Mchango wangu kwenye Star TV juu ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Nimeshiriki kidogo kwenye mjadala ndani ya Star TV mapema asubuhi Ijumaa hii nikichambua kwanini Sheria hii ni mojawapo ya sheria mbovu kabisa kupitishwa na Bunge letu, ikiwa na lengo la kudumaza demokrasia, kuzuia Wagombea huru na kudhibiti wagombea wa vyama kutumia haki yao ya kujieleza.

Nitaandika kwa kirefu nikichambua vifungu vyake mbalimbali na athari zake kwa demokrasia changa ya Tanzania na ni kwanini naamini Rais Kikwete ahakikishe kuwa Bunge linapokutana tena Aprili sheria hii inafanyiwa mabadiliko kabla ya kuanza kutumika baadaye mwaka huu.

Sikiliza hapa:
 
Kila la heri MKJJ, kwa tunaoamini Mungu , tunasema ........Mungu akutangulie, akupe afya, na ujasiri wa kueleza yoote mema.
 
kwa sisi tulioko nje ndio kusema tunasoma tu hapa baada ya hicho kipindi sio??

Kila kheri, Mungu ujasiri useme kile kilicho moyoni mwako.
 
Hii ndio dunia ya ujasusi naamini tutafundishana mengi tupate kuwa na majasusi wengi zaidi nchini
 
Nakutakia mafanikio mema hii ni kuonyesha kuwa hata mawazo ya JF yanaweza na yameanza kutoka nje na kuwafikia wananchi walio wengi big up MMKJ.
 
Safi sana mzee natumaini utachangia kikamilifu ila jitahidi kutujuza mazungumzo japo kwa ufupi kwani huku nje Tv za bongo haiwezekani hata kwa DSTV 143, tbc1 inagoma!
 
siyo mwanasiasa mimi...

Inawezekana kweli usiwe mwana siasa kama ulivyoandika. Ila ukweli ni kwamba, kuna mstari mwembamba sana kati ya watu kama wewe na mwanasiasa. Nyie watu kuvuka mstari na kuingia Dark Side (Star Wars) ni rahisi sana na matamanisho ni makubwa sana. Inataka uwe na roho ngumu saana hasa kwa nchi kama yetu ya Tanzania.

Naungana na wale wote waliosikitikika siku umeondoa hiyo avatar. Nilipojiunga tu na kuiona kwa mara ya kwanza, nilijisikia nipo nyumbani. Kama ungeliweza basi ifanyie kabisa TRADE MARK. Siku zote itabaki kuwa moja ya ALAMA moja wapo maarufu ya JF.

WALA USIOTE TENA KUIBADILISHA. Siku CCM ikifa, basi iwekwe kwenye Jumba la Makumbusho la Taifa pembeni mwa JF.
 
Nitawawekea sehemu ya audio ya mahojiano kutoka upande wangu, within the next 45 minutes
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom