Mchango wa ushuru wa vibanda vya biashara (magenge) Mshangano Songea umetusikitisha

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
90
Hongereni kwa ujenzi wa taifa.
Leo hapa kata ya Mshangano Songea afisa mtendaji ametangaza ushuru wa magenge ya mitaani shilingi elfu moja kwa siku. Yaani kwa mfano wewe hapo nyumbani kwako uweke genge dogo la kuuzia nyanya,mbogamboga, vitunguu nk ili kurahisishia majirani wasifunge safari ndefu kufuata vitu hivyo sokoni. Sasa mtu anajishughulisha kutafuta riziki unakuja na ushuru wa shilingi 1000 kwa siku sawa na 30,000 kwa mwezi. Je hii si sawa jamani kama sio uonevu?!Tunaomba mkurugenzi afuatilie wananchi mbona tutapata tabu sana kwa nini lakini!?
 
Wakurugenzi wameagizwa kubuni mbinu za kukusanya kodi kwa namna yoyote ile, nenda Masasi town uone vituko vya mkurugenzi Gimbana (mtoto wa shemeji yake Pombe) alichokifanya maduka makubwa ya mkuti. Hovyooo!
 
Pole, mkurugenzi afuatilie kwani si mtendaji anafanya kazi kwa niaba ya mkurugenzi?? Hivi ile kodi ya kichwa ilikuwa ijadiliwe na madiwani SONGEA manispaa ilikomea wapi??
 
Kiukweli sio sahihi, lakini ndio tayari agizo kutoka juu linatekelezwa hivyo....

Kama wanakijiji mnaumoja, pazeni sauti zenu.....kuwaamsha hawa wafalme jua. Nje ya hapo, mkubali tu kupata matokeo ya kazi mlioifanya mwaka 2015.....

All in all, napenda kuwapa pole ndugu zangu.
 
Inauma sana ila hongera zao walioichagua CCM
 
Back
Top Bottom