Mchango wa Luhaga Mpina (MB) jimbo la Kisesa (CCM) - kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2022/2023

Jun 25, 2022
3
7
MCHANGO WA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB), MBUNGE WA JIMBO LA KISESA (CCM) WAKATI AKICHANGIA MUSWADA WA SHERIA YA FEDHA WA MWAKA 2022/2023 (THE FINANCE ACT, 2022) BUNGENI DODOMA 28 JUNI 2022

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango amewasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha unaofanyia marekebisho ya Sheria 35 zinazohusu masuala ya fedha, kodi, ushuru na tozo.

2.0 MAREKEBISHO YA SHERIA

2.1. Waziri wa Fedha anapendekeza kufanyia marekebisho Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332 na Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148 Kifungu cha 127 cha Muswada ili kumpa Waziri wa Fedha mamlaka ya kusamehe kodi ya ongezeko la thamani na kodi ya mapato kwa wawekezaji mahiri maalum baada ya kupata ridhaa ya Baraza la Mawaziri. Ambapo awali misamaha hiyo itakuwa imeidhinishwa na kikao cha NISC. Endapo Bunge litaridhia marekebisho haya itasababisha changamoto zifuatazo:-

2.1.1 Kwanini Mheshimiwa Rais aingizwe kwenye mchakato wa utoaji wa misamaha ya kodi? na je itakuwaje endapo Mheshimiwa Rais atashauriwa vibaya na kuridhia utoaji wa misamaha ya kodi isiyo na tija na ambayo imetolewa kwa misingi ya upendeleo, rushwa na ufisadi. Maamuzi haya yanaweza kupelekea Serikali nzima kuingia kwenye kashfa kubwa ya ufisadi na kuchafua taswira ya nchi na kuharibu mahusiano ya kimataifa. Kwanini tunataka Bunge kumuingiza Mh. Rais kwenye kashfa huku tukimkingia kifua Waziri mwenye dhamana ya Fedha anapokiuka sheria za nchi?

2.1.2 Kwa kawaida misamaha yote ya kodi huridhiwa na Bunge, marekebisho haya ya Sheria yanapora Madaraka ya Bunge ya kuamua hatma ya mapato na matumizi ya nchi na kuyakabidhi kwa Serikali (Baraza la Mawaziri) jambo ambalo ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.1.3 Misamaha ya kodi kutolewa kwa baadhi ya wawekezaji walioko katika sekta husika kutaondoa ushindani wa haki na usawa baina yao, hali hii inaweza kupelekea kufungwa kwa viwanda vingine kutokana na kushindwa kushindana na viwanda vilivyopewa msamaha. Maamuzi haya pia ni kuvunja Sheria ya Ushindani Na 8 ya mwaka 2003 lakini pia tufahamu suala la ushindani ni global principle.

2.1.4 Misamaha ya Kodi ya mtu mmoja mmoja au Kampuni inapunguza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kwa mujibu wa ripoti ya CAG ukusanyaji wa mapato umeshuka kwa 0.2% katika mwaka wa fedha 2020/2021, wakati ukusanyaji wa mapato ya kodi ni 11.4% tu ya Pato la Taifa ikilinganishwa na nchi jirani za Kenya na Rwanda zenye wastani wa 16%. Misamaha ya kodi ya aina hii haifai kwa nchi kama ya kwetu ambayo bajeti yake kwa sehemu kubwa inategemea misaada na mikopo.

2.1.5 Misamaha ya kodi ya mtu mmoja au kikundi cha watu kinaweza kupelekea kufanyika upendeleo, rushwa na ufisadi mkubwa na hivyo kudidimiza uchumi wa nchi na kuikosesha Serikali mapato.

2.1.6 Vivutio vya wawekezaji sio misamaha ya kodi pekee isipokuwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu muhimu ya kiuchumi kama umeme wa uhakika na wa gharama nafuu, bandari, barabara, meli, reli, ndege na viwanja vya ndege, maji, upatikanaji wa malighali na masoko, hivyo kama Taifa tupambane tuwezavyo miradi ya kimkakati ikamilike na hivyo ndiyo vivutio vya wawekezaji .

