Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,764
"Mchawi akimaliza kuroga mtaa mzima, hugeukia familia yake." One of my most favourite age-old adages. Literally, msemo huu unamaanisha kwamba mtu akishamaliza kufanya mabaya kwa kila "asiyemhusu" hatimaye huwageukia wanaomhusu.
Sote tumeshuhudia yaliyojiri dhidi ya vyama vya upinzani katika miaka mitatu ya utawala wa Jiwe. Sihitaji kutonesha vidonda ambavyo havijapona hasa ikizingatiwa kuwa wahanga wa utawala wa mabavu wa Jiwe bado wanataabika - Mbowe na Matiko wapo jela, Tundu Lissu licha ya kuwa hajapona kamili bado anaandamwa kila kukicha, Azory na Ben Saanae "bado hawajulikani waliko," yaliyojiri MKIRU bado ni "siri kuu," Wapinzani wanaendelea kunyimwa haki zao za msingi huku CCM wakizichezea haki hizo kama mzaha vile....orodha ni ndefu.
Lakini pia Jiwe amefanikiwa sana katika kusambaza siasa za chuki, sio tu miongoni mwa wana-CCM wenzake bali hata kwa wafuasi wa Upinzani. Tumefika mahala kwamba aidha uwe unaimba mapambio kumsifia Jiwe - na hapohapo kupokea mvua ya matusi kutoka kwa wafuasi wa Upinzani - au uwe mfuasi wa Upinzani - na hapohapo uandamwe kama mhaini na MATAGA, Buku 7 Lumumba, na wapuuzi kama hao.
Kwahiyo "akina sie ambao itikadi yetu pekee ni maslahi na mustakabali wa Tanzania yetu," tunajikuta na choice moja tu: kukaa kimya ili kuepusha kugeuzwa punching bag la wanaojifunza matusi mtandaoni.
Hata hivyo, kukaa kimya wakati mwelekeo wa taifa sio mzuri ni sawa na usaliti, na ndio maana inalazimu mara moja moja "kuvaa kofia ya chuma" dhidi ya matusi yatakayojitokeza baada ya kuongea lolote lile, maana likiwafurahisha wafuasi wa Upinzani basi litawakera wafuasi wa CCM na hivyo kupelekea mvua ya matusi, na likiwakera wafuasi wa Upinzani litawafurahisha wafuasi wa CCM, na hivyo pia kupelekea mafuriko ya matusi.
Anyway, ndio tulipofikia hapo kama Taifa.
Hadi muda huu ni furaha tele huko CCM kwa jinsi Jiwe "anavyowaburuza" Wapinzani. Lakini sie wengine tunaofahamu yanayojiri nyuma ya pazia/chini ya kapeti tunafahamu vema kuwa haya wanayofanyiwa wapinzani ni tip of iceberg tu ya suala zima la kumuandama kila mtu anayeonekana kuwa tishio kwa dhamira ya Jiwe ya kutawala milele. Naam, kama hujui hilo ndo unaambiwa sasa. Huyo bwana hana mpango wa kutoka madarakani, sio 2025 wala baada ya hapo.
Kuna kundi moja lenye ushawishi mkubwa sana kwa jiwe. Kundi hili ni wanufaika wakubwa wa sera ya ukanda/ukabila inayoendelea kuitafuna Tanzania yetu. Wengi wa watu hawa ni vijana wa umri wa kati, waliosoma na Jiwe au waliwahi kufanya kazi pamoja huko nyuma.
Takriban wote wana nyadhifa mbalimbali, wengine wana nyadhifa muhimu kitaifa, wengine mikoani, wengine kwenye taasisi za umma, wengine wilayani. Sihitaji kuwataja majina kwani naamini wengi wenu mwawafahamu.
Uhusiano kati ya Jiwe na kundi hili ni symbiotic kama ule wa Kitengo na CCM: survival ya kila upande inategemea survival ya mwenzie. Hao jamaa hawakupewa madaraka na Jiwe kwa bahati mbaya.Hapana. Most of them walipigana kufa na kupona kuhakikisha kuwa "poti wao" anaingia Ikulu. Ikumbukwe kuwa suala la Jiwe kuingia Ikulu lilikuwa linaandika historia mpya kwa Kanda ambayo licha ya ukubwa kikabila, haikuwahi kuzalisha Rais, Makamu au Waziri Mkuu.
Kwahiyo baada ya Jiwe kuingia Ikulu, aliwalipa fadhila jamaa zake hao kwa kuwateua katika nafasi mbalimbali. Hiyo ilikuwa asante yake kwao. Lakini wakati hili sio siri sana, deni kubwa la Jiwe kwa watu hao ni "siri binafsi." Takriban wote wanajua masuala flani kuhusu Jiwe ambayo laiti wangeyamwaga hadharani 2015, Jiwe asingefika kwenye Tano Bora let alone kuibuka mshindi kwenye Tatu Bora.
