Mchechu akana kulipwa mshahara wa shilingi milioni 36

Kuna jambo moja la msingi ambalo tunashindwa kulielewa...,

Moja hili shirika priority inafaa kuwa service oriented na sio profit oriented (tena linafaa kuwasaidia wananchi wasiojiweza kupata makazi) hayo ya kuwalenga wenye fedha na kupata kipato na faida iwe ni nyongeza na sio core objective..

Huyu bwana angekuwa NSSF au PPF au Pension Funds yoyote ambayo jukumu ni kuzalisha pesa za wateja wake ningemuelewa, ila sio kubadilisha shirika ambalo kuundwa kwake mwanzo kulikuwa kutoa msaada, hata kama alilikuta linajifia ila lilikuwa lina asset za kutosha.., sasa kutumia hizo asset ili kutengeza faida na kuwanufaisha wenye nazo halikuwa wazo la hii kampuni wakati inaanzishwa..

Kwa Dar Sehemu ambapo nyumba hazitoshi wanashindwa vipi kutengeneza ma-flats ya kutosha kupunguza demand ya nyumba hence kupelekea hata wenye nyumba binafsi kushusha bei ?
 
Hata akilipwa 40 mill sio mbaya jamaa kapiga kazi sana amelifanya NHC isimame na kuwa bora kuliko miaka 10 iliyopita jamaa ni jembe
NHC unaiona kwa nje tu. huijui na hutokaa uijue milele yote!
 
Ukiona kuna maslahi zaid huko aliko omba kazi na ww uende huko hakuna mtu aliyezaliwa amepigwa mhuri kwamba atapata hiki au kile au atafanya hapo kazi, ni bidii ndio inayotoa watu, watanzania tunachotakiwa kupigania ni fair ground namna gani nafasi mbali mbali potential zinapatikana mfano ma CEO, commissioner mfano wa tra, kwamba ni nafasi zinazotakiwa kutangazwa watu waombe ikiwezekana kuwepo panel interviews kwenye tv tujue watu wanaoenda huko wana uwezo gani, sio kuleta umbea hapa kuwa wanalipwa sana. Watu wanafight hawalali kujenga weledi, kutafuta maarifa, kutafuta pesa.
 
Hivi lengo la Shirika la nyumba la Taifa ni kujenga nyumba na kuuza. Hivi mpaka 2018/19 mkataba wake utakapoisha Serikali itakuwa imebaki na eneo gani? Na hiyo faida anayojivunia sasa itatoka wapi? Au tatizo la nyumba litakuwa limeisha kupitia utaratibu wake wa kuuza kila ardhi ya serikali?
 
Swali kwa NHC:1. Wazawa hatustahili kuishi Upanga,Ada estates?
2. Ni kwanini eneo lote la kawe wapewe wao wakati kawe ingine inakaa slums kwanini isipimwe viwanja vikauzwa kwa watu
3. Mikataba wanayoingi kama Eco village kibada kigamboni ni kwa ajili ya wageni ma expert wanyekipato cha juu au wazawa
4. Kwanini hakuna sera mahsusi ya kuchanganya racial katika nyumba zilizopo katikati ya miji na wanakaa watu wa rangi fulani tuu haswa wahindi,waarabu etc
 
5. Nyumba ukiomba unakuwa kwenye waitinglist muda mrefu, Je le mbebez naye aliwekwa kwenye waiting list au jina na ukada ulimbebba kupata nyumba downtown u knoo
 
Kama anakataa halipwi hiyo 36M mbona hajataja analipwa kiasi gani?

Halafu asidanganye watu, nyumba zao bei iko juu sababu wanaweka na migharama yao ya miposho ya kifisadi wanayolipana
 
Watu kwa kutetea ujinga hamjambo, mlikuwa mnampamba Bade wa TRA hivi hivi kumbe mpiga madili hatari
 
Mimi sina shida na kulipwa kwa mchechu lakini tatizo langu ni hizo nyumba ambazo zinaitwa za bei nafuu bado si nafuu na kamwe watanzania wenye kipato hata cha kati kamwe hawewezi kununua nyumba hizi!

