondo cup, ligi yenye timu zisizo na madaraja rasmi TFF, hasa kipindi hiki cha mapumziko yake binafsi achilia mbali na utajiri wake, lakini akae kutimuliwa vumbi kiwanja cha kinesi, na kuwapa hali na mori vijana wa ubungo wenye ndoto kama yake ya kuchezea ligi za kulipwa ulaya.

Tunatamani wengine waje tuwape hadhi na heshima sawa na ya Victor Aliyo wapatia vijana wa ubungo, sembuse kuita jina la mtaa, tena wenye vumbi.

*Je na wewe unataka jina la mtaa wako?*

Ni rahisi sana chukua jukumu la kuhudumia moja ya barabara za mtaani kwako kisha nenda serikali ya mtaa unapoishi, waombe wakukabidhi rasmi barabara ya mtaa au fanya jambo lenye kuletea heshima na kuitangaza vema ndani na nje ya nchi halmashauri yetu ya Ubungo

*BONIFACE JACOB*
*MSTAHIKI MEYA UBUNGO*

*Senior Councilor*

======

UPDATES;

Baada ya Victor kupewa mtaa, Hatimaye Kibao cha Mtaa kimeondolewa. Zaidi soma=>Meya Ubungo: RC amelazimisha bango la mtaa wa Wanyama kuondolewa, kisa waliomleta ni Clouds Media
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,196
2,000
Anastahili kuenziwa ila imekuja mapema mno ilhali Kuna majina mengi tu ya watanzania waliopata kufanya mambo makubwa hayaenziwi. Ukiachilia mbali wanamichezo mtu kama Dayamondi tayari kafikia legendary status aidha unampenda au humependi ila sijui kama kuna hata choo cha jamii kinaitwa kwa jina lake achilia mbali shule au mtaa.

Tumejipendekeza mno kwa Wanyama hadi aibu wakati yetu hatujamaliza.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,130
2,000
Kwangu mimi huo ni upumbavu wa akili!! Who's Victor Wanyama kwenye soka la Tanzania?!

Nani bora kati ya Victor Wanyama na vijana wanaojitoa muhanga uwanjani kupigania taifa lao ambalo hata haliwajali?!

Ni leo tu hapa tumemshuhudia Mwakyembe akimtembelea Nahodha wa Serengeti Boys ambae ameumia lakini TFF imemtelekeza!!

Shame on You CHADEMA!!

I am sure ujinga kama huu ungefanywa kwenye halmashauri zinazoongozwa na CCM hivi sasa ingekuwa mnamwaga mapovu hapa!!!
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,363
2,000
Huu ni upuuzi tena wa kiwango cha juu.Ndio shida ya kuwapa uongo watu wasio jua mji vizuri. Mtu ambaye amekuja kwa safari yake binafsi unakurupuka kumpa heshima jina la mtaa. Hivi katika hilo eneo hakuna wazee au watu waliochangia maendeleo mpaka apewe mtu aliyekwenda kuangalia mechi ya ndondo?

Ni ukosefu maamuzi ya busara.
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
30,463
2,000
Kwangu mimi huo ni upumbavu wa akili!! Who's Victor Wanyama kwenye soka la Tanzania?!

Nani bora kati ya Victor Wanyama na vijana wanaojitoa muhanga uwanjani kupigania taifa lao ambalo hata haliwajali?!

Ni leo tu hapa tumemshuhudia Mwakyembe akimtembelea Nahodha wa Serengeti Boys ambae ameumia lakini TFF imemtelekeza!!

Shame on You CHADEMA!!

I am sure upumbavu kama huo ungefanywa kwenye halmashauri zinazoongozwa na CCM hivi sasa ingekuwa mnamwaga mapovu hapa!!!
Ni kwa heshima ya kwenda Ndondo Cup, Kinesi! Mbona tuna Sam Nujoma roads, Kenyatta Drive etc?? Povu la nini??
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
32,804
2,000
Kwangu mimi huo ni upumbavu wa akili!! Who's Victor Wanyama kwenye soka la Tanzania?!

Nani bora kati ya Victor Wanyama na vijana wanaojitoa muhanga uwanjani kupigania taifa lao ambalo hata haliwajali?!

Ni leo tu hapa tumemshuhudia Mwakyembe akimtembelea Nahodha wa Serengeti Boys ambae ameumia lakini TFF imemtelekeza!!

Shame on You CHADEMA!!

I am sure upumbavu kama huo ungefanywa kwenye halmashauri zinazoongozwa na CCM hivi sasa ingekuwa mnamwaga mapovu hapa!!!
Mkuu soma basi barua kabla ya kububujikwa povu,umeona mkono wa Chadema hapo,angalia hata nakala za barua zilikoenda,barua imeandikwa na CCM na imenakiliwa kwa CCM,hata meya hajanakiliwa,unatulaumuje sisi
 

Southern Highland

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
8,364
2,000
That is the motivation enough to reach where u want to be. I dont see the problem. Hiyo iwe hasira kwa wengine kuweza kupambana kufikia pale ambapo WALAU jamaa kafikia.
 

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,467
2,000
Mbona kuna mtaa unaitwa Ngoma

Acheni roho za kwann

Wenye mtaa wamekubali nyie povu za nini

Kwani mmekatazwa kuita mitaa yenu majina ya kibadeni ,kizota ,samatta? Ruksa yaiteni waacheni raia wa kinesi wajiamulie

33aac9218d6ab3224d2b09ab927039ed.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom