fiksiman
JF-Expert Member
- May 17, 2008
- 402
- 104
Huku akionekana kuwa ni Rais mwenye kuaminika na kuleta ari mpya miongoni mwa wanyonge wa Nchi ya Afrika Kusini, hatimaye Jacob Zuma ameibuka kidedea kwenye uchaguzi mkuu na sasa anakaribia kutawazwa kuwa Rais Mpya wa Taifa lenye nguvu Afrika.
Hata hivyo, safari yake imeanza kuingiwa na dosari baada ya kutoa mwaliko kwa Rais "wanted" na Mahakama ya Kimataifa, Alhaji Omari Al Bashir wa Sudan ambaye amewekewa RB ya kukakwamata kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya Ubinadanu. Zuma amemwalika Bashir katika sherehe za kuapishwa kwake pamoja na kutambua kuwa anatafutwa kwa udi na uvumba na Jumuiya hiyo.
Msemaji wa Serikali ya Afrika Kusini, Bwana Themba Maseko amethibitisha kualikwa kwa Rais huyo pamoja na wakuu kadhaa wa Nchi za Afrika japo uwepo wake umeshauriwa usiwepo ili kuepusha mahusiano mabaya na Jumuyia za kimataifa
Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zilizotia saini makubaliano ya Rome juu ya uwepo wa Mahakama hiyo na italazimika kumkamata kiongozi huyo wa Sudan endapo atatia mguu katika ardhi hiyo. Swali je kwanini wamemualika wakijua hali halisi ya Kiongozi huyo?
Huu watoto wa uswahili huuita MCHESHO WA HALI YA JUU.