Mchango wa harambee kusafirisha wanavyuo kwenda kupiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchango wa harambee kusafirisha wanavyuo kwenda kupiga kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshiiri, Oct 7, 2010.

 1. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Waheshimiwa wanajamvi, waheshimiwa wagombea uchaguzi, waheshimiwa wazalendo, mabibi na mabwana.

  Napenda kuwakilisha mchango wangu wa mawazo na mali kufuatia Serikali hii ya mafisadi kutaka kupoteza kura za wasomi wetu ifikapo hapo 31 Oktoba 2010; kimbembe cha uchaguzi kitakapofikia tamati.

  Ni makusudi tu. Hii ni kiashirio kuwa hizi ni kura ambazo mmoja wetu anataka kuzipoteza kwa kuwa zitamwangushia haijawahi kutokea. Tanzania ni nchi ya amani na chama nyambafu kitaanguka kistaarabu kabisa na wazi. Wataweza kuiba na kufanya ujanja ujanja lakini jambo hili sasa linabeba utaifa. Liko wazi kama vile mtu aliyepimwa na kubainika ana ngoma kisha kuanza kushambuliwa na magonjwa nyemelezi kama kifafa n.k. Ni ufundi wa kijinga. Kama mfuasi wa CHADEMA huku ughaibuni, nashauri yafuatayo ili tushinde kwa kishindo:

  -1. Tujichangishe fedha ili kupata kukodisha kama mabasi 26 yaani moja kila mkoa kubeba hawa wasomi wetu. Itakuwa gharama isiyozidi milioni 50 ama kwa hakika kwenda na kurudi. Likewise tuchange na niko tayari kutoa basi moja Arusha kwenda Dar mimi mshiiri naahidi.

  -2. Tuitishe tenda na watu wapo wenye vyombo vya usafiri.

  Hii itasadidi kuwakomoa hawa jamaa na kura tutakuwa tumezinunua kutoka kwao kwani walishapanga kuziharibu. Zitakuwa zetu anyhow.

  Ili kuwezesha yote hayo nitawapatia paypal account ili kuweza kutuma fedha za hali na mali au CHADEMA itupatie account number tuweze kuanza kuchangia jana.

  Tumeshashinda ila tunataka kushinda kwa kishindo.

  Naomba kuwakilisha mchango wangu. Naomba kuwakilisha.
   
 2. m

  mapambazuko Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu hii sijui lakini nilivyodokezwa utaratibu huu kwa sheria za uchaguzi hauruhusiwi kwa mgombea au chama iatakuwa kama kumshawishi mtu aje kukupigia kura akishindwa mgombea anaweza kukata rufaa sasa ni nani apewe jukumu la kushika michango hiyo ipo kazi kweli haki ya wasomi inapotea my be waje wenyewe sijui wengine mnasemaje
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,343
  Trophy Points: 280
  I'm sorry to say, it is too late to catch the train. The information regarding to the disfranchise was out two months ago. People discussed here in JF,but no one in students government or opposition candidates reacted promptly. I expected the erudite from high learning institutions could read and analyse every piece of information which could have an impact on their registration and voting process. If this could happen in 80's 0r 90's things would have been different, unfortunate this generation lacks some intellectual capacity. Now everybody is up with arms to solve the problem at eleventh hour. If the suggestion propounded is to be realised,then there should be a well organised and sophscated logist mechanism, which seems to be impossible because the window of opportunity is closed. This should serve as a lesson in future!
   
 4. S

  Sheka Senior Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nawashauri wanavyuo wajikamue ili kuonyesha uzalendo mbona wenzetu wa Zanzibar wanaweza kuhakikisha kuwa wanarudi kwao siku ya uchaguzi wanapiga kura na kurudi kwenye hekaheheka za kutafuta riziki cha msingi kuserve hela kidogo Amkeni Muonyeshe uzalendo saa ukumbozi ni sasa wala sio kesho.
   
 5. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,865
  Likes Received: 2,806
  Trophy Points: 280
  Mabasi yenu yatakamatwa yote na hamtafika kwenye vituo vya kupigia kura!!!!!!!!! Upo hapo? Wanachuo kama kweli wanahitaji mabadiliko ni bora wakajisafirisha wenyewe tu kwenda kwenye vituo vyao " Unless they are not serious with changes in this country" Mbona wengine tumepanga kutumia gharama isyopungu laki 1 kwenda kupiga kura??
   
 6. C

  Chamkoroma Senior Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi Mshihiri ametoa point ambayo ni yamaana sana japo nikama mtego kwa wagombea wa uchagu, lkn bado naamini kuwa kama hawa jamaa waliotoa kilio cha kupiga kura wakanyimwa wanao muda na nafasi ya kupokea mchango toka kwa wanachama wengine kupata nauli ya kurudi vyuoni, chamsigi hapa nikuwa mto kilio aende one of TV centres awaambie popote walipo wanavyuo ambao wako tayari kuja kupiga kura wajiandikishe ijulikane wangapi na hapo hao wanavyuo waje kama kwa utashi wao na si rushwa ili CCM wakitafuta njia wasiione, na vijana wa kazi majembe ya baadae wanavyuo waje kupiga kura naamini we can do as much as posible kuwchangia nauri kama wenzetu wanachama na sikuwa tunanunua kura.
  nawakilisha.
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni nzuri lakini ukishataja chama ful;ani kinahusika basi sheria ya gharama za uchaguzi inakubana sana na ukizingatia tuko upinzani basi Tendwa na Makame hawatachelewa kutujia labda chama cha mafisadi kingefanya hivyo!
   
