Mcheza filamu Zuberi Mohamed‘Niva’ juzi alijikuta akipata fedheha baada ya kupigana

Ibrahim300

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
390
68
Mcheza filamu Zuberi Mohamed‘Niva’ juzi alijikuta akipata fedheha baada ya kupigana na mwanamke anayesemekana kuwa kama ni mpenzi wake, sakata hilo la aibu lilitokea katika Hotel ya Ndeka iliyopo maeneo ya Magomeni, tukio hilo lilitokea mida ya saa tano usiku. Walioshuhudia tukio hilo amesema kuwa Niva alikuwa kapanga katika Hoteli hiyo na baadae alikuja na binti huyo na kuagiza chakula na kupelekewa chumbani huko ambako ugomvi ulitokea na kusababisha vurugu zilimfanya Niva kutoka nduki.

Kufuatia ugomvi huo uliotokea ghorofa ya tano chumba namba 5, msanii huyo alitoka nduki akiwa na nguo ya ndani tu na kukimbia hadi chini na kutoweka jambo lilofanya wahudumu kuingia katika chumba hicho na kushuhudia uharibifu uliofanywa na wapenzi hao, huku kuta za chumba hicho zikiwa zimetapakaa kwa uchafu wa vyakula.

Msanii hiyo katika tukio hilo amepoteza vito vya thamani kama vile saa, mkufu, simu na vitu vinginevyo, hadi habari hizi zisizo na shaka zinatufikia msanii huyo alikuwa hapatikani katika simu yake ya mkononi, ili aweke wazi kilichopilekea ghafla na mpenzi wake kugeuzaa Hoteli ulingo wa masumbwi.

Stori imedondoshwa kutoka
NIVA, Msanii Wa Bongo Movie Ala Kichapo Kutoka Kwa Demu Wake -bkuHABARI
 
Back
Top Bottom