Mchechu tunajua unafanya kazi kubwa na nzuri lakini bado swala la bei za hizo nyumba mnapaswa kulitazama upya ...
 
Swali kwa NHC:1. Wazawa hatustahili kuishi Upanga,Ada estates?
2. Ni kwanini eneo lote la kawe wapewe wao wakati kawe ingine inakaa slums kwanini isipimwe viwanja vikauzwa kwa watu
3. Mikataba wanayoingi kama Eco village kibada kigamboni ni kwa ajili ya wageni ma expert wanyekipato cha juu au wazawa
4. Kwanini hakuna sera mahsusi ya kuchanganya racial katika nyumba zilizopo katikati ya miji na wanakaa watu wa rangi fulani tuu haswa wahindi,waarabu etc


Mkuu ukisha achia sekta au idara flan ijiendeshe hasa katika mambo kama haya ambayo yanahitaji investment kubwa, kama govt haija "chip in' kidogo swala la UZAWA linabakia kuwa siasa, mfano mzuri ni DART serikali imejenga bara bara kama isipotoa hela kupunguza nauli, hakuna mwekezaji ataleta mabasi executive watu wapande kwa sh. 900,lazima watafute return on investment.
 
Mchechu! Nyumba iliyokuwa ya meneja Kigombe Sisal Estate umenunua 320,000$. Cash. Kwa mshahara upi? Una hisa katika kampuni hiyo hiyo 51%. The rest belonging to one Dr George. Limebadilishwa jina tu. Hivi ninavyoandika mpo katika mchakato kutumia rasimu ya Mpingo Golf Course kubadilisha matumizi ya ekari zako 500 pwani ya Kigombe. Need the masses know more?
 
Majitu mengine siyaelewi kabisa. NHC ilipokuwa ktk hali mbaya hamkusema, sasa shirika ameliboresha mnaanza fitna. Mwacheni Mchechu achape kazi. Mnawakatisha tamaa.vijana wazalendo wanaojitoa kulitumikia taifa.
 
Nasikia huyu jamaa analipwa zaidi ya 30mil,
Hawezi sema ukweli mana ni jipu huyu kijana
 
Hata akilipwa 40 mill sio mbaya jamaa kapiga kazi sana amelifanya NHC isimame na kuwa bora kuliko miaka 10 iliyopita jamaa ni jembe

Jembe, lipi Mkubwa? Hivi unajua Kwamba NHC imeama kutoka Shirika la Nyumba za watu Maskini Na Kuwa Shirika La Mabepari?

Angalia Miradi Yao Mingi Je! Inawagusa Watanzania Wa Kipato cha Chini au Makabwela?

Angalia Nyumba Zao wanauza Kima cha chini Ni ml 35 je! Mama ntilie au muuza mandazi anaweza kununua hiyo nyumba?

Laiti shirika hili lingejikita kwa ajili ya wanyonge Basi kila mtanzania wa chini kabisa angekuwa anamiliki nyumba yake na kulipa kidogo kidogo. Na hii ingeondoa hata tatizo la watu kujenga mabondeni maala pasipo salama.

Tusijidanganye nafsi zetu. Shirika hili limeshaondoka kwa wanyoge na kujikita kwa matajiri.
 
Kwanini wasitoe financial statement kwanza kila mtu aone afya ya shirika na waamue wenyewe kama kweli Mkurugenzi kaongeza value inayopimika; madeni kila mtu anajuwa wanayo na sasa hao hao wapangaji anaodai awana faida ndio wamewageuza cash cows wa kufidia madeni yao na kodi za kushtukiza tena zisizozingatia ongezeko la mishahara ilhali mambo yangekuwa tofauti sana kama wangekuwa wamewajengea watu wa chini au wamefuata strategy waliyoipima.

Common sense tu kama 70% ya miradi ni kwa sababu ya kuuza na nyumba zimeuzika karibu zote hizo faida azikizi kulipa madeni au kuyapunguza kwa kiasi kikubwa sasa iweje wadeni watake government guarantee na shirika bado lidai lina madeni sie wengine could not care less on what NHC does anymore kama serikari inaona jamaa anafaida.