Mheshimiwa Spika, Misamaha ya kodi ya aina hii itapunguza wigo wa ukusanyaji wa kodi, ushindani wa haki na itachochea rushwa na ufisadi na utaiingiza Serikali yetu kwenye kashfa kubwa na kuharibu hata mahusiano ya kimataifa.

Mheshimiwa Spika, Ninashauri vifungu hivi vya marekebisho ya Sheria vifutwe na badala yake kama lengo la marekebisho haya ni kufanikisha miradi mikubwa ya kimkakati ya kitaifa uwekwe utaratibu wa kuwasilishwa maombi maalum na kuridhiwa na Bunge lako tukufu kwa kila mradi kunapokuwepo na uhitaji.

2.2 Kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi Sura namba 438 kwa kuhamisha Mamlaka ya kusamehe riba na adhabu kutoka kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato na kuyapeleka kwa Waziri mwenye dhamana ya Fedha (Serikali imekubali ushauri wa wabunge tulioshauri katika eneo hili na Kamati ya Bajeti kwa kukiondoa kifungu hiki-hongera sana Serikali kwa usikivu wenu, marekebisho ya kifungu hiki cha 114 ya Muswada yalikuwa na athari kubwa katika shughuli za ukusanyaji wa mapato nchini)

2.3 Waziri wa Fedha amependekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura ya 290 ambapo 5% ya mapato ya Halmashauri yatumike kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na masoko ya wamachinga na hivyo kubakiza 5% tu ya mikopo ya kinamama, vijana na wenye ulemavu (Serikali imekubali ushauri wa wabunge tulioshauri katika eneo hili na Kamati ya Bajeti kwa kuviondoa vifungu vya 79, 80 na 81 vya Muswada hongera sana Serikali kwa usikivu wenu hiki kifungu kilikuwa na kinarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuwapatia ajira na mitaji akina mama, vijana na wenye ulemavu)

2.4 Serikali inapendekeza marekebisho ya kifungu cha 17A cha Sheria ya Korosho Sura ya 18 ili kuanisha mgawanyo wa mapato yatokanayo na korosho ambapo 50% itaenda Mfuko Mkuu wa Hazina, na 50% itagawanywa kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo na ruzuku za pembejeo za kilimo. Kabla ya Bunge kuridhia mapendekezo haya ni muhimu kupewa ufafanuzi ufuatao:-

2.4.1 Ni fedha kiasi gani zinakusanywa kutokana na ushuru wa usafirishaji wa korosho nje ya nchi ili Bunge liweze kuelewa linazungumzia ni fedha kiasi gani.

2.4.2 Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo na Wizara ya Kilimo kila mmoja atapata mgawanyo wa kiasi gani kutoka katika mgao wa 50% iliyotengwa.

2.4.3 Serikali iliweka utaratibu wa kisheria kuondoa retention zote kwenye wizara na taasisi za Serikali, Je marekebisho haya yana msingi gani wa kisheria?

2.4.4 Tunayo mazao mengi yanayotozwa ushuru wa usafirishaji nje ya nchi (export levy) kama mazao ya mifugo na uvuvi, kwanini mgawanyo wa mapato unapendekezwa kwa zao moja tu la korosho?

2.4.5 Je mapato hayo yamekasimiwa kwenye Bajeti ya Wizara ya Kilimo? matumizi ya pembejeo yanayopendekezwa ni kwa ajili ya wakulima wa Korosho au wakulima wote?

Mheshimiwa Spika, Marekebisho aliyopendekeza Waziri wa Fedha ni mazuri yenye lengo la kuboresha na kuongeza tija katika kilimo nchini, ili kuepuka kuvunja Sheria za nchi napendekeza fedha hizi 50% zipelekwe katika Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo kwa kazi na shughuli zile zile zilizopangwa.

