Mchango wa Dangote, Dewji, Bakhresa kuhusu tatizo la chakula nchini

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Ndugu zangu,

Hapa Tanzania wapo watu wengi wa Private Sectors na matajiri binafsi ambao,kwa umoja wao na kwa upendo wao wa dhati,wanaweza kusaidia sekta ya kilimo hasa cha umwagiliaji.

Kilimo cha umwagiliaji,cha kisasa kinahitaji nguvu ya pamoja.Kuna haja ya kuwahusisha watu binafsi hasa wawekezaji ili watusaidie kwenye swala hili.

Tulishakuwa na chakula cha kutosha,itatusaidia sana Mh Rais.

Asante.
 
Mawazo mazuri,lakini kama mnachagua viingozi wenye kufoji vyeti,wanaotoa matamko wasishaurika,wenyekujifanya wajuaji unafikiri watawawazia mema?
 
Miradi ya umwagiliaji inaweza kuanzishwa na wananchi wenyewe kienyeji na baadaye iboreshwe na serikali iwe ya kisasa.
Maendeleo huanza kidogo kidogo kuanzia kwa wananchi kama miradi midogo badala kuwa na fikra tegemezi au za kitumwa kwa 100%.
Mawazo haya mabaya ndiyo hufanya viongozi wa serikali kutumia asilimia kubwa ya kodi kwa matumizi ya kawaida na kutegemea wafadhili kwa miradi ya maendeleo.
 
Elimu:
Kuweka mifumo wa umwagiliaji sio sehemu ya miradi ya maendeleo? Jibu: ni sehemu ya miradi ya maendeleo. Pia usalama wa chakula ni agenda ya Taifa lolote lile ili liweze kuwa huru. Kumbuka; ADUI YAKO MWOMBEE NJAA. Njaa huuza uhuru wa Nchi.

Na ujue kuanza kidogokidogo kama mtu binafsi ndio chanzo cha bomoabomoa maana hufanyika kiholela. Bora kupanga kuanzia mwanzo. Nchi inatakiwa kuwa na ramani kuonyesha miundo mbinu yote ili kuepuka leo lami inawekwa, kesho unabomoa kupitisha bomba la gesi, keshokutwa unabomoa kupitisha mifumo ya umwagiliaji.

Pia ujue vyanzo vya maji sio binafsi. Ni vya umma. Kwa hiyo kuyatumia bila idhini ya serikali ni ubatili.
 
Watu wanalima wanakosa masoko, serikali inazuia wasiuze nje ikinunua inawakopa, pembejeo zinachelewa halafu ni feki. Watanzania wanajitahidi sana ila Serikali haina ushirikiano wa dhati, kama wawekezaji wa kigeni wanavyo thaminiwa.
 
Miradi ya umwagiliaji inaweza kuanzishwa na wananchi wenyewe kienyeji na baadaye iboreshwe na serikali iwe ya kisasa.
Maendeleo huanza kidogo kidogo kuanzia kwa wananchi kama miradi midogo badala kuwa na fikra tegemezi au za kitumwa kwa 100%.
Mawazo haya mabaya ndiyo hufanya viongozi wa serikali kutumia asilimia kubwa ya kodi kwa matumizi ya kawaida na kutegemea wafadhili kwa miradi ya maendeleo.

lebabu;
Aliyewahi kutoa mawazo mufilisi naona unaongoza. Mbona mnamuonea sana mlala hoi?? Maji yako shimoni, unategemea ayatoe kwa kata yanyweshee eka??
Swala lililopo mezani sasa hivi ni njaa. Hakuna aliyeileta. Ni hali ya hewa. Sasa hao unao watetea wamefanya juhudi gani za makusudi kuwawezesha hao wakulima wadogo??
Mfano;
Kuondoa kodi kwa vifaa vya umwagiliaji na kilimo?? Luwatafutia mbegu nzuri za mda mfupi?? Kweli, serekali haina shamba ila watu wake ndo wenye mashamba. Wakopeshwe pembejeo kwa mikataba mizuri wazalishe waiuzie serekali ikate huko hizo pembejeo.
Acha kuwatetea wanaojifikiria wenyewe tu. Hatuna fikra tegemezi ila tunafikirishwa tuu. Mama yangu hajui hata duka la pembejeo hupanda darini akafukuzana na panya akatoa huko mbegu. Unategemea mbegu hiyo imuwezeshe??
 
