Mchengerwa awashukia maofisa ‘wanaobania’ watumishi kupanda madaraja

Huyu waziri anachapa kazi na anafahamu vizuri matatizo sugu ya wizara yake na jinsi ya kuyatatua. Wafanya kazi tujitokeze popote pale ( Mitandaoni, magazetini, maofisini, bararani, katika sherehe tofauti........) kumpongeza Waziri huyu.

Mohamed Mchengerwa ni moja kati ya viongozi 40% aliowasema Prof Assad kuwa ndio wana uweledi katika nafasi zao. Hongera.
Aje kwanza na vitendo, maneno kasema sana
 
Mchengerwa !Unapaswa kuwapandisha madaraja mara mbili watumishi waliotumika muda mrefu kazini bila kupanda daraja!mf.walioajiriwa miaka 2013,2014 wote wametumika kwa miaka 7 hadi 8 na wamepanda mara moja tu!!nashauri wapandishe marambili zaidi ili kufidia miaka yao ya utumishi walioitumikia!!!!
KuNA tuliotumika miaka 22 hatujawahi kupanda Vyeo zaidi ya kuhuishwa kwenye Scheme of Service. Ikitoka mwaka huu utaitwa assistant registar Mshahara wako huo. Ikitoka nyingine utaitwa Assistan minor Registrar salary scale F
 
mchengerwa pic

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewaagiza waajiri wote nchini kuchukua hatua kuwaondoa katika nafasi zao baadhi ya maofisa utumishi walioshiriki kuficha sifa za watumishi wenzao hali iliyosababisha kutopandishwa madaraja.

===
Arusha. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewaagiza waajiri wote nchini kuchukua hatua kuwaondoa katika nafasi zao baadhi ya maofisa utumishi walioshiriki kuficha sifa za watumishi wenzao hali iliyosababisha kutopandishwa madaraja.

Akizungumza katika mafunzo ya viongozi wa matawi ya Chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) na waajiri yaliyofanyikia jijini Arusha, Mchengerwa amesema waajiri waende kuwashusha vyeo maofisa utumishi hao na nafasi hizo wawekwe watu wenye uwezo ambao watakuwa tayari kusikiliza kero za watumishi wenzio.

Amesema si watumishi ambao wapo katika ofisi kwa ajili ya matumbo yao hiyo haikubaliki hivyo ni lazima kila mmoja akabadilisha mitazamo yake kwa sababu Serikali ya sasa haitaki uonevu.

"Kila kiongozi lazima atengeneze ushawishi wa kuleta mapinduzi ya kifkra kama tunakuwa na watendaji ambao hawapendi kuona wenzao wanafanikiwa na wakipewa nafasi wanadhani miji yote ya kwao, hawafahamu kuwa vyeo hivi ni vya kupita tu pia wanasahau kwamba utumishi wa umma una muda," amesema waziri huyo.

Waziri huyo amehimiza waajiri kujenga utamaduni wa kuwajengea uwezo watumishi wao ili kuweza kupata weledi na kuleta uelewa ambao utakwenda kutoa kasoro ambazo zitakwenda kuleta ajali kazini.

Naye Katibu Mkuu wa Tughe, Hery Mkunda amesema mafunzo hayo yanalenga kuleta uelewa wa pamoja katika masuala ya waajiri na watumishi lakini pamoja na ushirikiano huo bado wanakabiliwa na changamoto ya uwepo wa baadhi ya vifungu vya sheria na kanuni ambazo zinaweza kuleta mgongano katika utendaji kazi.

Source: Mwanachi
Asante Sana Waziri. Wapo baadhi maafisa utumishi wenye sifa hizi za roho mbaya hasa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
 
Kuna kipindi huko nyuma alisema maneno ya namna hii, ila tatizo zilongwa mbali zitendwa mbali......in mkwere's voice.
 
Hajapata kutoke waziri kama huyu jamani! Kama kuna mtu ana namba yake naomba anipatie nimtajie baadhi ya maafisa utumishi wa manispaa wanaomkwamisha kwa maslahi ya matumbo yao!
 
Ndio muelewe ukiwa kiongozi unatakiwa uwe na akili nyingi kama mchengelwa. Hapo anawaremba watumishi tu hamna lolote.
 
mchengerwa pic

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewaagiza waajiri wote nchini kuchukua hatua kuwaondoa katika nafasi zao baadhi ya maofisa utumishi walioshiriki kuficha sifa za watumishi wenzao hali iliyosababisha kutopandishwa madaraja.

===
Arusha. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amewaagiza waajiri wote nchini kuchukua hatua kuwaondoa katika nafasi zao baadhi ya maofisa utumishi walioshiriki kuficha sifa za watumishi wenzao hali iliyosababisha kutopandishwa madaraja.

Akizungumza katika mafunzo ya viongozi wa matawi ya Chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) na waajiri yaliyofanyikia jijini Arusha, Mchengerwa amesema waajiri waende kuwashusha vyeo maofisa utumishi hao na nafasi hizo wawekwe watu wenye uwezo ambao watakuwa tayari kusikiliza kero za watumishi wenzio.

Amesema si watumishi ambao wapo katika ofisi kwa ajili ya matumbo yao hiyo haikubaliki hivyo ni lazima kila mmoja akabadilisha mitazamo yake kwa sababu Serikali ya sasa haitaki uonevu.

"Kila kiongozi lazima atengeneze ushawishi wa kuleta mapinduzi ya kifkra kama tunakuwa na watendaji ambao hawapendi kuona wenzao wanafanikiwa na wakipewa nafasi wanadhani miji yote ya kwao, hawafahamu kuwa vyeo hivi ni vya kupita tu pia wanasahau kwamba utumishi wa umma una muda," amesema waziri huyo.

Waziri huyo amehimiza waajiri kujenga utamaduni wa kuwajengea uwezo watumishi wao ili kuweza kupata weledi na kuleta uelewa ambao utakwenda kutoa kasoro ambazo zitakwenda kuleta ajali kazini.

Naye Katibu Mkuu wa Tughe, Hery Mkunda amesema mafunzo hayo yanalenga kuleta uelewa wa pamoja katika masuala ya waajiri na watumishi lakini pamoja na ushirikiano huo bado wanakabiliwa na changamoto ya uwepo wa baadhi ya vifungu vya sheria na kanuni ambazo zinaweza kuleta mgongano katika utendaji kazi.

Source: Mwanachi
Kazi nzuri sana hii
 
Back
Top Bottom