Luhaga Mpina ataka maeneo ya kiuchumi yatungiwe sheria

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
Mheshimiwa Spika, Maeneo mengi muhimu ya kijamii na kiuchumi kutotungiwa Sheria mahsusi na badala yake kutumika matamko ya baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali

(a) Mheshimiwa Spika, Biashara za Machinga, Bodaboda, Mama Ntilie, Wauza mbogamboga kundi hili liko kwenye hekaheka kila leo mara hawa wasionekane mjini, mara wafukuzwe na kuhamishwa, mara hawaruhusiwi kufanya biashara sehemu fulani, mara kupangwa katika maeneo maalum na hivyo biashara zao kutegemea matamko ya viongozi kila uchao hali inayowaletea usumbufu mkubwa na wengi kuishia kufilisika.

(b) Mheshimiwa Spika, Kundi la Vijana na Ajira, hakuna sheria inayomuongoza kijana kupata ajira na masharti ya ajira yanabadilika kila tangazo la ajira linapotoka, mara ajira zitapatikana kwa usaili (Interview), mara kwa kuchaguana tu, mara ukiomba upande huu huruhusiwi kuomba upande mwingine, mara umri huu hautakiwi, mara lazima uwe umepitia JKT, huku wakijua vijana wengi hawapati fursa hiyo na wakati mwingine ajira kutolewa kwa upendeleo hali iliyopelekea Serikali kulalamikiwa kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Spika, Ili kuondoa matamko na utashi binafsi kuwa mbadala wa Sheria, ni muhimu maeneo nyeti yatambuliwe na kutungiwa Sheria mahususi kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa na kuondoa bugudha na usumbufu unaojitokeza mara kwa mara kwenye jamii zetu.
 
Wakiwa hawana madaraka wanajifanya akili zao zinafanya kazi!

Ni huyu huyu Luaga Mpina aliyezunguka na Task Force yake akichoma nyavu za vijana wavuvi na kuwapiga vijana fine na rushwa kubwa kubwa na hatimaye kuwafilisi kabisa!

Hivi huyu Mpina akiwa Waziri wa Uvuvi aliwahi kujiuliza kama watu aliowachomea nyavu walikuwa ni importers wa hizo nyavu na kama siyo je ilikuwa ni sahihi kuwachomea nyavu wavuvi au ilikuwa ni sahihi kuzuia importation ya hizo nyavu ?!

Huyu mtu sasa naamini ni kichaa kichaa kama alivyosema Mwendazake!
 
  • Thanks
Reactions: F4B
Back
Top Bottom