Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo

Kama ni mchawi wa kweli hao waliomuua watapona kweli? Tusije kuanza kuzika kila nyumba hapa DSM.
 
Nchi za magahribi watu wengi sana wanavaa miwani kuliko huko kwetu, je hili linamaanisha sisi hatuna wagonjwa wa macho?

Nchi za magharibi watu wengi, hususan wazee, wanavaa "hearing aids", hivi sisi wazee wetu hawana matatizo ya kusikia?

Nchi za magharibi utasikia magonjwa/ conditions ya akili kibao, mara schizophrenia, mara depression, mara obsessive compulsive disorder, mara separation anxiety disorder, mara bipolar disorder etc etc.

Huko kwetu mbona hatusikii habari za hawa watu?

Usije kukuta ugumu wa maisha unawatia watu uchizi wanajisemea ovyo, wana mi mental disorder, au wamechotwa tu kisaikolojia, halafu kundi la watu masikini wasio elimu wala huruma linawamaliza kama Warumi walivyokuwa wanafurahia gladiator games au rednecks wa Jim Crow South USA walivyokuwa wanafurahia kunyonga watu weusi.

Ukiwauliza kama kuna mtu kamuona anaanguka, utasikia wanakwambia "tumesikia".

Barbaric.

umeona? wengi wa hawa 'wachawi' ni mental disorder cases halafu tunakimbilia kuwaua
 
MCHAWI AKAMATWA DAR NA KUUAWA LIVE BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

December 23, 2013

15.JPG

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.

Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.

Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”

“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”

Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.

“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.

21.JPG

Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.


19.JPG

Wananchi hao wakimzonga mchawi huyo.

20.JPG

Kipigo kitakatifu kutoka kwa wanachi.

16.JPG

Kipigo kinaendelea hadi kupelekea umauti wake.

17.JPG

Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.

wanaoua kwa upanga watakufa kwa upanga, damu ya ndugu yangu kama amekufa itadaiwa mikononi mwao, alaaniwe yeye afanyaye matendo kama haya kwa binadamu wenzake na watu wote waseme amina
 
That is simple minded brain! Kwani Mama Rwakatare, Gwajima na Lusekelo ni waarabu au wana amini imani ya Kiarabu? Mwanzo umeongea hoja nzur tu kumbe umebahatisha hovyo kabisa ww!
Naamini hakuna dini yyt inayopropose wa2 kufanya uchawi ni mapungufu ye2 wanaadamu 2 na kutofikir sana ndio kunapelekea ujinga huu!
Huujui uislam weye
 
Hao waliomuua wamechukua maamuzi ya kijinga sana wanahukumu tu utafikiria kama hawana makosa wameniuzi sana.Nyie wenye tabia kama hizi mkome na muache mara moja.Mambo gani haya mnauwauwa watu ovyo kama vile hamna hatia.
 
Back
Top Bottom