2.5 Waziri wa Fedha anapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Bima Sura ya 394 kwa kuongeza kifungu kipya cha 133A kinachoweka masharti ya bima ya lazima kwa majengo ya biashara, masoko ya umma, bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, vyombo vya majini na vivuko.

2.5.1 Kumekuwepo na taarifa za kuungua moto baadhi ya masoko na bidhaa za wafanyabiashara kuteketea kwa moto, Je ni hasara kiasi gani imepatikana kutokana na majanga hayo ya moto? na je Serikali imechukua hatua gani ya kuwafidia wananchi hao? na je Tume za kuchunguza matukio hayo ya moto zilizoundwa na Mhe. Waziri Mkuu zilileta majibu gani?

2.5.2 Maamuzi ya kuingiza masoko na minada katika bima ya lazima ni jambo zuri ili kuwa na uhakika wa kuwafidia wananchi wetu wanapopata majanga yakiwemo ya moto katika maeneo yao ya biashara, nashauri jambo hili lifanyike kwa namna ambayo haitaathiri utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa katika Serikali za Mitaa.

2.5.3 Kuamua bidhaa zote kutoka nje ya nchi kukatiwa Bima ya lazima huku Storage and Transport facilities zikiwa zimekatiwa bima ni jambo halieleweki hiyo bima inayokatwa katika bidhaa ni kwa ajili ya nini, lakini pia suala hili linaongeza gharama kwa walaji wa mwisho. Kwanini tufanye maamuzi haya huku tukijua Taifa liko kwenye mfumko mkubwa wa bei na ugumu wa maisha kwa wananchi wetu?

Mheshimiwa Spika, nashauri bidhaa kutoka nje ya nchi ziondolewe kwenye bima ya lazima na ukataji wa bima wa masoko na minada uwekewe utaratibu ambao hautaathiri bajeti zilizopitishwa na Baraza la Madiwani na baadaye kuridhiwa na Bunge.

3.0 MAMBO YA KISERA

3.1 Upitishaji wa Bajeti

Mheshimiwa Spika,
Bunge limekuwa likipitisha bajeti kwa mbunge mmoja mmoja kupiga kura kwa jina na baada ya hapo huchukuliwa Bunge limepitisha Bajeti ya Serikali ambapo Muswada wa Matumizi (Appropriation Bill) husomwa kwa mara ya kwanza ya pili na ya tatu na kupitishwa na Bunge ikiwa ni kuridhia matumizi ya mwaka husika wa fedha.

Mheshimiwa Spika, maamuzi ya kupitisha bajeti ya Serikali yamekuwa yakifanyika kabla ya kupitishwa Muswada wa Sheria ya Fedha (The Finance Bill) na hii inaondoa maana ya Bunge kupitisha bajeti wakati hamjakubaliana eneo la mapato. Bunge linaposhughulikia Finance Bill wakati limepitisha Bajeti halina nguvu ya kufanya marekebisho na marekebisho madogo yanayofanywa hutengeneza upungufu wa bajeti (Deficit Budget).

Mheshimiwa Spika, miaka ya nyuma hali ilikuwa mbaya zaidi ambapo Bunge lilikuwa linaidhinisha bajeti halafu linakwenda kujadili vifungu kwa kila Wizara, bajeti ilijadiliwa hadi Mwezi Agosti wakati utekelezaji wake unaanza Julai 1, pia hatukuwa na Kamati ya Bajeti. Baadaye tulifanya marekebisho chini ya uongozi wa Mwana Mama shupavu Mhe. Anna Semamba Makinda, Spika wa Bunge la 10 ambapo Kamati ya Bajeti ilianzishwa, Mjadala wa Bajeti ulianzia na Wizara na baadaye Bajeti Kuu ya Serikali na kuhitimishwa kabla ya Julai 1.

