Mchango wangu kwa serikali kufikia lengo la trilioni mbili kila mwezi

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
Inafahamika kwamba kila siku duniani kote wafanyabiashara wanapanga mbinu za kila aina kuweza kukwepa kodi,ndio maana watu kama Ronaldo na Messi wamewahi kukamatwa na kushtakiwa kwa kukwepa kodi,

Kama tumeamua kuwabembeleza wafanyabiashara, basi kuna mambo mawili ya kufanya mdaiwa asipolipa kodi kwa wakati,

1-Mdaiwa asipolipa kodi kwa wakati deni lianze kuongezeka, atakaa akijua deni lina riba na lazima alipe kwa maendeleo ya Taifa maana nchi ama taifa halina biashara wala chanzo kingine cha mapato zaidi ya kodi,kodi zetu hizo ndio zinalipa watumishi wa umma wanaotembea kwenye mav8.

Tunaweza kurudi nyuma enzi zile za mtokambali baada ya ruksa, Iwe tu kama enzi zile magari yanalipiwa Motor Vehicle Licence,muda ukipita haujalipa utakutana na adhabu kali na adhabu hizo hazikomi hadi ulipe,na watu waliheshimu sana hilo,na trafiki walifanya kazi yao vizuri kutimizwa kwa adhabu hizo.

2. Jambo la kwanza linaposhindikana ndio uja kukufungia duka,Sasa kama mazingira ya biashara ni mazuri naamini hakuna Mfanyabiashara atayekubali kufungiwa duka.

Nashauri pesa zote za umma ambazo ni kodi,ziwekewe adhabu kali na isiyo na kikomo kwa wale wote watakaoshindwa ku meet deadline.

Hii itaondoa usumbufu na lawama nyingi Serikalini, Lawama kama Serikali kufungia biashara nk hazifakuwepo.

Ukweli ni kwamba mamlaka za Serikali mara nyingi sana zinatupiwa lawama na lawama hizo zinaonekana ni kweli bila kusikiliza upande wa pili.

-Uadilifu kwa wakusanya Kodi.

Mimi nipo Kariakoo,katika shughuli zangu,kila siku nakutana na wafanyabiashara wengi tu Wazambia,Wamalawi,Wakongo,Wakenya,warwanda na Waburundi,awa wanakuja na kuondoka,lakini nakutana na wafanyabiashara wenyeji na Wachina ambao wana Residence permit na working permit, sasa wakusanya kodi sio waaminifu kwa wafanyabiashara awa, Mfanyabiashara mgeni mfano Mchina anaambiwa unadaiwa kodi Milioni 600 akilalamika wanamwambia wewe una shilingi ngapi,anataja nusu bei,

Milioni 300 sasa mpaka hapo kodi halisi wanaijua wao, wanamwambia toa milioni 200 chakula au toa yote Milioni 600,mchina anatoa 200 jamaa wanasepa na hela naamini hela kama hizo zimepotea hazijawahi kufika popote Serikalini,huu umekuwa mtindo hata kwa wafanyabiashara wazawa wasio waaminifu wanawaendea wanawapiga kodi hadi Mfanyabiashara anapata BP halafu wanampunguzia alipe nusu naamini akilipa hela hiyo inapotea na haifiki popote Serikali, wafanyakazi hao wakusanya kodi wasio waaminifu nawaonaga kila siku hakuna anayelala na njaa,tunawaamini lakini sijui kama ninyi ni Wazalendo kwa taifa letu la Tanzania.

Ningefurahi Serikali iache sheria na nguvu kadiri inavyowezekana itumike ili Serikali ipate kodi yake na kuendeleza miradi lakini nimeona pia kutumia nguvu kunatumiwa vibaya na wakusanya kodi wasio waaminifu kwa manufaa yao binafsi na maslahi yao binafsi, hivyo basi napendekeza approach iangaliwe upya.