Ndugu zangu,

Hapa Tanzania wapo watu wengi wa Private Sectors na matajiri binafsi ambao,kwa umoja wao na kwa upendo wao wa dhati,wanaweza kusaidia sekta ya kilimo hasa cha umwagiliaji.

Kilimo cha umwagiliaji,cha kisasa kinahitaji nguvu ya pamoja.Kuna haja ya kuwahusisha watu binafsi hasa wawekezaji ili watusaidie kwenye swala hili.

Tulishakuwa na chakula cha kutosha,itatusaidia sana Mh Rais.

Asante.
Fanya kazi kwa bidii na maarifa wewe ƴunawaza misaada tu acha uzembe utaolewa mkuu
kwanza ungehoji mchango wa chama tawala aka chama tajiri afrika ni upi?
 
lebabu;
Aliyewahi kutoa mawazo mufilisi naona unaongoza. Mbona mnamuonea sana mlala hoi?? Maji yako shimoni, unategemea ayatoe kwa kata yanyweshee eka??
Swala lililopo mezani sasa hivi ni njaa. Hakuna aliyeileta. Ni hali ya hewa. Sasa hao unao watetea wamefanya juhudi gani za makusudi kuwawezesha hao wakulima wadogo??
Mfano;
Kuondoa kodi kwa vifaa vya umwagiliaji na kilimo?? Luwatafutia mbegu nzuri za mda mfupi?? Kweli, serekali haina shamba ila watu wake ndo wenye mashamba. Wakopeshwe pembejeo kwa mikataba mizuri wazalishe waiuzie serekali ikate huko hizo pembejeo.
Acha kuwatetea wanaojifikiria wenyewe tu. Hatuna fikra tegemezi ila tunafikirishwa tuu. Mama yangu hajui hata duka la pembejeo hupanda darini akafukuzana na panya akatoa huko mbegu. Unategemea mbegu hiyo imuwezeshe??

Mangatara,

Serikali za nchi masikini kama za kiafrika, mara nyingi viongozi wao hulenga kuvuna kutoka kwa wananchi na siyo kupanda.
Fikra za viongozi walio wengi wa serikali masikini ni kukusanya kodi kwa kumnyonya mwananchi bila kujua anapata nini huku zikitegemea misaada kwa miradi ya maendeleo. Viongozi hawa wametokana na wananchi hao hao wanaotegemea wafadhili kwa kila wazo la kujiendeleza kiuchumi.
Mawazo chanya ya kufanya vitu vya kimaendeleo yanatakiwa kuanzia kwa mtu mmoja halafu kaya, kijiji, kata, wilaya, mkoa hadi taifa.
Ukombozi wa fikra za mwananchi kwa kuondokana na mawazo ya kinyonge yatawafanya waendelee na pia kuwafutilia mbali viongozi wasiowajali.
 
Elimu:
Kuweka mifumo wa umwagiliaji sio sehemu ya miradi ya maendeleo? Jibu: ni sehemu ya miradi ya maendeleo. Pia usalama wa chakula ni agenda ya Taifa lolote lile ili liweze kuwa huru. Kumbuka; ADUI YAKO MWOMBEE NJAA. Njaa huuza uhuru wa Nchi.

Na ujue kuanza kidogokidogo kama mtu binafsi ndio chanzo cha bomoabomoa maana hufanyika kiholela. Bora kupanga kuanzia mwanzo. Nchi inatakiwa kuwa na ramani kuonyesha miundo mbinu yote ili kuepuka leo lami inawekwa, kesho unabomoa kupitisha bomba la gesi, keshokutwa unabomoa kupitisha mifumo ya umwagiliaji.

Pia ujue vyanzo vya maji sio binafsi. Ni vya umma. Kwa hiyo kuyatumia bila idhini ya serikali ni ubatili.

Serikali inafanya mambo kinadharia zaidi na siyo vitendo.
Ni kweli kwamba ni vizuri kupanga tangu mwanzo lakini serikali haiwezi kusimamia kwa sababu ya uzembe au ujinga tu wa wenye mamlaka.
Chukua mfano wa miji, sehemu kubwa inajengeka kama ya wadudu huku viongozi wakigawana nyumba na maeneo yale yaliyopangwa na kujengwa na mkoloni.
Wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya kujifunza kubuni miradi yao yenye mpangilio hata kama siyo rasmi lakini unaoweza kuboreshwa baadaye.
 