Mheshimiwa Spika, Historia huwa inajirudia nakuomba leo, Spika wetu makini na msikivu, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ukubali kurekebisha utaratibu wa uridhiaji wa bajeti kwamba Bunge lijadili Bajeti kuu ya Serikali na Muswada wa Sheria ya Fedha kabla ya kuridhia Bajeti kwa kupiga kura. Bunge lipige kura ya kupitisha bajeti ikiwa Muswada wa Sheria ya Fedha umepitishwa na pia utaratibu wa kufanya Finance Bill kuwa jambo la SIRI ukataliwe.

3.2 Upitishaji wa Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004

Mheshimiwa Spika,
Nakubaliana na changamoto za upitishaji wa Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004 ambapo Bunge lako limekuwa halishiriki kikamilifu kupitisha mapendekezo ya Sheria hiyo kila mwaka wa fedha. Sheria hii mabadiliko yake hufanywa na Mawaziri wa Fedha, Uwekezaji na Biashara wa Afrika Mashariki na baadaye huridhiwa na Bunge la Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, nakubaliana kwa asilimia 100 na ushauri wa Kamati ya Bajeti kuwa ni wakati muafaka wa kuweka suala hili ama kikanuni au kwa kisheria ambapo itamlazimu Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo hayo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na baadaye Bunge zima kabla hayajaridhiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti walipaswa kuwasikiliza wabunge katika maeneo ya mabadiliko yaliyofanywa katika sheria hii na kuyajengea hoja ili Serikali iwasilishe taarifa ya marekebisho kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kulinda viwanda vyetu vya ndani na uchumi wa nchi. Badala ya kutupia mpira kwa Serikali kwamba ndiyo ichukue maoni hayo.

3.3 MISAMAHA YA KODI

Mheshimiwa Spika
, Hotuba ya Waziri wa Fedha haijatoa tathmini ya misamaha ya kodi iliyokwishatolewa miaka ya nyuma ili kuendelea kujenga uhalali wa kuendelea kusamehe, kuanzisha au kufuta na kutoza kodi husika. Zipo taarifa kuwa misamaha mingi ya kodi haitoi unafuu wa bei kwa wananchi kama lengo la kutolewa misamaha hiyo, kauli hii inathibitishwa pia maelezo ya Waziri wa Fedha wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Lakini pia inaonyesha hakuna usimamizi thabiti wa misamaha ya kodi inapotolewa. Eneo hili lisiposhughulikiwa kikamilifu haliwezi kuleta tija tarajiwa na badala yake litaendelea kutumika kama uchochoro cha kujipatia rushwa na kufanya ufisadi kwa baadhi ya watumishi wa umma wasio waadilifu, Kuleta ushindani usio sawa na kuikosesha Serikali mapato.

Nawasilisha,

Luhaga Joelson Mpina (Mb)

Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM)

Attachments

  • 3 (1).jpg
    3 (1).jpg
    53.3 KB · Views: 10
Mbunge Makini, mwenye Akili na Mzalendo, anayetumia muda wake kujichimbia Mahali, nakisoma na kupitia na kuja Hoja zinazowaacha Vichwa maji Kumwonea wivu .

Wenye Akili tunamuelewa MPINA !! Wengine watamuelewa Baadae.
 
Tumpe uhuru wa kusamehe kodi mtu ambaye hashitakiwi kikatiba hata akituibia?
 
Haya yote Mwigulu hakuyaona?
 
CCM haiwezi kuipinga CCM

Maoni mazuri ameangalia sera na sheria hajazungumzia maoni yetu wananchi.

Sisi tunataka hotuba ya waziri ya fedha iainishe uwajibikaji pia kwenye ripoti za CAG.
 
Huyu mbunge ni moja kati ya wabunge wachache ninaowakubali kutoka CCM.

Ni wazi kuwa anafanya paperwork ya kutosha na anajua wajibu waje wa bunge kuisimamia na kuishauri serikali.

Much respect kwa Mpina.
 
Back
Top Bottom