Ndio tumeona Ulaya kina Messi na Ronaldo wakishtakiwa kwa kukwepa kodi,hivyo tunapata funzo kuwa kutegemea kodi itapatikana kwa kubembelezana na wafanyabiashara ni kujidanganya kabisa, hasa kwa wafanyabiashara na wananchi wa nchi yetu Tanzania ambao hawana kabisa Utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari bali shuruti, tuliona mifano mingi bandarini na tuliona matajiri wengi wakiibuka miaka kumi iliyopita kumbe wote walikuwa wakwepa kodi, kumbe tufanye siasa kote lakini kwenye kodi ili nchi iende mbele tuwaachie TRA Wafanye kazi yao kwa weledi na kwa uaminifu wanapodhihakiwa ndipo tuwaongezee nguvu ya vyombo vya dola.

Kodi na pato la Taifa ukijulisha na miundo mbinu yote katika nchi na miradi mikubwa ukiigawanya kwa idadi ya Watanzania Milioni 60 tunapata pato ambalo limetupeleka kwenye uchumi wa kati, hivyo basi tusicheze kabisa na vyanzi vya mapato ikiwemo kodi,China ya leo ni maono ya Mao Zedong na hata sasa kodi na mapato ya nje ndio mhimili wao kiuchumi hata kuipita Marekani.

Hakuna vita mbaya kama vita ya uchumi hasa kupitia ukwepaji kodi ndio maana Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli alijenga ukuta Mererani, akajenga masoko ya dhahabu, akaenda hadi bandarini yeye mwenyewe kukamata wakwepa kodi wakubwa waliokuwa wanaingiza bure bidhaa mbalimbali hata pure oil wakisingizia ni crude cooking oil na kukwepa kodi ya mabilioni.

Sasa tukirejea hayo,kwa mtazamo Wangu TRA wanatakiwa waongezewe nguvu kubwa kuhakikisha kodi inapatikana kwa mujibu wa sheria, suala la kodi halina mjadala ni muhimu sana kwa uchumi na maendeleo ya Taifa letu la Tanzania,tukileta siasa kwenye kodi Serikali itapoteza mapato mengi sana.

-Lengo la kupata Trilioni 2 kila mwezi.

Nina mode nzuri mno ya kusaidia serikali kuingiza mapato katika majiji yote nchini.Nimetafiti nimejiridhisha ndio nika share,Jam na namna ya kukusanya pesa ninayo njia ya kushauri. A very modern one. Automated ways ya kutambua na ku receipt magari yote 24/7
Labda kama itasubili watoto wa mjini aka wapigaji waje na proposal wapi he hela, Mimi yangu ni bure,Kama kila siku ubungo yanapita magari 60,000. ( nime Google) njia ya gemeld, Kigamboni, Pugu Maana yake ni sure kila siku magari 100,000 ya naingia jijini. Kwa kila Gari 200. Piga kwa mwezi.Huo ndio mchango wangu kwa taifa.

Kama kuna mtu ana gari na hawezi kulipa 200,basi hasiingie na gari lake mjini,gari sio basic need labda utashindwa kuishi au kufanya kazi,zipo Mwendokasi na treni ya SGR,Exception kwa gari za biashara. Hii itasaidia pia kujua tax bubu nk,

5M kwa kila jiji ni 25M majiji 5. 125M kwa mwezi. Hiyo ni robo ya uhalisia,katika zile 2T inasaidia kuongeza,zaidi ya hapo kuna mwendelezo mwingine to make it 500M kwa mwezi no doubt.Majiji yetu yatapinguza foreni na yatakuwa na amani kwa shughuli nyingine na watu watakuwa na akili fresh wanapoingia ofisini kufanya kazi,

The whole deal,iItaongeza 1B kwa mwezi no doubt. Kwa kadirio la robo ya uhalisia,lazima tuwe na utaratibu,na utaratibu huu utatupa nafasi za utulivu maofisini, na sio lazima kuja mjini na gari yako,kuna shida kubwa inakuja mijini Ikiwa udhibiti wa magari yanayoingia mijini hautakuwepo.

