Environmental Security
Senior Member
- May 21, 2020
- 181
- 261
Habarini wanajamii intel...
Leo nimeona ni vema namimi kutoa contribution yangu kwa idara yetu nyeti ya usalama wa Taifa juu ya usalama kutoka katika mrengo wa kimazingira - Environmental Security
Kabla sijaendelea naomba kudeclare;
*Mimi ni kijana MTANZANIA mzalendo kwa taifa langu.
*Mimi ni mmoja kati ya watu ambao ninaridhika sana na utendaji na uimara wa idara yetu nyeti ya usalama wa Taifa na ninaamini hivyo.
*Naamini idara imara ya usalama wa Taifa ni msingi muhimu wa uimara na maendeleo ya taifa katika nyanja zote
*pia Naamini idara ya taifa letu imejitosheleza vema lakini bado naweza pia kuongeza mchango wangu wa mawazo kama yanaweza kusaidia kuboresha mahali
Nijielekeze ktk mchango wangu.
Environmental Security kwa kiswahili rahisi ni kama nilivyoeleza hapo juu kuwa ni Usalama kwa mrengo wa kimazingira
Nipende kusema kuwa kuna uhusiano wa karibu sana na wa moja kwa moja kati ya uharibifu unaotokea katika mazingira na usalama katika taifa, na hii ni katika short-run na long-run, kama tunavyojua Usalama ni ile hali ya kuwa salama (safe and free) kutoka katika hali na aina zote za hatari, uhatarishi, madhara, hofu au matisho ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu, mali au jamii kwa ujumla. Kwa kutumia maana hiyo rahisi ya usalama tunaweza sasa kujua kuwa uharibifu wa mazingira una uhusiano wa karibu sana na suala nyeti la usalama katika taifa lolote.
Uharibifu katika mzingira ni suala pana sana kutokana na ukweli kuwa mazingira yanajumlisha vitu vyote vinavyotuzunguka, hii inaweza kuhusisha uchafuzi wa mazingira kwa kupitia taka zinazozalishwa katika miji hasa makazi, masoko na sehemu nyingine za biashara, uchafuzi wa hewa, taka ngumu na vimiminika kutoka viwandani na migodini, uharibifu unaotokana na kilimo, mipango mibovu au kutokuwepo kabisa kwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na mengine mengi sana ambayo sitoyaorodhesha hapa
Mifano:
Sitaeleza kwa kina sana ila nitagusia ili nieleweke
●Migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu, kwa kiasi kikubwa ina uhusiano wa kimazingira ambapo watu huondoka maeneo yaliyoharibika kimazingira na kuelekea maeneo mengine yenye rutuba ambako pia wanakuta mipango mibovu au haipo ya matumizi bora ya ardhi hivyo kupelekea kuzuka kwa migogoro hiyo ambayo huleta madhara kwa maisha ya watu, uharibifu wa mali, kuongezeka uhasama hivyo kuathiri hali ya usalama. Ashukuriwe Mungu huwa haienei sana na huwa inadhibitiwa.
