Mchango wa Zitto Bungeni Julai 15: Madini, na Tatizo lake na mwitikio wa Symbion | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchango wa Zitto Bungeni Julai 15: Madini, na Tatizo lake na mwitikio wa Symbion

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 17, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hii ni sehemu ya hansard ya siku ya Julai 15, 2001 (Ijumaa iliyopita) ambapo Zitto alipata nafasi ya kutoa mchango kwenye mapendekezo ya bajeti ya Nishati na Madini. Amezungumzia kwa kirefu kuhusu sekta ya madini na kidogo amegusia suala la umeme. Maangalizi yake kuhusu suala la madini, mambo ya kodi kwenye sekta hiyo na hasa haja ya kuhakikisha kuwa utaratibu unawekwa ili kuwezesha dola kubakia nchini ni ya kuzingatiwa kwani ilivyo sasa naweza kusema (kama nimemuelewa vizuri) kuna "dollar flight" kitu ambacho kimechangia kukosokena kwa dola na hivyo kufanya bei ya dola nchini kuwa juu - hili lina matokeo makubwa kiuchumi.

  Zaidi ya yote (na hapa amenigusa vizuri) ni kutaka serikali ifikee mahali iache kuzungumza na makampuni ya madini. Kimsingi anauliza haya mazungumzo ya tangu 2006 hayakomi tu? Amezungumzia mengine mengi japo kwa kupita au kwa haraka sababu ya constraint ya muda. Je yuko sahihi? na wapi anakosea?

  Kwa maoni yangu, amekosea sana katika suala la Symbion. Baadhi yetu hatukuwa na tatizo na Dowans kwa sababu ya mitambo chakavu - kwa upande kwa mfano, sijawahi kuwa na issue na uchakavu wa mitambo ya Dowans. Wengi tulikuwa na tatizo na Dowans na Serikali kwa sababu mbili kubwa tu - mchakato wa Dowans was corrupt, na corruption can not be rewarded. Hivyo tukakataa serikali kufanya biashara na Dowans on that simple fact.

  Symbion haijaingia kilaghai kama ilivyo ingia Dowans na unlike Dowans, Syimbon kama shirika linalofanya kazi na US government na kama shirika la Kimarekani linafungwa na sheria za Marekani zinazozuia makampuni yake kujihusisha na rushwa ya namna yoyote. Lakini zaidi ni kuwa Serikali ya Tanzania haijanunua mitambo ya Dowans kitu ambacho yeye alikipendekeza na sisi wengine kukipinga. Symbion ndio iliyonunua mitambo hiyo bila ya fedha za Watanzania kuingizwa tena kwenye mifuko ya makuwadi wa ufisadi wa Dowans wakiongozwa na kina Al Adawi na Rostam. Hivyo, basi serikali imefanya exactly kile ambacho sisi wengine tulikitaka, KUTOKUFANYA biashara na Dowans.

  Nafikiri katika hili ni sisi wengine tumekuwa sahihi.

  Hata hivyo, kama Symbion ina tatizo jingine- ambalo kwangu naona ni la aina mbili hasa kuhusiana na hukumu ya mahakama na pili ushindani wa kuweza kuingia nchini. Hili hata hivyo kama ni tatizo na ni la msingi haiwezekani kuwa ni kwa sababu ya Wamarekani. Nimesikitika kidogo ku-tubait na hoja ya Umarekani kwa sababu kila mtu anajua kabisa kuwa kabla ya Dowans kampuni ambayo ilituingiza kwenye vurugu zote hizi ni Richmond, ya Houston Texas, Marekani. Kumbe hoja ya Umarekani haina msingi in the context of what has transpired so far kwenye suala hili.

  Kwenye hoja ambayo ameisema kwa kupita tu kuwa
  Maoni yangu bado ni yale yale.
   

  Attached Files:

 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwani zitto akichukua nchi au vijana kutakuwa na mabadiliko hapa nchi?..IMO
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena mwanakijiji, zitto anaweza kuthibitisha, symbion imenunia zile jenereta kama kampuni binafsi, imefunga network zake sasa itauza power time zake kule tanesco kwa makubaliano, kidog alitoka nje maana tulichopinga na ambacho ndio kimekuwa serikali tuliikataza kununua mitambo hiyo na haijanunua mitambo hiyo kwa kodi zetu. Katika hilo sikumbuki kama zito alishawishi kampuni binafsi ndio inunue kama ilivyotokea au alitaka serikali ndio inunue. Kimsingi kama tukipata more symbion tutakuwa mahala pazuri maana kitakachobaki ni kuwaregulate tu ktk price basi tunasonga mbele. Katika mada zingine zitto alinivuta by 100 pct, kuhusu dola kaeleza vema sana, kuhusu madini safi sana. Thanks mwanakijiji kumbe tuko pamoja
   
 4. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  sasa huyu kaka yetu zito sijui tumuweke kundi gani. ina maana hajui kwamba ata richmond ilisajiliwa huko marekani anakodaikuna sheria zisizoruhusu makampun ya huko kupokea au kutoa rushwa.?
  this is s.t.up..dity. kusifia kwamba symbion ni halali, basi tupewe ata mkataba wao ukoje kimaslahi ili wananchi wote wajue.
   
