SoC01 Mchango wa Jamii katika kuboresha Elimu Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Semu Msongole

Member
Jul 19, 2021
16
421
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu

Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana.

Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni

Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh.

Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi

Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko.

Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule

Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea.

Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
 
Mimi Niko katika swala la usafiri kwa wanafunzi...

Miongoni mwa mambo yanayoshusha taaluma kwa wanafunzi ni changamoto hii ya usafiri...

Huwa nashuhudia jinsi wanafunzi wanavyoteseka barabarani hususani katika jiji la Dar...

Mfano, ikifika jioni, pita maeneo ya Kibamba pale barabara ya Morogoro... Uone jinsi walivyorundika kusubiri usafiri kurudi makwao...

Mimi nashauri:

Serikali inapaswa kutafuta mabasi maalumu kwa ajili ya wanafunzi tuu kwa ajili ya Shule za serikali..

Kama vile wanavyofanya Private Schools kuweka School Buses, Serikali nayo ifanye hivyo hivyo kwa kutokana na maeneo...

Mfano, kuwepo na School Buses kwa ajili ya zone ya Kimara, Mbezi na Kibamba...
Zone ya Gongo La Mboto, Ukonga nk.. Na maeneo mengineyo katika mikoa tofauti na wilaya tofauti hapa nchini...

Serikali ina Pesa nyingi Kiasi kwamba haiwezi kuendesha jambo hili.
Pesa inatawanywa katika mambo yasiyo ya msingi badala ya kuwekeza katika elimu kwa kuwapatia wanafunzi usafiri wa uhakika..

Na wawe wanachangia hiyo hiyo sh. 200/- au hata chini ya hapo..

Nawasilisha.....
 
Mimi Niko katika swala la usafiri kwa wanafunzi...

Miongoni mwa mambo yanayoshusha taaluma kwa wanafunzi ni changamoto hii ya usafiri...

Huwa nashuhudia jinsi wanafunzi wanavyoteseka barabarani hususani katika jiji la Dar...

Mfano, ikifika jioni, pita maeneo ya Kibamba pale barabara ya Morogoro... Uone jinsi walivyorundika kusubiri usafiri kurudi makwao...

Mimi nashauri:

Serikali inapaswa kutafuta mabasi maalumu kwa ajili ya wanafunzi tuu kwa ajili ya Shule za serikali..

Kama vile wanavyofanya Private Schools kuweka School Buses, Serikali nayo ifanye hivyo hivyo kwa kutokana na maeneo...

Mfano, kuwepo na School Buses kwa ajili ya zone ya Kimara, Mbezi na Kibamba...
Zone ya Gongo La Mboto, Ukonga nk.. Na maeneo mengineyo katika mikoa tofauti na wilaya tofauti hapa nchini...

Serikali ina Pesa nyingi Kiasi kwamba haiwezi kuendesha jambo hili.
Pesa inatawanywa katika mambo yasiyo ya msingi badala ya kuwekeza katika elimu kwa kuwapatia wanafunzi usafiri wa uhakika..

Na wawe wanachangia hiyo hiyo sh. 200/- au hata chini ya hapo..

Nawasilisha.....
Asante sana kwa mchango wako umeelezea vizuri sana hili swala na suluhisho lake. 🙏
 
Wazo zuri sana, ushauri wangu ni " ujumbe huu usiishie kuwa maandishi tu, kama ulivyojitosa kufikisha ujumbe huu katika mtandao huu (Theoretically) , jitose hivyo hivyo kufikisha ujumbe huu makanisani kwa kuanza na sehemu unayosali (practically)"
 
Wazo zuri sana, ushauri wangu ni " ujumbe huu usiishie kuwa maandishi tu, kama ulivyojitosa kufikisha ujumbe huu katika mtandao huu (Theoretically) , jitose hivyo hivyo kufikisha ujumbe huu makanisani kwa kuanza na sehemu unayosali (practically)"
Asante sana kwa maoni yako ntajitahidi kuyafanyia kazi. 🙏
 
Najaribu kuvote inanikatalia, sijui nimechelewa ama vp, ila ni bandiko Zuri. King in ningependa pia tufikiriea Je elimu inayo tolewa sasa inayo ubora na sifa za kukabiliana na hatimaye kutatua changamoto zinazo izunguka jamii yetu?
Math alanine tuliwahi kuwa na kikombe cha babu, Mindoro mbinu ilijengwa, mawasiliano yakalazimishwa kupatikana kule alipo babu ila kila mwenye shida ya Marathi alike atibiwe, Gharama kubwa zilitumika, je kikombe cha babu no kilikuwa suluhisho la Marathi ya wa TZ?
Jibu ni hapana.
Sasa basi tunaweza wekeza Mindoro mbinu ya elimu ili watoto wetu waste, swali ni je hiyo elimu wanayo kwenda kusoma ipo?
....
 
Back
Top Bottom