Mchango wangu kuhusu nafasi za ajira kwenye taasisi za muungano

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Makubaliano yanasema kwenye taasisi na wizara zote za Muungano ajira iwe Zanzibar 21% na Tanzania 79%.

Issue hapa naona haijakaa sawa maana mzanzibari anaweza kuingia kwa hizo 21% lakini pia hiyo asilimia 21% ikijitosheleza anaweza kuingia kwenye taasisi hiyo hiyo kama Mtanzania maana nae ni mtanzania.

Upande wa pili Mtanganyika anagombea 79% iliyobaki pamoja na mzanzibari mtanzania mwingine aliyeshindwa kuingia kupitia ile 21%.
Wakati haya mambo yanajadiliwa viongozi wetu wa Tanganyika wanakuwa wapi? Je tunapeleka watu gani kwenye mijadala ya mambo ya msingi kama haya?

Wazanzibari sasa hivi wanaajirika hata kwenye wizara zisizo za muungano sababu wao ni watanzania ila kijana wa kitanganyika akienda Zanzibar haajiriki serikalini hadi awe na kitambulisho cha uzanzibari mkazi.

Haya mambo tusipoyaangalia vizuri wajukuu zetu watatulaumu sana.
 
Kuwe na bodi ya ajira ya jamhuri ya muungano ambayo itasimamia ajira zote kwa vigezo sawa bila kuangalia pande za muungano
 
Back
Top Bottom