Mchango wa Halima Mdee kuijenga Chadema ni sawa na Wajumbe wote waliobaki Chadema ukimtoa Mbowe

Ukweli lazima usemwe.
Chadema ilipofikia inaelekea kufa kabisa katika siasa za vyama vingi Tanzania.

Chadema haikujengwa kwa sera bali ilijengwa na umahiri , weledi na uwezo wa mtu mmoja mmoja.

Alipo ondoka Zitto ndani ya Chadema, chama kiliyumba na hakikuwahi kukaa sawa mpaka sasa. Dr Slaah alijitahidi saana kuziba pengo la bwana Zitto.

Alipo ondoka Dr Slaah, Chadema sio kwamba kiliyumba tu bali kilipoteza mwelekeo, kimekuwa Chama cha matukio tu, kila wanachojaribu kufanya wanadondokea pua, movement zao zote zinafeli.

Sasa wameamua kumuondoa Halima Mdee na wenzake.
Hakuna asiyetambua uwezo binafsi wa Halima Mdee katika uwanja wa siasa za Tanzania. Mdee amekijenga chama, amefanya akina mama wengi wajiunge na siasa za upinzani.

Hakuna mwanamke yeyote hapa Tanzania ambaye anaweza lingana na Mdee katika siasa za upinzani. Mchango wa Mdee kwa Chadema ukimtoa Mbowe ni sawa na Wanachama wote waliobaki Chadema.

Katika vita vyote ulivyowahi kupigana Mh. Mbowe hii ya akina Halima Mdee na wenzake umeshindwa.

Ni chuki tu zimewaondoa Chadema akina Mdee na wenzake .
Hao akina Hilda si level ya Mdee.

Chadema kinaenda kuzikwa moja kwa moja kwenye siasa za Tanzania
#MUNGU IBARIKI TANZANIA #MUNGU MBARIKI MH. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA #SSH
SAWA! vipi na hawa tuambie na mchango wa SLAA na mdogo wake ZITTO je chama kiliyumba?
THIS IS CHADEMA mtaumia sana
 
Back
Top Bottom