Lakini habari za kuwageuza wapangaji n'gombe wa maziwa na kodi za ajabu ajabu kila wakati sio sahihi kabisa hakuna mtu alitegemea sehemu wanazoishi zitapanda thamani kwa sababu ya uzembe wa serikari kuwekeza kutanua jiji sehemu zingine leo mnazoziita prime areas miaka hiyo (kabla amjaja mjini na mbio za mwenge) zilikuwa ni makazi ya watu mchanganyiko upanga ilikuwa imejaa nyumba za walimu na wafanyakazi wa wakaida tu serikarini leo imekuwa sehemu ya matajiri whose fault is that wapangaji au serikari.

Siku hizi imekuwa shida kila kukicha kodi mpya tena zinatisha na fukuza fukuza hivyo ndio serikari inavyofanya kazi kweli kwenye mashirika ya umma si ndio unyanyasaji wenyewe wa wapangaji kisa kuingizwa katika wigo la sehemu ambazo mnadai ni prime wakari huo huo mnawatumia kufidia madeni huku kama sio kuchosha raia bila ya mpango nini kwani waliomtangulia awakuona kama wale wapangaji wengi walikuwa watu wakaida tu ndio maana wakaawacha na wengine.

Huyu jamaa mpaka dakika hizi anakazi ni Tanzania tu the concept of government public company aipo ata ukisoma nakala shughuli yao ni kuwaweka watanzania wa chini mjengoni na sii kufanya miradi ya mahoteli sijui kutuambia wanajenga majumba ambayo sisi wengine ayatuhusu.
 
Kwanini wasitoe financial statement kwanza kila mtu aone afya ya shirika na waamue; madeni kila mtu anajuwa wanayo na sasa hao hao wapangaji anaodai awana faida ndio wamewageuza cash cows wa kufidia madeni yao na kodi za kushtukiza tena zisizozingatia ongezeko la mishahara ilhali mambo yangekuwa tofauti sana kama wangekuwa wamewajengea watu wa chini.

Common sense tu kama 70% ya miradi ni kwa sababu ya kuuza na nyumba zimeuzika karibu zote hizo faida azikizi kulipa madeni au kuyapunguza kwa kiasi kikubwa sasa iweje wadeni watake government guarantee na shirika bado lidai lina madeni sie wengine could not care less on what NHC does kama serikari inaona jamaa anafaida lakini habari za kuwageuza wapangaji n'gombe wa maziwa na kodi za ajabu ajabu kila wakati sio sahihi kabisa hakuna mtu alitegemea sehemu wanazoishi zitapanda thamani kwa sababu ya uzembe wa serikari kuwekeza kutanua jiji sehemu zingine leo mnazoziita prime areas miaka hiyo (kabla amjaja mjini na mbio za mwenge) zilikuwa ni makazi ya watu mchanganyiko upanga ilikuwa imejaa nyumba za walimu na wafanyakazi wa wakaida tu serikarini leo imekuwa sehemu ya matajiri whose fault is that wapangaji au serikari. Leo anakuja mtu kama huyu anataka kuongeza kodi kila uchao hivyo ndio serikari inavyofanya kazi kweli kwenye mashirika ya umma si ndio unyanyasaji wenyewe wa wapangaji huo kisa kufidia madeni huku kuchosha raia bila ya mpango.

Huyu jamaa mpaka dakika hizi anakazi ni Tanzania tu the concept of government public company aipo ata ukisoma nakala shughuli yao ni kuwaweka watanzania wa chini mjengoni na sii kufanya miradi ya mahoteli sijui kutuambia wanajenga majumba ambayo sisi wengine ayatuhusu.

Ukweli Mtupu.
 
Mbona taarifa ya faida iliyopata shirika kwa mwaka 2010 zinatifautiana?

Mwanzoni mmetaja 2010 mlipata faida ya tsh. 3.1 bilioni lkn hapo mwishoni unasema 2010 mlipata faida ya tsh. 36.6 bilioni.

Lipi ni sahihi?
 
Back
Top Bottom