 5. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Naibu Spika, nimeiambia Serikali mara kwa mara, kwanza sijui
  kama nitawahi kumaliza. Sasa hivi tuna SYMBION inazalisha umeme sijui megawati
  ngapi kupitia mitambo iliyokuwa ya DOWANS, mitambo hii tuliambiwa ni mitambo
  chakavu na kelele zilipigwa sana na wengine tulipewa majina mengi sana. Leo sisikii
  mtu kila mtu ameufyata, nobody is saying anything kwa sababu sijui ni Wamerikani.
  Lakini mimi I am happy kwamba niliyoyasema mwaka 2009 mnayatekeleza mwaka
  2011. Tumeumia sana. Lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba kabla sijaondoka
  duniani limeonekana nililolisema na watu wote ambao walikuwa wanapinga wanaona
  aibu hawasemi sasa hivi. Sijui kwa sababu Mmarekani amechukua, we don't know.

  Hapa miwsho Zitto alichemka! Amejenga hoja vizuri kuanzia mwanzo hasa katika eneo hilo ambalo kwa kweli hata ukizungumza naye au ukimsikiliza utajua kuwa amelisoma vizuri na kulielewa (masuala ya madini, hasa katika kudeal na hizo multinationals companies namna yanavyotuibia na namna tunavyoweza kukuza uchumi wetu kupitia sekta hiyo). Wakati ule alisema/alishauri serikali inunue mitambo ile, wakai bado tunagombana na rushwa iliyokuwa ikinuka dhahiri katika Dowans ikitokea Richmond. Wakati ule alisema serikali inunue mitambo ile hata kama ikibidi kuvunjwa au kubadilihswa kwa sheria ya PPRA, lakini sikumbuki kama atika deal la Dowans to Symbion, kuna sheria yoyote ya manunuzi imevunjwa au kubadilishwa.

  Wengine kwa kweli tulipinga katika vyote, kwa nini serikali ishughulike kununua mtambo ambao unanuka rushwa ya wazi iliyofanywa na watendai wake kwa kuhirikiana na wafanyabiashara wakubwa wasiokuwa waaminifu wengine wakiwa ni wanasiasa? Lakini pia kwa nini serikali ishindwe kujipanga mpaka iwe conered kununua mitambo chakavu?
   
 6. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,596
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Hapana Mkuu, Richmond ni Kampuni feki, haijawahi Kuexist.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Richmond, kwa maoni yaliyowezesha Dowans na kesi yao dhidi ya Richmond, Marekani wanatambua uwepo wa kampuni hiyo.
   
 8. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MMK,Richmond inaonekama kama a briefcase company started for the sole purpose of kuja kufanya biashara ya kunyonya watanzania. Kama Dowans vile.Richmond na Symbion ni usiku na mchana.Kwa nini hatusikii who are the owners of Richmond?What is the history of Richmond? At least bio's za real owners wa Richmond?Does it still exist in Texas?
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Bado hawajanipata....Hivi,STAMICO haiwezi kuwa na mgodi hata mmoja wa dhahabu? Kwanini?
  Mimi naona hawa jamaa bado wanarukaruka tu.
  Kuhusu umeme,tungeacha mambo ya kujifanya mkataba ulikuwa si wa kihalali.Tulikuwa tunapata umeme wa bei rahisi sana,na ulikuwa haukatiki under Dowans.Naomba mtu yoyote aniambie mkataba upi ulikuwa unadeliver umeme constantly kwa bei cheaper than Dowans?
  Sasa hivi hii symbion ina mkataba wa miaka mingapi na serikali?.....Wamesema emergency,but it looks like this is what we gonna have for the rest of our lives....We don't need non-renewable sources of energy,they are killing us!!!
  Angalau kiwira naweza kukubali,ila haya mafuta yanatumaliza tu hayana chochote,na wabunge wetu(tena vijana) need to grow some ballz and speak the revolutionary language.
   
 10. b

  bulunga JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama sikosei hoja ya Zitto ilikuwa ni kuunga mkono hoja ya kubadilishwa sheria ya manunuzi iliyokuwa inakataza serikali kununua mitambo iliyotumika, sheria hii inatakiwa kubadilishwa kwa sabababu ya dharula kwa JANGA la taifa la sasa, kama sikosei kuna mitambo ILIYO TUMIKA iko mbioni kununuliwa na serikali (chini ya DHARULA) hii haitawezekana unless sheria ziruhusu kununuliwa ikiwa imetumika, wasi wasi wangu ni mambo yale yale DHARULA tena inatumika kutatatua tatizo la umeme.
  kama mnakumbuka alikuwa ni Mbunge wa Singida Mchemba, alikuja na hoja hiyo baada ya naibu waziri Malima kujibu swali lilohusiana na utatuzi wa tatizo la umeme, hapo ndipo waziri Mkuu alitilia mkazo kwamba kwa hali hii inayo likabili taifa itabidi mitambo ya dharula ipatikane na akasema kuwa kwa vile mitambo mipya inachukua muda kupatikana itabidi ipatikane hata iliyotumika , kama sikosei haya ndo mh Zitto aliyapigia mstari kuwa alishawahi kusema mitambo hata kama ya zamani itabidi inunuliwe
   
Loading...