Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo

Nalaani kitendo hiki cha kijinga na kipumbavu kwa nguvu zangu zote.wao walijuaje kwamba jamaa ni mchawi au kachanganyikiwa? Damu yake iko juu yenu enyi wapumbavu wa mbezi luis.
 
huyu mchawi ana tofauti gani na majangili,wezi wa mali za umma,mawaziri mizigo,wala rushwa,nk
mbona hatuwaui hao tunanganga na mtu alietumia utaalamu wake kusafiri wakati hajadhuru mtu?
nadhani wahusika wanaonekana katika hizi picha,walishika tofali na kumuua wachukuliwe hatua kali.
 
mimi ni mkazi wa Mbezi Luis. Namfahamu huyu kijana ni mkichaa wa siku zote na siku zote yuko hapa Luis. kosa lake siku ya tukio alivua nguo sasa kwa kua wananchi wa huku wana uchu wa kumwaga damu hata iwe ya kichanga ndio wakamsingizia ili wamtoe roho. Hivi we are grown ups. kweli kuna raia anaamini huu upuuzi wa kusafiri na ungo ? kama mnaamini basi mtaamini rais ajaye ni Kingunge ngombale

matunda ya Gwajima, Getrude Lwakatare, Mzee wa Upako..
 
Wakazi Wa Mbezi wengi wao ni walala hoi homeless People Watu wa vijiweni hawana kazi ya kufanya wanakwenda kumuwa mtu kwa sababu yupo uchi* sa ingine ni mgonjwa wa wenda wazimu huyu mwanamme? Wana Ushahidi gani kuwa huyu jamaa ni Mchawi? Mwenyeezi Mungu atawalipa malipo makubwa waliomdhulumu nafsi yake huyu jamaa damu yake haitokwenda bure waliofanya kitendo cha uuwaji watavuna kile walichokipanda inshallah.

Hilo lisikushangaze, Tanzania wanauliwa wazee kwa kuwa wana macho mekundu tu, wanaambiwa wachawi.
 
na jk aliangushwa na nini jukwaani wakati wa kampeni 2010! siyo kwamba ndiyo imani zenu?

Sijui, nikuulize wewe.

Imani yetu ni kujisalimisha kwa Allah, hazai wala hajazaliwa, akitaka husema tu, "Kun, Fa Yakun", "kuwa, na inakuwa".
 
Hapo utakuwa humtendei haki. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Unakumbuka kwanini Ali Hassan Mwinyi alijiudhuru wakati wa Nyerere? au ulikuwa hujazaliwa bado?

We FaizaFoxy Wacha ujanja ujanja wako wa mjini, jibu hizo tuhuma kama Jakaya ni binamu yako?


BTW mbona mie na ungo wangu huwa nafungua macho kutoka Alaska hadi Emirates ... .... .... wamemuonea tu thubutu nitatua Bongo new year nione kama watanifanya kitu!
 
Hii ina tofauti gani na wale watu wanaouliwa kwa kupigwa mitaani kwa tuhuma za wizi?

Ina tofauti gani, kimsingi, na yale matukio ya akina dada kupewa wakati mgumu mchana kweupe kwenye sehemu za hadhara kutokana na mavazi yao?

Tafakari.....
 
We FaizaFoxy Wacha ujanja ujanja wako wa mjini, jibu hizo tuhuma kama Jakaya ni binamu yako?


BTW mbona mie na ungo wangu huwa nafungua macho kutoka Alaska hadi Emirates ... .... .... wamemuonea tu thubutu nitatua Bongo new year nione kama watanifanya kitu!

Umelewa gongo?
 
na jk aliangushwa na nini jukwaani wakati wa kampeni 2010! siyo kwamba ndiyo imani zenu?

Sasa wewe hapa unajichanganya. Ukisema JK aliangushwa na imani za kishirikina ina maana kwamba na wewe unaamini hivyo halafu wakati huo huo unataka kutuaminisha kuwa huamini!!!!!!!
 
Ila badili kichwa cha mada. Huna uhakika kama huyo ni mchawi. Ilitakiwa ikae hivi, "Apigwa hadi kufa kwa tuhuma za uchawi" au kitu kama hicho.
 
Hii ina tofauti gani na wale watu wanaouliwa kwa kupigwa mitaani kwa tuhuma za wizi?

Ina tofauti gani, kimsingi, na yale matukio ya akina dada kupewa wakati mgumu mchana kweupe kwenye sehemu za hadhara kutokana na mavazi yao?

Tafakari.....

Toka lini Miafrika tuka-tafakari?

Miafrika Ndivyo Tulivyo.
 
Hizi imani za Kiarabu ni tabu sana.

That is simple minded brain! Kwani Mama Rwakatare, Gwajima na Lusekelo ni waarabu au wana amini imani ya Kiarabu? Mwanzo umeongea hoja nzur tu kumbe umebahatisha hovyo kabisa ww!
Naamini hakuna dini yyt inayopropose wa2 kufanya uchawi ni mapungufu ye2 wanaadamu 2 na kutofikir sana ndio kunapelekea ujinga huu!
 
Acheni use nge hii mbona ya zamani 2011 shenz kweli mleta maada, tena ilikuwa mbezi mazulu
 
jaman kama hujawahi kutembelewa na jamii za kichawi basi ni halali yako kulaumu watu kumshushia kipigo.
malipo ni hapahapa dunian.
hawa watu wanakutia uwaskini huku unacheka nao.
wanaharibu sana mimba za watu.
"wapigwe tu"
 
Watanzania ujinga unazidi kutumaliza, mtu
mwenye akili timamu hawezi kuamini huu
wendawazimu unaoitwa uchawi!!
Hivi kuna mtu alimshuhudia akianguka? Kuna mtu
anaweza kutuwekea picha ya huo ungo!? Mauaji
ya namna hii si ya kushabikia hata
kidogo...otherwise uwe na imani za kijingajinga !!
 
Back
Top Bottom