Miongoni mwa "siri" hizo ni hiyo inayomfanya Jiwe kuwa "mateka wa Mtu Mrefu Paulo."
Kwahiyo, kwa namna flani, kama ilivyokuwa kwa JK ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa kama mateka wa mafisadi waliomsaidia kuingia mdarakani, Jiwe nae ni kama mateka wa hilo genge la marafiki zake ambao sio tu walimsaidia kuingia madarakani lakini pia wanamhifadhia "nyeti" ambazo zikivuja tu, amekwisha.
Kwa wenye uelewa wa yanayojiri nyuma ya pazia/chini ya kapeti, zama za ufisadi sio tu zimerudi bali inaelezwa kuwa katika kipindi cha takriban miaka mitatu ya Jiwe, hali ni maradufu ya yaliyojiri katika miaka 10 ya JK. Huku media zikiwa zimezibwa mdomo, kitu pekee kinachosikika ni vigelegele na mapambio kwa Jiwe. Hakuna wa kuthubutu kueleza hali halisi. Ndio maana ufisadi wa mradi wa passport za kielektroniki, ufisadi wa shilingi trilioni moja unusu, changa la macho kwenye Koroshow, ujenzi wa Chuttle Intl Airport, Ununuzi wa bombadia/drimlayna, nk ni masuala ambayo kamwe hayatowekwa hadharani.
Wanasema "wakati enzi za JK ufisadi ulikuwa suala la EQUAL OPPORTUNITY" - kwa maana kila aliyeweza kuuza unga, poa; kila aliyeweza kufanya ujangili, poa; kila aliyeweza kuchapisha noti feki, poa, nk - zama hizi za Jiwe, ufisadi ni kwa privileged few - hao washkaji zake aliotoka nao mbali, waliompigania kwenye kampeni, waliohifadhi "mabaya" yake, na wakazawadiwa madaraka katika ngazi mbalimbali. Some of them ni ndugu wa damu wa Jiwe.
Kuna mambo mawili hapa. Kwanza, utawala wa Jiwe unawanufaisha hao jamaa zake katika namna ambayo "hawawezi kuishi hivyo bila yeye kuwepo madarakani." Kwahiyo, hawa wanataka aendelee kuwepo madarakani ili nao waendelee kufakamia keki ya taifa. Lakini pili, ni maovu yanayoambatana na ufakamiaji huo wa keki ya taifa. Kama alivyotahadharisha mbunge mmoja kuhusu "mpwa wa Jiwe," pindi Jiwe akiondoka, genge hilo nalo lipo katika hatari ya kutupwa jela. Hawa ndio the brains behind idea ya "Jiwe kutawala milele."
Sijui kama hii ni habari njema au la, kuna jithada kubwa zinafanyika chinichini ndani ya CCM kukabiliana na genge hili, japo hadi sasa matokeo ni "kundi la Jiwe 5 wapinzani ndani ya CCM 0." Na sababu ni nyingi: Kitengo hasa kwa kupitia MATAGA, Msaada kutoka kwa Mtu Mrefu Paulo na teknolojia ya Waisraeli, na ukweli tu kuwa mfumo waloutengenza CCM hautoi fursa nzuri kwa wanaotaka mabadiliko ya dharura.
Sasa, baada ya kumaliza kuwashughulikia Wapinzani, ngwe iliyopo ni kuwashughulikia "wapinzani ndani ya CCM." Kuna mbinu chafu zinazotumika, kwa mfano kuna jitihada kubwa ya kukusanya taarifa kuhusu maisha binafsi ya JK - michepuko yake and stuff, - kama miongoni mwa silaha zitakazotumika kum-blackmail endapo atasimama kidete dhidi ya "mabaya" yanayoendelea ndani ya chama chao.
Kwa kuhitimisha, hatua ijayo - na ambayo imeshaanza kutimia - ni maandalizi ya ushindi wa kishindo kwa Jiwe mwaka 2020, yanayoambatana na kuondoa "wapinzani ndani ya CCM." Sambamba na "wapinzani ndani ya CCM" ni watu wanaoonekana kuwa na potential ya kuunga mkono upinzani dhidi ya Jiwe ndani ya CCM. No wonder ile approach ya awali ya kuwakalia kooni viongozi wa dini imegeuzwa na badala yake "wamerejeshwa kundini." Walengwa wengine ni wafanyabiashara na private sector kwa ujumla.
In conclusion, whether Jiwe atawarudi CCM wenzake baada ya "kuwamaliza" wapinzani au la, moja ya tafakuri muhimu ambayo "wapinzani halisi" kwa maana ya vyama vya upinzani wanapaswa kujiuliza ni jibu la swali hili kutoka kwa Watanzania: "MLI/MNA/MTAFANYA NINI KUZUWIA JANGA HILI?"