Mchango wa Dkt. John Pombe Magufuli nchini Tanzania na Bara la Afrika kwa Ujumla

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MCHANGO WA DR. JOHN POMBE MAGUFULI NCHINI TANZANIA NA BARA LA AFRIKA KWA UJUMLA.

Dr. John Pombe Magufuli aliyehudumu kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Tano aliheshimika nchini Tanzania, Barani Afrika na Duniani kwa Ujumla kutokana na namna alivyosimama kidete kuhakikisha maslahi ya Wananchi wa Tanzania na Nchi za Kiafrika kwa ujumla yanapewa kipaumbele cha kwanza.

Dr. Magufuli ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Bara la Afrika kwa namna tofauti tofauti katika kipindi chake cha Uongozi.

MCHANGO WA DR. MAGUFULI KATIKA UKUAJI WA KISWAHILI BARANI AFRIKA.
Dr. John Pombe Magufuli alihamasisha matumizi ya Kiswahili kama lugha kuu ya mawasiliano katika Nchi za Bara la Afrika. Nchi nyingi za Bara la Afrika zilihamasika kuanza kutumia kiswahili katika shughuri zake za kila siku na pia kuanza kufundishwa kwa lugha ya kiswahili katika mataifa malimbali Barani Afrika. Wakati fulani Dr. Magufuli alisafiri katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika ikiwa ni pamoja Afrika Kusini ambako aliwapelekea zawadi ya Vitabu vya Kiswahili wananchi wa Nchi hizo ikiwa ni kuonyesha namna alivyosimamia kampeni yake kuhusu maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Baada ya jitihada hizo Nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini zilianza kufundisha Kiswahili na pia Kiswahili kilitambulishwa kama Lugha Rasmi katika mikutano yote ya Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pia Dr. Magufuli alihamasisha kutafsiriwa kwa sheria zote za Tanzania pamoja na mikataba mbalimbali kama sehemu ya kukifanya kiswahili kuwa lugha rasmi katika Shughuri zote za kiserikali nchini Tanzania. Dr. John Pombe Magufuli alitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano yake takkribani yote hali iliyopelekea wakosoaji wake kusema kuwa hajui kuongea lugha ya Kiingeleza. Muda wote Dr Magufuli alijivunia kuongea Kiswahili kwa vile aliamini matumizi ya lugha ya Kigeni ni sehemu ya Ukoloni wa Kifikra.

MCHANGO WA DR MAGUFULI KATIKA UKOMBOZI WA KIFIKRA.
Muda mwingi Dr. Magufuli alisisitiza kuwa Afrika ni tajiri sana. Dr Magufuli aliwahamasisha wa Afrika na Watanzania kutembea Kifua mbele kwa kujivunia uafrika wao. Dr. Magufuli hakuwahi kuamini kuwa suluhisho la matatizo ya Afrika litapatikana kutoka Nje ya Bara la Afrika. Hivyo alisisitiza Nchi za Afrika kutumia raslimali walizo nazo kwa manufaa ya Wananchi wao na kutokujihisi wanyonge mbele ya wawekezaji wa kigeni ama mataifa ya Kigeni. Dr. Magufuli alikuwa tayari kuhatarisha uhusiano na muwekezaji yoyote yule ama Taifa lolote lile ambalo lingetaka kuonyesha kutaka kufanya maamuzi yenye kunyonya ama kudharau Watanzania na wa Afrika kwa ujumla. Lakini pia Dr Magufuli alipandikiza fikra ya kufanya kazi kwa bidii kupitia kauli mbiu yake "HAPA KAZI TU, "ASIYEFANYA KAZI ASILE" na nyinginezo kama hizo. Kauli mbiu hizi ziliwachochea wananchi hususani Vijana kufanya kazi kwa bidii.

MCHANGO WA DR MAGUFULI KATIKA SAYANSI NA UTAFITI.
Dr. John Pombe Magufuli ambaye kitaaluma ni Mwanasayansi alitoa changamoto kubwa kwa wataalamu wa Bara la Afrika kufanya tafiti badala ya kusubiri kuletewa madawa kutoka katika mataifa ya Kigeni. Wakati wa Janga la CORONA Dr. John Pombe Magufuli aliamua kutofautiana na madakati wengi wa Bara la Afrika pamoja na wale wa Shirika la Afya Duniani kwani aliamua kupima Ubora wa Vifaa vya kupima ugonjwa wa CORONA ambapo alibaini kuwa Vifaa vile havikuwa madhubuti hata kidogo kwani vilionyesha kuwa mbuzi, papai, na sampuli iliyochukuliwa kwenye ndege aina Kanga vina maambukizi ya Ugonjwa wa CORONA. Ugunduzi huu uliwaamsha usingizini wanasayansi kutoka mataifa mbalimbali ambao waliamua kuzuia kwa muda matumizi ya Vifaa hivyo. Lakini pia Dr. Magufuli alikataa matumizi ya Barakoa zilizozalishwa kutoka katika mataifa ya Kigeni kwani zinaweza kutumika kueneza maambukizi kwa kiasi kikubwa. Lakini pia Dr. Magufuli alihamasisha matumizi ya Tiba mbadala badala ya kutumia Chanjo ambayo ilikuwa bado kwenye majaribia na iliyokuwa ikionyesha madhara kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji.

