kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Kusema kweli nimeguswa sana na Gwaji boy kiasi kwamba pamoja na mapungufu yake yaliyonifanya nisimuheshimu tena, umenifungua akili na kunifanya nirudi nyuma kutafakari upya jinsi ninavyomchukulia.
Ijapo aligusia tu kama mfano,wazo la kuhakikisha kila mtanzania anayeweza kusoma hadi chuo kikuu apewe nafasi, wakati akizungumzia taifa kuwa na vision, jambo hilo limenigusa sana kwa kuwa ninawafahamu watu wengi wenye uwezo wa kiakili, ila kutokana na sera isiyo rafiki ya elimu,wameshindwa kufikia ndoto zao za kufika chuo kikuu.Kikwazo kikiwa ni gharama kubwa mno kwa mtanzania wa kawaida.
Kipo chama cha upinzani kilikuwa na sera hii kwamba kingehakikisha kila mtanzania mwenye uwezo wa kusoma anasoma hadi atakapoamua kuchoka mwenyewe.
Taifa linakosa wasomi wa kweli kwani hakuna ushindani wa kweli katika elimu,na matokeo yake wale wachache waliopata bahati ya elimu ya chuo kikuu,kazi yao imekuwa kuitumia kama kitu cha kutambia mtaani tu huku wakishindwa kuonesha tofauti,jambo lililoamsha kasi ya mbunge mmoja anayejiita LY kuwaponda hadi maprof. kila wanapoongea kwa kuwa wanaonekana kutokuwa na faida inayoonekana na wakihisiwa ni watu waliojipanga kupiga dili tu kwa jina la usomi wao, huku wakikejeli kuhojiwa na watu wasio na elimu.
Natamani mawazo ya Gwajima yangekuwa ya Rais wetu akaliona hilo. Wasomi wakiwa wengi watashindana kuwa wabunifu kama wachezaji wanavyogombania namba kwenye timu.Tofauti na sasa,wale wachache wanashindwa kuwa wabunifu na ndio maana wanadharauliwa tu na wanaojiita LY.
Unaweza kuchukua tu mfano mtu ni LY anasomesha watoto wake zaidi ya watano kwa level za degree, lakini wanaporudi nyumbani,anasikitika kuwa walipoteza muda kwani wanarudi nyumbani wakiwa hawana uwezo wowote kukabiliana na mazingira wanayoyakuta nyumbani na mtaani.Aliyesomesha anabaki kuhoji,ni utafiti upi na nani aliufanya ulioonesha ni lazima watu wote wasome mwaka mzima kabla ya kuongia darasa jingine!
Gwajima leo umenigusa sana