Mchawi wa kinachotokea na kitaendelea kutokea ndani ya CHADEMA Iringa ni mbunge Peter Msigwa

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
Katika hali ya kushangaza jana tarehe 26/1/2018, Ndg Alex Kimbe meya wa Manispaa ya Iringa aliwaahadaa wana Iringa juu ya kutaka kununuliwa na aliowataja makada wa Ccm Ndg Sawani na Mlowe jambo ambalo si la kweli.

Chama cha Mapinduzi hakina mawakala wa kununua watu katika zama hizi ambazo chama kimekuwa kinajimbanua zaidi katika kuwa chama kinachojali shida za watu na kuitekeleza ilani yake ya uchaguzi ya 2015-2020.

Ikumbukwe kuwa hamahama ya viongozi wa chadema ndani ya manispaa na nje ya mkoa katika ngazi mbalimbali inatokana na viongozi hao kuridhishwa na kasi ya utendaji na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania kwa uadilifu unaofanywa na M/kiti wa ccm Taifa na Rais wa Tanzania Dk John. P. Magufuli katika kuijenga Tanzania mpya yenye misingi thabiti.

Kama hoja ni kununuliwa ?
Ni vyema kama aijulishe Takukuru akiwa na ushahidi ili chombo hicho kiweze kufanya kazi yake na wanairinga waweze kupata ukweli na sio Kutapatapa kwa meya Kimbe.

Suala la kuvunjwa nyumba ya Ndg Lijuja na kuchomewa nyumba aliyekuwa akiishi katibu wa vijana wa ccm Ndg Muyinga. Ni suala ambalo lipo katika vyombo vya ulinzi na usalama kiuchunguzi zaidi hivyo kwa viongozi wa chadema tunawaomba wasiharibu utaratibu ambao unafahamika siku zote.

Chanzo cha yanayotokea ndani ya chadema Iringa ni mbunge wao Ndg Peter Msigwa.
Hili sasa ndo lipo wazi kwa dhahiri ikumbukwe katika mahojiano yake aliyofanya na kituo cha redio Ebony fm tarehe 8/1/2018 Ndg Nyalusi diwani wa kata ya mivinjeni na mwenyekiti wa Chadema manispaa alisema yanayotokea ni ubabe na ukiritimba wa kutaka kumpitisha naibu meya wa manispaa ya Iringa anayetokana na chama hicho Ndg Dady Igogo na ndo hapo wakapishana na viongozi wenzake ambao hawakuwa tayari kuburuzwa.

Kimbe unalijua hilo ingawa una wahadaa wana Iringa.
Ushauri wangu kwa Ndg Kimbe.
Nafahamu kuwa wewe kama meya umeisoma na mpaka sasa ndani ya manispaa yako unatekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm 2015-2020, ni bora sasa ukatoka huko uliko na ukaja ungana nasi wana ccm kumsaidia Rais wetu kipenzi cha wanyonge Dk Magufuli, katika juhudi zake za kuijenga Tanzania imara na kuitekeleza na kuiishi ilani yetu ya uchaguzi ya ccm 2015-2020, kumbuka kuwa waswahili wana msemo mzuri sana wa hiyari yashinda utumwa.

Imetolewa Na

Ramadhani M.Baraza Katibu wa siasa na uenezi Ccm mkoa Iringa.
 
Wewe ni mnafki msigwa anapiga kazi kuliko hata waziri wa ulinzi singida ambaye sasa kakimbia ofisi amebaki kupiga kampeni.msigwa ni sawa na wabunge wa,ccm 12



$wissme
 
unachofanya wewe ni kukanusha kua ccm haijaweka mawakala wa manunuzi pande hizo, ila pande zingine tayari mawakala wapo!
 
Back
Top Bottom