●Migogoro ya wananchi na wawekezaji hasa maeneo ya migodi, viwanda na mashamba makubwa (plantation) mf. nyamongo, kapunga na maeneo mengine yenye viwanda na shughuli kama hizo. Ukichunguza kwa makini utagundua kuna uhusiano wa migogoro hiyo na uharibifu wa mazingira
●Migogoro ya wananchi na miradi mikubwa ya maendeleo, hii kwa kiasi inasababishwa na kutozingatiwa kwa ripoti za tathmini ya athari za kimazingira (EIA /SIA) hivyo mapendekezo kutofanyiwa kazi ipasavyo
●Migogoro ya wafugaji na hifadhi za taifa au mapori ya akiba - mipango mibovu ya matumizi bora ya ardhi na uharibifu wa mazingira uliopelekea kukosekana kwa malisho
●Migogoro ya ardhi
●Ongezeko la wasio na ajira kutokana na uhamiaji toka maeneo ya vijijini kuja mijini na kupelekea uhalifu na uvunjifu wa amani kutokana na vijana wasio na kazi waliokimbia kilimo kisicho na tija vijijini na uzalishaji hafifu uliotokana na uharibifu wa mazingira au mipango mibovu ya matumizi bora ya ardhi vijijini
Na mifano mingine mingi ktk taifa letu. Huko duniani usiseme juu ya mto Nile na yanayoendelea, kuna migogoro Philippines, maji middle east, uharibifu wa misitu carribean n.k
NB: katika ulimwengu wa usalama hakuna sababu za moja kwa moja za kupelekea machafuko katika taifa ambazo hizo pekee ndio hasa chanzo, lakini kila sababu ya migogoro isipochukuliwa kwa uzito stahiki inaweza kupelekea machafuko. (Hata za kimazingira)
Duniani wenzetu wanafanya nini juu ya hili;
▪Umoja wa mataifa - UN kupitia shirika lake la mazinugira (UNEP) wamehakikisha kuwa ishu ya usalama katika mrengo wa kimazingira linapewa kipaombele "The General Assembly Resolution 42/186 mandated UNEP to deal with the issue; Paragraph 86 of the
Resolution reads: “One of the roles of the United Nations Environment Programme is to promote
environmentally sound development in harmony with peace and security, and towards this end, issues of
disarmament and security, in so far as they relate to the environment, should continue to receive appropriate attention".
▪NATO pia wamelichukulia suala hili kwa uzito tena kwa muda mrefu. "The North Atlantic Treaty Organization (NATO) and its Committee on Challenges of Modern Society (CCMS) organised a workshop on ‘Environmental
Security in an International Context: Environment and Development Policy Responses’.14 The workshop
recognised monitoring compliance as a crucial issue in environmental politics and stressed the need for
capacity building as a major part of a strategy to combat environmental threats to security"
Naweza kusema suala hili lilianza kupewa uzito mara tu baada ya kumalizika kwa miaka ya vita baridi, na kwa sasa sehemu kubwa ya dunia wanialitazama kwa uzito katika sera zao na hasa katika vyombo vyao vya usalama (angalia Biden ambavyo amelipa uzito suala la climate change, mapema kamteua John Kerry)
Environmental Security Ni suala muhimu sana na nyeti katika kuhakikisha taifa linakuwa salama. Ningeweza kueleza kwa kirefu na kina zaidi sana juu ya hili lakini nimejaribu kugusia walau kutoa mwanga na picha ili mchango wangu ufike ipasavyo na ninatarajia kuendelea kueleza kupitia nyuzi mbalimbali humu huku nikiamini haya yanazingatiwa na wahusika.
MCHANGO WANGU NI:
Sifahamu sana muundo wa idara yetu nyeti ya usalama wa Taifa na mipangilio mingine ya ndani, ila nina uhakika ni idara iliyojipanga vema sana lakini ningeomba kama inawezekana kuwepo na kitengo kamili cha Environmental Security katika idara yetu nyeti ya usalama wa Taifa, ili iwepo mikakati madhubuti ya kuhakikisha suala hili linachukuliwa kwa uzito stahiki hata kama halijaonesha kuwa na impact kubwa ktk taifa letu kwasasa.
Uwepo wa kitengo maalum cha Environmental Security ndani ya TISS itasaidia sana kufanya informed decision zinazoweza kuwa na uhusiano wa kimazingira. Sera zetu zitazingatia hili, uwekezaji na miradi mbalimbali pia itazingatia hili, kutakuwepo na ubadilishanaji wa taarifa, pia mitaala yetu itazingatia hili maadamu linachukuliwa kuwa issue of national security
Pamoja na masuala mengine kama siasa, uchumi, mambo ya kijeshi, ugaidi, na mengineyo ambayo yanaangaziwa moja kwa moja na idara zetu za usalama, naomba suala la Environmental Security rasmi liwe issue ya kimkakati kiusalama katika taifa letu.
Kwa leo napumzika hapa na naahidi kuanza kwenda deep kidogo ili mchango wangu uwe na maana.