Mchango wangu mchakato wa katiba na siasa za Tanzania, wewe je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchango wangu mchakato wa katiba na siasa za Tanzania, wewe je?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmh, Mar 5, 2011.

 1. mmh

  mmh JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 852
  Likes Received: 652
  Trophy Points: 180

  · Ombea mchakato wa katiba mpya ya nchi yetu ili kuondoa vigezo vilivyo kwenye katiba iliyopo vilivyo na udhalimu kiutendaji kwa manufaa ya kundi dogo,chama au maslahi ya mtu binafsi Zab 7:26-27
  · Ombea tume itakayoundwa na Rais, isitende kwa hujuma na kwa maslahi ya kundi dogo, chama au mtu binafsi.
  · Ombea maoni ya wananchi yaweze kuzingatiwa, na isifanyike tu kama ushahidi na kutoa taarifa tofauti (ya uongo) na kusema ni maoni ya wananchi. Yosh 9:12-14
  · Weka upeo wa kiMUNGU ndani ya wananchi ili mapendekezo yao yawe yenye mantiki kwa manufaa ya nchi na yenye kuujenga UFALME WA MUNGU.

  · Kumbuka KATIBA NI AGANO KATI YA MWANANCHI NA SERIKALI YAKE, Ebr 7:11,12,18. Omba sana ndani ya mchakato huu wa katiba usiwe njia ya kuingiza sheria na taratibu za kishetani, bali iwe ni njia/mlango wa kujenga na kuuleta UFALME WA MUNGU.

  · Ondoa kabisa madaraka ya rais wa Tanzania/Tanganyika yanayompa udikiteta kisiri katika mfumo wa uteuzi wa viongozi kitaifa. Dan 7:26

  · Ondoa kinga juu ya Rais na viongozi wakuu wa serikali ya kutoshitakiwa pindi anatumia vibaya madaraka au anapouhujumu uma.Rum 1:

  · Ondoa kwa viongozi wa serikali kusimamia na kutetea chama badala ya kutetea maslahi ya wananchi hata kama kuna ubadhilifu na hasara kubwa.

  · Weka wana wa MUNGU sasa kumiliki nchi na kushika nyongozi na nyadhifa mbalimbali katika nchi. Dan 7:27
   
Loading...