 8. m

  masawila Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 25, 2007
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mshiiri ni moyo mzuri ulionao lakini, I`m sorry hii tabia ya kuomba omba kwa kila jambo ndo imetufikisha hapa tulipo. Kama mtu unataka kupig kura, unajali kura yako, lazima uone umuhimu wa kupiga kura na inabidi ufanye kila uwezalo ili uweze kupiga kura Oct 31. Kwa hiyo basi, kama upo tayari kutoa msaada wa kuwasafirisha hao wasomi, basi wasiliana na Administrator ili mpange jinsi ya kukutana na hao wanafunzi ili kuunganishwa noa kwa ajili ya kutoa huo msaada. Lakini tabia ya kuomba omba ndio inatufanya tunaendelea kuwa na taifa tegemezi kwa kila jambo. NI hayo tu.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  watanzania tuna maradhi ya kupenda 'ushindi' bila ya kutaka kuingia gharama.

  wanafunzi watu wazima wa chuo kikuu wamepata loophole ya kulalama kuwa 'wamezuiwa' kupiga kura wakati wangejipanga uzuri wangelikuwa na akiba mahsusi kwa ajili ya kupiga kura.

  wanafunzi wa shule za sekondari za bweni jee nani awalipie?

  Kila mmoja ajifunze kubeba mzigo wake mwenyewe hasa tunapotaka kupigania mageuzi yenye manufaa kwa wote
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mshairi ameleta wazo kwa alivyoona yeye. Tukichangia vizuri twaweza pata suluhisho la tatizo hili!!

  Hima wana JF, tuamue, hawa wanafunzi wanapaswa kuelelwa maana na uzito wa kura yao! La sivyo wakiendelea kuchukulia "poa tu" italeta matizo kwao na vizazi vyao!! By default tunategemea wanafunzi na elimu ya juu kufili critically, we can raise something for assistance kwa wale wenye hitaji la kweli!!

  "If we want changes, then we have to be ready with all associated costs"
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mchango wangu ni wazo lifuatalo,

  Bakini huko mlipo, jiungeni na kampeni za wagombea ama chama mnachokiamini ama kukipenda, pigeni kampeni ya nguvu kuhakikisha watu wanaenda kupiga kura tena hasa vijana wenzenu waliokosa bahati ama kunyimwa nafasi ya kupata elimu kama mliyopata ninyi.....Baade muwasaidie wagombea wenu wa udiwani na ubunge kusimamia/kulinda kura....hukohuko mlipo....

  Lakini pia huu ni wakati wa kujifunza zaidi hali halisi ya wapiga kura wenu wa baadae ili mkitoka huko vyuoni muache kujiona kuwa ninyi ndio wajuvi wa yote wakati wazee walishasema kuwa kupokea digrii ni uthibitisho wa u-mbumbu wako....

  Mnaweza pia kuanzisha mtandao wenu ambao utawaweka pamoja na kupeana taarifa ya mambo yanavyoenda huko mliko....

  Jinsi gani mtakavyo handle ushabiki wa vyama hilo ni zoezi lenu kulitatua.............

  Take it as a blessing in disguise...I always believe in this and most of the time it works...
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wazo zuri sana, lakini this guys Kiravu and the company wanaweza pia wasipeleke hivyo vifaa vya kupigia kura huko kwa kuwa vyuo havijafunguliwa hili ni jambo la kulifikiria pia.
   
 13. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Kuwabeba kwenye malori, kulipa mafuta ya bajaji, nk. ili waje kusikiliza wanachodanganywa je si tabu ila ni usafirishaji wa hisani. Usiwe na akili finyu. Kura ni siri. Panda basi kapige kura kwa umtakaye. Hapo kuna shida? Akishindwa kwa kutokupata kura anashitaki kwa nani. Hii nchi ina wenyewe na wenyewe ni wananchi.

  Tusiwe na mawazo finyu.
   
 14. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Jamni mimi sidhani kuwa hawa wanafunzi ni masikini saaaana kiasi kwamba hata hawawezi kukopesheka. Mapinduzi ni sharti yawe na gharama na mwana mapinduzi ni lazima agharamie. Nimeambiwa kuwa Vyuo vitafunguliwa tarehe 8 November, wiki moja tu baada ya kura. Najua wengi wa wanafunzi hasa wa mikoani huwa wanalala off campus. Jamni kopa, kuwahi chuoni kwa wiki moja tu haitakuwa gharama sana kwako, nenda kapige kura. Wanafunzi wanaosoma hapa Dar, sidhani kama kuna mmoja ambaye hana hata ndugu ama rafiki wa kumwomba kukaa ili aje kupiga kura. Kwa mfano mimi nimewaita wadogo zangu kumi, nimewaambia watakaa kwangu kwa wiki hiyo moja wakisubiri vyuo kufunguliwa ilimradi tu wapige kura. Lakini nilitaka waniahidi kuwa watampa kura Dr Slaa na wabunge wa CHADEMA. Tafuteni kila njia, hii ya kukodi magari itakuwa na shida kwani itahujumiwa tu, hawa jamaa wako kila kona.
   
 15. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mshiiri,
  ni wazo zuri, inabidi tuhakikishe wadogo zetu wanapewa haki yao ya kikatiba kuweza kupiga kura kumchagua kiongozi wanayeona atawafaa.
  Mimi nitakodi basi la abiria 57 kuwawezesha kwenda Morogoro au Dar es Salaam kupiga kura.
  Bila kuangalia umbali, ningependelea safari ianzie Dodoma au Arusha.
   
Loading...