Mchawi akamatwa jijini Dar na kuuawa baada ya kudondoka na ungo

kwanza aina ya watu walio kwenye eneo la tukio ni ambao hawana kazi,ndo maana kwso hiyo ni shughuli.
 
Aisee hii mbaya sana ila sidhani kama hawa wananchi wenye hasira kali wamefanya sawa
 
Hapo utakuwa humtedei haki. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Unakumbuka kwanini Ali Hassan Mwinyi alijiudhuru wakati wa Nyerere? au ulikuwa hujazaliwa bado?

Hata huyu juzi alistahili kifinyo sawa na huyu.

Halafu nina hofu anaweza akawa na kadi ya ccm nyumbani kwake!
 
Safi sana, Maandiko ya biblia yanasisitiza kuwa , Mchawi asiachwe aishi.

Halafu tukisema dini zinachochea ugaidi tunasemwa, au watu wanafikiri tunaongelea uislamu tu.

Huyu mtu inawezekana kabisa ana matatizo ya akili au kachanganyikiwa kutokana na ugumu wa maisha, au ndugu zake wamembalasa nyumbani kwao.

Anahitaji mental health evaluation.

Kibongobongo anauawa hivihivi bila uchunguzi.

Kwa sababu ya a medieval piousness.

Biblia my foot!
 
..Kwa kweli inasikitisha sana kuona jinsi huyo kijana alivyo uwawa kikatili na wananchi,ni sababu gani ya msingi iliyofanya auawe?kwa maana amehukumiwa pasi na sheria kuchukua mkongo wake.Huenda kama angefikishwa kwenye vyombo vya sheria tungepata kufahamu mengi na kuujua huo mtandao.Sasa wamesha muua ndio iweje?Serikali inapiga sana kelele wananchi wasichukue sheria mikononi,si kwamba namtetea kwa vitendo vyao viovu lakini haikupasa kumuua,na wale wote walio shiriki kumuua wanayo kesi ya kujibu kesho kwa M.Mungu.Anae uwa pasi na sheria na yeye auliwe.
Hili tukio limenigusa na kuniumiza!. Kiukweli huyo jamaa was insane, ila hao watu nao ni kama mashetani fulani!, naamini miongoni mwao walikuwepo walioona kabisa kuwa huyo jamaa sio mzima!.

Tueneze elimu ya "karma" kuwa kila baya lolote utakalo lifanya duniani, utalilipa hapa hapa duniani!. Hata kama ni kweli ni mchawi na alikuwa kwenye safari zake, sasa mnamuua kwa kosa gani?!. Hatua ya kwanza kabisa ya kumpima insane ni dress code!. Kwa kuziona tuu hizo nywele, mtu yoyote mwenye akili timamu atajua huyo ni kichaa!. Hata kama ukichaa wake ni wa kuchukuliwa msukule, ila kwa macho ya kawaida tuu ile sura yale macho, utajua fika huyu sii mzima!.

Ukiondoa mob psychology ya wengine kufuata mkumbo, hata hao walioshiri kumuua pia nao ni vichaa fulani!. Siku zote nasisitiza humu, Tanzania tunao vichaa wengi kuliko tunavyojidhania, japo sio wote ni mpaka waokote makopo!.

Rip an innocent victim!, hakuna damu inamwagika bure, kila aliyeshiriki kwenye mauaji haya lazima atalipia tus, tatizo wakati wa maripo, yaani "the payback time", mtu anakuwa hawezi kukumbuka kuwa chanzo cha majanga yanayomkuta ndio malipo yenyewe ya udhalimu alioufanya, mtu atadhani ni majanga tuu ya kawaida, kumbe ndio fidia yenyewe ya "karma"
Paskali
 
mimi ni mkazi wa Mbezi Luis. Namfahamu huyu kijana ni mkichaa wa siku zote na siku zote yuko hapa Luis. kosa lake siku ya tukio alivua nguo sasa kwa kua wananchi wa huku wana uchu wa kumwaga damu hata iwe ya kichanga ndio wakamsingizia ili wamtoe roho. Hivi we are grown ups. kweli kuna raia anaamini huu upuuzi wa kusafiri na ungo ? kama mnaamini basi mtaamini rais ajaye ni Kingunge ngombale
Nakubaliana na wewe mkuu, hizo picha hazihitaji uwe na akili ya ziada kujua kama aliyeuwawa ni kichaa. Watanzania hatujielewi kabisa, na mpaka habari inatolewa kwenye gazeti eti mchawi kauawa. Very sad kwa huyu jamaa.
 
