Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,814
109,091
MCHAWI AKAMATWA DAR NA KUUAWA LIVE BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

December 23, 2013

15.JPG

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.

Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.

Kabla ya kufariki alisema "mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu"

"Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu"

Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

"Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto" alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.

"Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe" alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.

21.JPG

Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.

19.JPG

Wananchi hao wakimzonga mchawi huyo.

20.JPG

Kipigo kitakatifu kutoka kwa wanachi.

16.JPG

Kipigo kinaendelea hadi kupelekea umauti wake.

17.JPG

Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.
 
Watanzania ndipo tulipofikishwa hapa tunaacha vitu vya msingi kama vile elimu, ajira nk ambavyo ndiyo kikwazo cha maendeleo yetu sisi tunashughulikia kuwaMabina ndugu zetu ambao wako ktk harakati zao za maisha.
 
MCHAWI AKAMATWA DAR NA KUUAWA LIVE BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

By: Ahmed Ismail on Monday, December 23, 2013

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.
Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema "mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu"
"Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu"
Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.
"Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto" alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.
"Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe" alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.
Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.
Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.

Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.

Wananchi hao wakimzonga mchawi huyo.

Kipigo kitakatifu kutoka kwa wanachi.

Kipigo kinaendelea hadi kupelekea umauti wake.

Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.

Source: tzya kijanja: MCHAWI AKAMATWA DAR NA KUUAWA LIVE BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

i am sure you are happy! hapa ndipo tulipofikishwa na binamu yako JK!
 
zamani tulijua wazee peke yao ndio wachawi,,,,sasa hivi hizi ajira milioni 1 kwa mwaka ndizo zinatendewa haki na vijana
......maisha bora
 
mimi ni mkazi wa Mbezi Luis. Namfahamu huyu kijana ni mkichaa wa siku zote na siku zote yuko hapa Luis. kosa lake siku ya tukio alivua nguo sasa kwa kua wananchi wa huku wana uchu wa kumwaga damu hata iwe ya kichanga ndio wakamsingizia ili wamtoe roho. Hivi we are grown ups. kweli kuna raia anaamini huu upuuzi wa kusafiri na ungo ? kama mnaamini basi mtaamini rais ajaye ni Kingunge ngombale
 
..Kwa kweli inasikitisha sana kuona jinsi huyo kijana alivyo uwawa kikatili na wananchi,ni sababu gani ya msingi iliyofanya auawe?kwa maana amehukumiwa pasi na sheria kuchukua mkongo wake.Huenda kama angefikishwa kwenye vyombo vya sheria tungepata kufahamu mengi na kuujua huo mtandao.Sasa wamesha muua ndio iweje?Serikali inapiga sana kelele wananchi wasichukue sheria mikononi,si kwamba namtetea kwa vitendo vyao viovu lakini haikupasa kumuua,na wale wote walio shiriki kumuua wanayo kesi ya kujibu kesho kwa M.Mungu.Anae uwa pasi na sheria na yeye auliwe.
 
Pengine waliomuuwa ni wachawi wenzake na hawakutaka siri zao zijulikane.
 
matukio ya kuua watu kwa imani za kichawi ni ya kijinga na kinyama.Huyu ni chizi tu ambaye labda ni bangi ilimuharibu. Bora angekua jambazi,wengi tusingeshituka.Nyakati hizi kweli tunaamini mtu anaweza safiri na ungo!? Tukiendekeza haya,laana itaiangukia nchi hii.
 
Hapo utakuwa humtedei haki. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Unakumbuka kwanini Ali Hassan Mwinyi alijiudhuru wakati wa Nyerere? au ulikuwa hujazaliwa bado?

na jk aliangushwa na nini jukwaani wakati wa kampeni 2010! siyo kwamba ndiyo imani zenu?
 
Nchi za magahribi watu wengi sana wanavaa miwani kuliko huko kwetu, je hili linamaanisha sisi hatuna wagonjwa wa macho?

Nchi za magharibi watu wengi, hususan wazee, wanavaa "hearing aids", hivi sisi wazee wetu hawana matatizo ya kusikia?

Nchi za magharibi utasikia magonjwa/ conditions ya akili kibao, mara schizophrenia, mara depression, mara obsessive compulsive disorder, mara separation anxiety disorder, mara bipolar disorder etc etc.

Huko kwetu mbona hatusikii habari za hawa watu?

Usije kukuta ugumu wa maisha unawatia watu uchizi wanajisemea ovyo, wana mi mental disorder, au wamechotwa tu kisaikolojia, halafu kundi la watu masikini wasio elimu wala huruma linawamaliza kama Warumi walivyokuwa wanafurahia gladiator games au rednecks wa Jim Crow South USA walivyokuwa wanafurahia kunyonga watu weusi.

Ukiwauliza kama kuna mtu kamuona anaanguka, utasikia wanakwambia "tumesikia".

Barbaric.
 
Back
Top Bottom