MCHANGO WA DR. MAGUFULI KATIKA KUPIGANIA UHURU WA KIUCHUMI.
Dr. John Pombe Magufuli aliamini katika ushirikiano na uwekezaji usio na Chembe ya Uonyonyaji. Muda wote alikuwa mkali kwa makampuni ya uwekezaji yaliyokuwa yakikwepa Kodi na kufanya Shughuri za uhujumu uchumi. Kutokana na msimamo wake huu Viongozi wengi wa Bara la Afrika walianza kuiga nyendo zake na hapa ndipo msamiati "MAGUFULIFICATION OF AFRICA" ulipotengenezwa ukimaanisha Kuchukua maamuzi ama kutenda mambo kama Magufuli kwa manufaa ya Bara la Afrika. Itakumbukwa vema namna msimamo wa Dr. Magufuli kuhusu kampuni ya BARRICK ulivyosaidia kuanzisha mfumo mpya wa uwekezaji ambao ulilenga kuwanufaisha Watanzania. Mfumo huu ndio ambao sasa unatumiwa na Kampuni ya Barrick kote barani Afrika katika kutekeleza shughuri za Uchumbaji wa madini.

MCHANGO WA DR. JOHN POMBE MAGUFULI KISIASA NA KIJAMII.
Dr John Pombe Magufuli aliamini katika ushirikiano na mataifa ya Afrika kuwa ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo barani Afrika. Hivyo Dr. Magufuli alihubiri katika siasa zenye Kuchochea maendeleo kwa wananchi. Dr. Magufuli aliguswa na matatizo ya Wananchi wa Bara la Afrika kwa kiasi kikubwa sana. Muda wote yalipotokea majanga katika Nchi za Afrika alikuwa msatari wa mbele kutoa msaada katika Nchi hizo. Mfano Dr. Magufuli alitoa msaada wa madawa, Blanketi na wataalamu pale Nchi ya Msumbuji ilipopigwa na Kimbunga. Lakini pia Dr. Magufuli ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa usalama , amani na mshikamano miongoni mwa Nchi za Afrika unakuwa mkubwa.

Kwa kuhitimisha, Dr. Magufuli alikuwa mwana wa Afrika, Kiongozi aliyeielewa vema na Kuiishi Falsafa ya Umajumui wa Afrika. Kiongozi huyu aliamini katika kuliunganisha Bara la Afrika na miundombinu bora ingekuwa Suluhisho la matatizo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika. Katika kufanya hivyo alijenga miradi ya Kimkakati iliyolenga kunufaisha Bara zima la Afrika kama Bomba la Mafuta kutoka Tanzania mpaka Hoima Uganda, Ujenzi wa Reli ya Umeme ambao ungeunganisha Nchi za Congo, Burundi, Rwanda nk, lakini pia Ujenzi wa Bwawa la Umeme ambalo lingezalisha umeme ambao ungetosheleza kuuzwa katika Nchi Jirani pia.

Josias Charles
MAGUFULIST
 
He was pragmatic na alitaka vyote vitokee Mara moja...

Tunamshukuru kwa.misingi aliotuachia...

Sasa watz wamekomaa na wamejifunza kwake Kama walivyojifunza kwa Marais waliopita...


Kikubwa kwa Mara ya kwanza watz wamejifunza kwamba kuwekeza Ni dili.....

Hope chini ya mh SSH bado kutakuwa na maboresho...

Tumuombee Rais wetu mh mama SSH...

Everything will be ok
 
Magufuli kafa ili moja lakini kwanini tunapenda kuishi kwa kusifu tu kila siku? Yote yaliyofanye katika ripoti ya CAG hayawezi kukupa mwaga wa viongozi tuliyokuwa nao? Magufuli katika serikali aliweka watu wa ovyo kabisa ili umuone wewe kuwa ni shujaa, katika serikali ya Kikwete tulimjua Magufuli kama waziri wa ujenzi lakini katika kipindi chake watu walikuwa hawamjui waziri wa ujenzi!