mimi ni mkazi wa Mbezi Luis. Namfahamu huyu kijana ni mkichaa wa siku zote na siku zote yuko hapa Luis. kosa lake siku ya tukio alivua nguo sasa kwa kua wananchi wa huku wana uchu wa kumwaga damu hata iwe ya kichanga ndio wakamsingizia ili wamtoe roho. Hivi we are grown ups. kweli kuna raia anaamini huu upuuzi wa kusafiri na ungo ? kama mnaamini basi mtaamini rais ajaye ni Kingunge ngombale

Mmmmmmmmh eti pana ukwelii apa embu ngojaa nika angalie magazeti ya mwananchi kama yalichapisha izi seko wiik hi
 
Hiyo dhana isiyo na ushahidi, mmemuonea, hakika kesho mtaulizwa juu ya hukumu hii mliyofanya. Mungu amlaze pema.
 
Hili tukio limenigusa na kuniumiza!. Kiukweli huyo jamaa was insane, ila hao watu nao ni kama mashetani fulani!, naamini miongoni mwao walikuwepo walioona kabisa kuwa huyo jamaa sio mzima!.

Tueneze elimu ya "karma" kuwa kila baya lolote utakalo lifanya duniani, utalilipa hapa hapa duniani!. Hata kama ni kweli ni mchawi na alikuwa kwenye safari zake, sasa mnamuua kwa kosa gani?!. Hatua ya kwanza kabisa ya kumpima insane ni dress code!. Kwa kuziona tuu hizo nywele, mtu yoyote mwenye akili timamu atajua huyo ni kichaa!. Hata kama ukichaa wake ni wa kuchukuliwa msukule, ila kwa macho ya kawaida tuu ile sura yale macho, utajua fika huyu sii mzima!.

Ukiondoa mob psychology ya wengine kufuata mkumbo, hata hao walioshiri kumuua pia nao ni vichaa fulani!. Siku zote nasisitiza humu, Tanzania tunao vichaa wengi kuliko tunavyojidhania, japo sio wote ni mpaka waokote makopo!.
Rip an innocent victim!, hakuna damu inamwagika bure, kile aliyeshiriki lazima atalita tatizo wakati wa payback time, huwezi kukumbuka ndio malipo yenyewe, utajua ni majanga tuu ya kawaida!.
Pasco.
Pasco.

Pasco
Haya mambo yanapaliliwa na viongozi wa hizi dini za kilokole na utapeli wa kufufua misukule. Hawa wakina mzee wa Upako matapeli wakubwa wanawajaza watu hofu na imani potofu za uchawi halafu watu hawawezi kufikiria tena. Inapotokea mchungaji anafanya utapeli kwa kujifanya sala zake ndio zimetungua mchawi aliyekuwa anapita na ungo watu wengi wanaamini. Au anapojifanya kufufua misukule! Huyo marehemu anaonekana kabisa alikuwa ni mgonjwa wa akili! Sijawahi kuona nchi inayoamini mambo ya ushirikina kama Tanzania. Kweli dunia ya leo kuna watu bado wanaamini kuna mtu anaweza kuruka na ungo angani! Nimeshangaa kweli kweli kweli!
 
mimi ni mkazi wa Mbezi Luis. Namfahamu huyu kijana ni mkichaa wa siku zote na siku zote yuko hapa Luis. kosa lake siku ya tukio alivua nguo sasa kwa kua wananchi wa huku wana uchu wa kumwaga damu hata iwe ya kichanga ndio wakamsingizia ili wamtoe roho. Hivi we are grown ups. kweli kuna raia anaamini huu upuuzi wa kusafiri na ungo ? kama mnaamini basi mtaamini rais ajaye ni Kingunge ngombale

................/??????????
 
Nyie endeleeni kumwaga damu ya kichaa isiyo na hatia kwa imani zenu za kishetani lakini tarehe 1 jan 2014 muandae elfu 20 ya kununua umeme unit 5,pumb.vu kabisa nyie.kama akili zenu ndio hizi naomba Mungu mafisadi wabakie madarakani kwa miaka 50 ijayo wawapeni darasa hadi muache ujinga!nyambaf kabisa!
 
Hili tukio limenigusa na kuniumiza!. Kiukweli huyo jamaa was insane, ila hao watu nao ni kama mashetani fulani!, naamini miongoni mwao walikuwepo walioona kabisa kuwa huyo jamaa sio mzima!.

