Wanabodi!
Nilifuatilia utoaji tuzo za Mo Simba Awards 2019. Kwa ujumla tukio hilo lilifana sana. Nawapongeza waandaaji.
Lakini nimeona kitendo alichokifanya nyota wa uchekeshaji MPOKI kwa mchezaji bora mwanamke wa Simba Sc kisipite bila kukemewa. Ni kuhusu maswali aliyoulizwa dada huyu.
Kitendo cha kumuuliza mbele za watu "una mume?" kwa sauti isiyo na staha kwa dada zetu ni udhalilishaji.
Mbaya zaidi baada ya kujibiwa kwamba "sina" ukaonesha kushangazwa kama vile ni kitu cha ajabu sana.
Pia kitendo cha kumuuliza nyota huyo mbele ya watu kwa mshangao mkuu "una mtoto?" na pia kushangazwa zaidi baada ya kujibiwa "sina".
Ndugu Mpoki siyo kila swali waweza uliza mbele za watu. Maswala ya kuolewa na kuwa na watoto hasa kwa wanawake ni sensitive sana. Wengi wao kutokuwa na mume ama watoto huwa iko nje ya uwezo wao.
Wengi wana matatizo ya uzazi hivyo kumdhalilisha mbele za watu ni kumwongezea machungu dada yetu. Mengine unauchuna tu.