Yani kila siku ni kusifu tu ,hunashindwa kusema vitu alivyokosewa ili watu warekebishe, haya ni sio malumbano ni kutetea Tanzania maana kila wakati ipo lakini watu wanapita tu.

Yani waziri mkuu anasema wanataka bajeti ya maendeleo billion 23 ,wakati bajeti ya ofisi wanachikuwa billion 93!!!! Yote haya husemi umebaki kusifia tu!!! hata ufanye mabaya yake watu kuyatoka yatachukuwa muda. Tanzania ipo pigania nchi yako tu ndugu
 
Mwendazake ameacha majeraha makubwa kwenye Utawala bora, Utawala wa Sheria, Katiba na uhuru wa kujieleza.

Miaka 6 ya utawala wake ilikua ya Machozi, Jasho na Damu kwa Watanzania. Haya ni baadhi ya matukio niliyoyakumbuka kwa haraka, baadhi yalitokea nikiwa huko nyumbani na mengine yametokea nikiwa nimeshaondoka.

1. Alizika uhuru wa vyombo vya habari na kutia saini sheria kandamizi kwa vyombo vya habari. Vyomno vyote vililazimishwa kumuandika kwa kumsifu na kumpamba, kilichothubutu kumkosoa kilifungiwa.

2. Alitumia nguvu nyingi kupambana na upinzani na kutesa wanasiasa wa upinzani kwa kuwafungulia kesi za uongo mpaka leo bado wengi wapo jela kwa kesi za kisiasa za kubambikiziwa.

3. Aligawanya nchi kwa misingi ya ukabila, ukanda, uchama na udini na ubaguzi wa kijinsia. Serikali yake ilijaa watu wa kanda ya ziwa na 75% ya serikali yake ilijaa wakristo.

4. Alikua na ubaguzi wa kijinsia na aliendekeza mfumo dume. Wanawake walikua 17% tu ya mawaziri katika serikali yake.

5. Alihakikisha wakuu wa vyombo vya ulinzi wanatoka kanda ya ziwa ili kumlinda likitokea lolote, CDF - Mara, IGP - Mara na CGP - Geita na CGF - Mwanza. Madikteta wote hufanya hivi maana wanajua watu wa kwao hawawezi kuwageuka.

6. Hakupandisha mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa miaka yote 6 ya utawala wake.

7. Hakutangaza ajira mpya katika kipindi chote cha utawala wake. Waalimu waliomaliza vyuo mwaka 2015 hadi leo wapo mtaaji jobless.

8. Aliua sekta binafsi kwa kutoza kodi kubwa, na kuharibu mazingira ya biashara. Hoteli nyingi za kitalii zimekufa kama vile Ngurdoto, Impala, Naura Spring na nyingine zimegeuka hostel za wanafunzi kama Landmark ya Ubungo.

9. Alipunguza mzunguko wa pesa mtaani na kuhakikisha matajiri wanaishi kama mashetani.

10. Katika utawala wake waliibuka watu wasiojulikana ambao waliteka, kujeruhi na kuua watu wasio na hatia. Watu hao walimpiga risasi Tundu Lissu mchana kweupe na mpaka leo hawajakamatwa.

11. Aliwapa nguvu baadhi ya viongozi kama vile Makonda na Sabaya kutesa na kuumiza wananchi kadri walivyojisikia. Makonda alishambulia kituo cha CMG kwa mitutu ya bunduki lakini hakuchukuliwa hatua yoyote. DC Sabaya majuzi kampiga diwani wa Sombetini nusura kifo.

12. Alifuta fao la kujitoa na kusababisha watumishi wengi wenye mikataba ya muda mfupi kuishi maisha magumu baada ya ajira zao kukoma.

13. Katika serikali yake Wapinzani walionekana maadui na sio watu wenye mawazo mbadala. Waliteswa na kufunguliwa kesi za uchochezi. Wengine walipotezwa na hata kuuawa. Alitamani upinzani ufe.

15. Katika utawala wake maiti 17 ziliokotwa ufukwe wa Coco na nyingine 6 ziliokotwa mto Ruvu kwa pamoja zikiwa zimefungwa kwenye sandarusi, na baadhi zikivuja damu.

16. Aliharibu mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengi ukimwenguni. Serikali yake ilichoma vifaranga vya kuku kutoka Kenya na kutaifisha ng'ombe waliovuka mpaka kuja Tanzania.

17. Alisababisha wanasiasa wa Tanzania wakimbie nchi na kuishi uhamisho kama wakimbizi wa kisiasa wakiwemo Ansbert Ngurumo, Tundu Lissu na Godbless Lema.