Kuelekea kupata Trilioni mbili kwa mwezi, Magari yote yaingizwe na yahusiane na utambulisho wa NIDA( kama bado).Mfano kwa Dar atakayeingia na private car kutoka Morogoro akifika Mbezi,kimara alipe sh 200 kama ndogo Shilingi 200 basi iwe 500 iwe hivyo ataepita daraja la Tazara, Daraja la Kigamboni, Daraja la Tanzanite na Daraja la Kigongo feri, Alipie shilingi 200 au 500 Atakayeingia Fire, kamata nk alipie 500. Kwa mawazo yangu Usafiri wa Mwendokasi uboreshwe, phase zote 4 zikamilishwe haraka ili wazo hili liweze kufanya kazi kusaidia watu kuingia mjini bila magari yao binafsi, Ita punguza msongamano, tujenge taifa la walipa kodi,wataolipa kwa bill,basi bill hizo zitumwe kwa njia ya sms,itasaidia kuondoa usumbufu wa kuazima gari au watoto kuiba magari ya wazazi usiku,

We take charge kujenga nchi yetu,Wazo limekuja baada ya kusikia takwimu za idadi ya magari kwa siku katika daraja la ubungo,na wakati huo huo kusikia target ya mapato kufikia Trillioni 2 kila mwezi,Naamini Inawezekana maana vyanzo vya mapato ni vingi na kimoja wapo ni hiki chanzo ninachokizungumzia hapa,ni aibu mtu kuwa na gari la milioni 10 kuweka petrol ya lita kwa shilingi elfu mbili halafu ushindwe kulipa 200 au 500 kuingia mjini,hii pia itasaidia kutengeneza vipato, kwa watu wa car packing kabla ya kuingia mjini,pia itasaidia biashara ya mabasi ya Mwendokasi kupata wateja na pia daladala binafsi kupata wateja,

Nimalizie tozo ya vifurushi kwenye mitandao ya simu,madhara ya kuongezeka kwa gharama za mawasiliano yanashusha ufanisi wa mapato kwa sector nyingine pia. Hili suala naamini litatazamwa upya, Wizara husika itambue umuhimu wa wizara nyingine pia,vnginevyo ni sawa na kuhamisha pesa mfuko mmoja wa kushoto kwenda kulia na sio kuongeza,Biashara za wanaotegemea mtandao zikishuka Maana yake pato la nchi pia linashuka. Hakuna tija yena katika kuongeza makusanyo. Sector zote zinategemeana.

MAWAZO YA KUSAIDIA: kuwepo na mgawanyo wa aina za matumizi na bei zake. Simu za biashara zisajiliwe na zipewe nafuu kama zamani na simu binafsi ndio zifikiriwe ongezeko, Nimalizie kwa kuuliza Ule MKONGO WA TAIFA. Miaka ya 2000 walichimba na kuzika fiber cables nchi nzima ulishaanza kazi? Umekuwa na manufaa?? Sijui kama mnakumbuka zoezi hili,nina Imani na TTCL lakini kama haina mpango hivi kujitanua kimasoko, mfano tu tpesa na vocha zao sijui zinapatikana wapi, sioni matangazo yao.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Risala ndefu lakini hakuna cha maana, bali uwongo mwingi.

Hujui hata kilichobadilisha uchumi wa China, umebakia kusema uwongo kuwa ni mawazo ya Mao. Hujui chochote juu ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa na China katika kuruhusu uwekezaji mkubwa wa mataifa ya Magharibi nchini China, na athari zake chanya kwenye ukuaji wa uchumi wa China.

Nitajie angalao makampuni mawili yaliyopo katika top 10 yanayomilikiwa na Wachina.

Nitajie pia angalao nchi 3 zilizokuwa maskini halafu zilibadilika na kuwa na maendeleo makubwa kwa kuobgeza ukubwa na uwingi wa kodi.
 
Nitaanza kulipa kodi halali siku nikisikia ripoti ya CAG inasema hakuna taasisi yoyote ya serikali iliyopata hati chafu.
 
Back
Top Bottom