Tueneze elimu ya "karma" kuwa kila baya lolote utakalo lifanya duniani, utalilipa hapa hapa duniani!. Hata kama ni kweli ni mchawi na alikuwa kwenye safari zake, sasa mnamuua kwa kosa gani?!. Hatua ya kwanza kabisa ya kumpima insane ni dress code!. Kwa kuziona tuu hizo nywele, mtu yoyote mwenye akili timamu atajua huyo ni kichaa!. Hata kama ukichaa wake ni wa kuchukuliwa msukule, ila kwa macho ya kawaida tuu ile sura yale macho, utajua fika huyu sii mzima!.

Ukiondoa mob psychology ya wengine kufuata mkumbo, hata hao walioshiri kumuua pia nao ni vichaa fulani!. Siku zote nasisitiza humu, Tanzania tunao vichaa wengi kuliko tunavyojidhania, japo sio wote ni mpaka waokote makopo!.
Rip an innocent victim!, hakuna damu inamwagika bure, kile aliyeshiriki lazima atalita tatizo wakati wa payback time, huwezi kukumbuka ndio malipo yenyewe, utajua ni majanga tuu ya kawaida!.
Pasco.
Pasco.

#Pasco huyu Jamaa ameonewa sana! sijui kwanini tunauwa badala badala ya kutumia akili! hata kama ni mchawi kweli ina maana tunaupenda uchawi sana au tunauchukia lakini hatujui namna ya kupambana nao.

Elimu ya uchawi africa inasemwa kama dhana lakini tumeshindwa kuidocument kwa ujinga wetu, tumekuwa wajinga kuliko kipimo, kama ni mchawi kweli kwanini tusimtunze ili tupate abc za uchawi ili kama tunauchukia basi tuujue maana huwezi kupambana na tatizo ambalo hulijui vyema. Sio kuwa alikuwa darasa tosha hata la kuwapa watu PhD!? Ujinga wetu ndio majanga yetu. RIP man umeuwawa kwa uzembe bila kutiwa hatiani.

Roho na mwili vimetengana, lakini unge kuwa wa faida gani wakati duniani sote tunapita.
 
Nahisi akili za waliomuua huyo jamaa hazikai kichwani, Na watu wa eneo hilo wote wapuuzi, na askari polisi wanawachekea au wazembe kama alivyosema shuhuda mmoja aliyekuwepo eneo hilo.Kwasababu picha zinaonesha watuwaliokua wanampiga jamaa ni watu wachache katika kundi la watu wengi waliokua wanashangaa watumie picha kuwakamata. basi utasikia unatufundisha kazi, ndo zao wanatumia neno wananchi wenye hasira ili wasitumwe kwenda kuwakamata waharifu.Tanzania hakuna mwananchi mwenye hasira hata mmoja na wangekuwepo Mafisadi wasingetamba. Hivi sababu hasa ya kumuua nipi?!! Watanzania tulipofikia sasa ni pabaya na mwisho wa haya ni mbaya zaidi. Haiwezekani kumuua mwenzako kwa jambo la kuanguka na ungo bali ilikuwa kumhubiria ili amjue mungu na aache na mwisho wa siku tuwenae katika kujenga Taifa. Hao waliomuua wako safi katika matendo yao hapa duniani. Na pengine kwa tabia ya watanzania sisi huo ni uzushi mtupu walikua na sababu nyingine wakaona wamsingizie jambo ili wamuue. Ila mungu atahukumu, ole wenu wenye hasira za kijinga.
 
MCHAWI AKAMATWA DAR NA KUUAWA LIVE BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

December 23, 2013

15.JPG

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.

Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.

Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”

“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”

Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.

“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.

21.JPG

Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.

19.JPG

Wananchi hao wakimzonga mchawi huyo.

20.JPG

Kipigo kitakatifu kutoka kwa wanachi.

16.JPG

Kipigo kinaendelea hadi kupelekea umauti wake.

17.JPG

Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.
Wakazi Wa Mbezi wengi wao ni walala hoi homeless People Watu wa vijiweni hawana kazi ya kufanya wanakwenda kumuwa mtu kwa sababu yupo uchi* sa ingine ni mgonjwa wa wenda wazimu huyu mwanamme? Wana Ushahidi gani kuwa huyu jamaa ni Mchawi? Mwenyeezi Mungu atawalipa malipo makubwa waliomdhulumu nafsi yake huyu jamaa damu yake haitokwenda bure waliofanya kitendo cha uuwaji watavuna kile walichokipanda inshallah.
 
Back
Top Bottom