18. Alitumia mabavu kulazimisha ushindi kwenye uchaguzi wa 2020 na kuhakikisha CCM inashinda majimbo yote. Alipora ushindi wa upinzani kwenye majimbo mengi kwa mtutu wa bunduki.

19. Alitumia sheria ya uhujumu uchumi kutesa wapinzani wake kisiasa na wafanyabiashara aliokua na kisasi kwa mfano Rugemala na Lema wa Elerai Construction.

20. Alipenda kuabudiwa, kutukuzwa na kuogopwa. Wote waliomnyenyekea aliwapa vyeo.

21. Aliamini mawazo yake ndio sahihi na hakutaka kushauriwa kwenye jambo lolote. Aliwahi kusema yeye hapangiwi cha kufanya.

22. Alipenda kuonekana mcha Mungu japo kiuhalisia ni dikteta katili aliyetisha. Alimpoteza Ben Saanane baada ya kuhoji kuhusu PHD yake.

23. Alitangaza kuwa Tanzania haina corona na akataka watu wasivae barakoa wala wasikubali chanjo kutoka nje ya nchi.

24. Alipeleka miradi mingi ya maendeleo kijijini kwake Chato kama uwanja wa ndege, hospitali ya rufaa, benkiz barabara za lami na mbuga ya wanyama ambayo haikua na wanyama ikabidi kuhamisha kutoka mbuza zingine.

25. Aliingilia mihimili yote ya dola ikiwemo mahakama na bunge. Aliwazawadia vyeo vya ujaji mahakimu waliowafunga wapinzani jela.

26. Aliigeuza Tanzania kama mali yake binafsi na katika kila mradi alipenda atajwe yeye. Aliamini akiondoka hakuna atakayeweza kuendeleza yale aliyofanya. Bunge liliwahi kupendekeza kumuongezea muda wa kutawala atakapomaliza mihula yake miwili, kumbe Mungu ana mipango yake hata hiyo miwili hamalizi.
 
Hana mchango wowote zaidi sana aliiharibu nchi, na laiti Mwenyezi Mungu angemuacha miaka10 mbele tungeshuhudia mambo ya ajabu sana kuwahi kutokea duniani!
Ni kweli kabisa JPM alichukua behewa liitwalo. TANZANIA uelekeo ni ZIMBABWE wasukuma gang wanajitahidi kumnadi ila wapi JPM alikuwa na roho yenye kutu ka ruin maisha ya watu wengi mno hususani WAPINZANI ilifika pointi upinzani nchini ulionekana kama ugaidi ama uhaini huku kwenye katiba unatamburika.

JPM ni rais pekee aliekuwa anapelekea nchi yetu kutengwa na nchi jirani na mataifa mbalimbali kwa sababu ya kiburi binafsi na ubabe mavi huku akitumia nguvu nyingi kutuaminisha kuwa bifu lake liwe bifu la taifa.

Pia jamaa alikuwa muongo wa kiwango cha lami alituaminisha eti tupo kwenye vita vya kiuchumi na MABEBERU a.k.a MAREKANI uongo mwingine ni.ule wa kusema eti TANZANIA CORONA haipo utafikili TANZANIA ipo sayari ya PLUTO.

Kwangu mimi ni rais mbaya ambae hajawahi kutokea hapa nchini.

R.I.P JPM lakini ukweli ndo huo uliopo moyoni mwangu.
 
Ni kweli kabisa JPM alichukua behewa liitwalo.TANZANIA uelekeo ni ZIMBABWE wasukuma gang wanajitahidi kumnadi ila wapi JPM alikuwa na roho yenye kutu ka ruin maisha ya watu wengi mno hususani WAPINZANI ilifika pointi upinzani nchini ulionekana kama ugaidi ama uhaini huku kwenye katiba unatamburika.
JPM ni rais pekee aliekuwa anapelekea nchi yetu kutengwa na nchi jirani na mataifa mbalimbali kwa sababu ya kiburi binafsi na ubabe mavi huku akitumia nguvu nyingi kutuaminisha kuwa bifu lake liwe bifu la taifa.
Pia jamaa alikuwa muongo wa kiwango cha lami alituaminisha eti tupo kwenye vita vya kiuchumi na MABEBERU a.k.a MAREKANI uongo mwingine ni.ule wa kusema eti TANZANIA CORONA haipo utafikili TANZANIA ipo sayari ya PLUTO.
Kwangu mimi ni rais mbaya ambae hajawahi kutokea hapa nchini.
R.I.P JPM lakini ukweli ndo huo uliopo moyoni mwangu.
Kiufupi alikuwa ni TAKATAKA ndiyo maana Mungu kamuondolea mbali
 
Back
Top Bottom