Mwaka huu ni tani kiasi gani zimekopwa na Serikali? Nini kinatakiwa kuanza, kuzalisha kwanza ndo utafute masoko au unatafuta soko kwanza ndo unazilisha kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na soko? Elimu hii ni mujimu sana kwa wakulima wetu ili wasitegemee sana serikali kuwatafutia masoko.
 
Elimu:
Kuweka mifumo wa umwagiliaji sio sehemu ya miradi ya maendeleo? Jibu: ni sehemu ya miradi ya maendeleo. Pia usalama wa chakula ni agenda ya Taifa lolote lile ili liweze kuwa huru. Kumbuka; ADUI YAKO MWOMBEE NJAA. Njaa huuza uhuru wa Nchi.

Na ujue kuanza kidogokidogo kama mtu binafsi ndio chanzo cha bomoabomoa maana hufanyika kiholela. Bora kupanga kuanzia mwanzo. Nchi inatakiwa kuwa na ramani kuonyesha miundo mbinu yote ili kuepuka leo lami inawekwa, kesho unabomoa kupitisha bomba la gesi, keshokutwa unabomoa kupitisha mifumo ya umwagiliaji.

Pia ujue vyanzo vya maji sio binafsi. Ni vya umma. Kwa hiyo kuyatumia bila idhini ya serikali ni ubatili.

Maendeleo ni relative, huwezi ukafanya mambo makubwa kama huwezi madogo.
Kila kitu ni muhimu kufanywa kulingana na hali halisi.
Vyanzo vya maji ni mali ya uma na uma wenyewe ni wanavijji. Hizi mamlaka za kitaifa zinatakiwa kuangalia maslahi ya wanavijiji kwanza.
Sheria zinatungwa ili zitusaidie na siyo kutufanya watumwa.
 
Hivi ktk baraza la mawaziri na pogba mwenyewe,kuna sura yenye kuleta matumaini ya kuinua sekta ya kilimo au viwanda.hili janga hili daah?
 
Maendeleo ni relative, huwezi ukafanya mambo makubwa kama huwezi madogo.
Kila kitu ni muhimu kufanywa kulingana na hali halisi.
Vyanzo vya maji ni mali ya uma na uma wenyewe ni wanavijji. Hizi mamlaka za kitaifa zinatakiwa kuangalia maslahi ya wanavijiji kwanza.
Sheria zinatungwa ili zitusaidie na siyo kutufanya watumwa.

Bahati mbaya Sheria haipo hivyo. Kwenye kutumia vyanzo maji vijiji havina mamlaka.
 
Ndugu zangu,

Hapa Tanzania wapo watu wengi wa Private Sectors na matajiri binafsi ambao,kwa umoja wao na kwa upendo wao wa dhati,wanaweza kusaidia sekta ya kilimo hasa cha umwagiliaji.

Kilimo cha umwagiliaji,cha kisasa kinahitaji nguvu ya pamoja.Kuna haja ya kuwahusisha watu binafsi hasa wawekezaji ili watusaidie kwenye swala hili.

Tulishakuwa na chakula cha kutosha,itatusaidia sana Mh Rais.

Asante.
Kama kuna mahali tulirogwa basi ni hapa pa kuabudu hawa wawekezaji. Ndugu muwekezaji sio malaika ni mtafutaji haweki ambapo hana uhakika wa kuchuma. Uwekezaji ni uporaji.
Kukiwa na sera madhubuti za ardhi zitakazolinda na kuthamini wazalishaji wadogo wadogo (wakulima + wafugaji) ambao actually ndio wanalisha nchi then kilimo kikapewa kipaumbele na hii serikali unayotaka ikakumbatie wawekezaji wanyonyaji hakika njaa itapungua.

Wakulima na wafugaji wanaochomana mikuki na kuuana kila uchao si kwamba hawapendani no, tatizo ni hao hao wawekezaji ndio wamepewa ardhi yote na tija yake haionekani na chache iliyobaki inagombewa na hawa wafugaji na wakulima. Haijathibitika kuwa tumeshindwa kabisa matumizi sahihi ya rasilimali ardhi hadi ilazimu uwekezaji, hapana ni sera mbovu na wizi wizi tu. Ni sisi wenyewe ndio tutaondoa tisho la njaa.
 
Hao si wanalipa kodi, imebaki serikali kutumia hizo fedha za kodi kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa na chenye mavuno mengi.

!!NA SI KUNUNILIA MABOMBAIDER!!
 
Back
Top Bottom