Mchango wa wana JF Walioko nje ya nchi unatosha ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchango wa wana JF Walioko nje ya nchi unatosha ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bw.Ukoko, Jul 23, 2009.

 1. B

  Bw.Ukoko Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  naleta kwenu mada hii kwa nia njema kabisa kuhusiana na wenzetu walioko nje ya Tanzania ambao ni member hapa JF.

  Nimekuwa nikisoma post zao na michango kadhaa kuhusiana na masuala mbalimbali kwa maendeo yetu,wao,taifa letu nk lakini nimegundua kuwa jamaa hawa hawatusaidii sana.

  kwanza (kwa maoni yangu) nafikiri jamaa hawa wangetazama hali halisi ya suala lamaendeleo katika nchi walipo ambayo yanaweza kutusaidia sisi binafsi badala ya kutegemea serikali hata mbinu za kuazisha miradi badala ya kujadili tu siasa(wanaogoza kwa post za kisiasa).

  Aidha kwa kuwa wamezaliwa hapa bongo na kwenda huko kwa sababu mbalimbali watupatie mbinu mbadala za sisi kujikwamua na umaskini badala ya kutegemea serikali.

  aidha watanzania hapa watuwekee hapa JF habari zinazotaagzwa na vyombo vya huko waliko kuhusu tanzania kusudi tujadili badala ya wao kujadili yanayotokea hapa bongo.

  sina lengo la kubeza mchango wao lakini naona wao wanaendelea kula bata ugaibuni huku ewnzao wakifa kwa njaa,tupeni michango ya kutukwamua na umaskini kwani masula yanayohitaji uzoefu wa maeneo mbali na Sera za nchi ,elimu,mitaji nk.

  kwa kuwajulisha tu katika mkoa nilopo mimi bei ya kutumia internet kwenye cafe ni sh 1000 kwa nusu saa hivyo................................


  lakini nasikia baadhi yenu hamuwezi kurudi nyumbani bongo kwa kukosa nauli hii ikoje.

  nawatakia maisha mema.
   
 2. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Sasa unataka waseme nini? wamekwisha kimbia shida za bongo kwa nini wazijadili waache wakale maisha ,nyinyi na wenzako muendelee kusota .

  Lakini wengine wamechoka licha ya kuwa ughaibuni,tuwaombee warudi salama kwani nauli ya kutoka walipo ni sawa na bajeti ya Tarafa yako.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mtegemea cha ndugu...
   
 4. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,132
  Likes Received: 23,744
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wewe unaposikia watu walioko nje wanabeba box unaamini kabisa kuwa hata nauli ya kuwarudisha hawana sio, pole sana ndugu.
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  ok kaka tmekusikia lakini michango yetu si ya kisiasa pekee.
   
Loading...