matongo manawa
JF-Expert Member
- Apr 6, 2011
- 336
- 79
Ni bint mdogo mno lkn mwenye ujasiri wa pekee,Changamoto aliyoitoa kwa jamii ktk kumtetea mtoto wa kike apateElimu si ya kubezwa hata kidogo,lakini hasa ukizingatia pia mazingira magumu anakoishi.Nimetafakari msimamo na mchango wa mtoto huyu mana hata alipoulizwa akiwa mwenye maumivu makali kuwa ataendelea na harakati zake bila kuogopa kuuawa alijibu ataendelea.Nimemweka kwenye mzani mmoja Malala na na Dr Asharose Migiro(mtanisamehe)Huyu ni mama msomi na mwanamke aliyebahatika kushika nafasi ya juu ktk taasisi nyeti Duniani(UN)Katika utumishi wake sijawahi kufanikiwa kusikia au kusoma mchango chanya juu ya harakati za wazi za kutoachangamoto kwa ulimwengu kuhusiana na nafasi ya mwanamke,achila mbali duniani bali pia ktk serikali ya Nchi yakeambayo ameitumikia,Kuna wanawake mfano Marehemu Prof Wangai walisimama imara wataendelea kuwa mfano wa kuigwa karne na karneNa sasa bint Malala.Dr Migiro tumkumbuke kwa lipi?