Mchango na nafasi ya vijana wasomi kwenye maendeleo nchini

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,893
2,000
Habari ndugu, wana jf katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwalimu. Nyerere baba wa taifa nimeona nilete mada hapa ili tuijadili kwa pamoja kuhusu "mchango na nafasi ya vijana wasomi kwenye maendeleo nchini".

Kwanza ifahamike kwamba kwa tanzania kijana msomi ni yule aliyepata cheti cha elimu kuanzia form 4 na kuendelea na kwa takwimu mbalimbali vijana nchini ni asilimia 35% hawa ni wale wenye umri kati ya miaka 18-35. Pia inakadiriwa kila mwaka zaidi ya vijana laki nane 800,000 wanahitimu vyeti na fani mbalimbali nchini. Idadi hii inaweza ikadouble kufikia vijana 1.6 hadi 2 milioni kwa mwaka kuanzia mwaka 2025 ambapo kwa form 4 peke yake kutakuwa na vijana zaidi ya 1 milioni wanamaliza masomo yao.

Kabla ya kufika miaka hiyo ebu tuangalie kwa sasa mchango na nafasi ya vijana wasomi kwenye maendeleo nchini. kwa kifupi bado mchango wa vijana kwenye maendleo nchini ni hafifu sana, vijana wengi wasomi waliosoma kwa kutumia gharama kubwa sana na muda mrefu return yake ni ndogo sana ukizingatia fursa zilizopo duniani na nchini kwa jumla.

Ni kawaida kwa sasa kukuta vijana kwa maelfu kwenye interview inayoitaji watu kumi tu. pia nikawaida sana sasa kumkuta kijana msomi mmachinga amepanga vitu chini katikati ya jiji anauza kwa rejareja na pia imezoeleka sasa kwenye jamii zetu wasomi kwa maelfu hadi wa level kubwa zaidi degree na master kuwa tu idle mtaani wapo kwenye vijiwe wakisubili ajira zitangazwe.

hivi kama taifa tulishawahi kudajili na kuziuliza kwa nini hali hii na je itakuwaje hapo badae vipi athari zake kwenye uchumi na maendeleo kwa ujumla au tunadhani itakuja toke tu kudra siku moja vijana wote wawe na kazi na wengine wawe wafanyabiashara automatic la asha! hali hii ni dalili ya kujenga taifa lisilo salama huko mbeleni na lenye fujo za kila aina..

Tatizo lipo wapi hasa na ufumbuzi wake
kwanza serikali iwe na mipango rafiki kwa vijana wasomi idara zinazosimamia vijana na kazi kama taesa ziangaliwe upya majukumu yake yasiishie tu kwenye kuwapa wasomi wachache internship ila kiwe ni kitengo cha kitaalam cha mambo ya vijana wasomi kinachotoa ushauri na usimamizi wa vijana katika kujikwamua na umasikini na kuleta maendeleo nchini.

Pia mbio za mwenge zitumike kuamsha hari za vijana wasomi nchini kwa kuwafikia vijana hao na miradi yenye tija ikaguliwe na kutolewa mitaji. Mwenge usiishie tu kufungua madarasa na zahanati na barabara za kilometa 1 kila mwaka ni hivyohivyo.

Pili vijana tujipambanue kwa kufuatilia fursa mbalimbali nchini na nje ya nchi.. tujikite kwenye kutumia ujuzi tulioupata kwenye vyuo na shuleni kwenye kuleta tija ya maendeleo nchini. tufikilie bila kuchoka tusome na kufanya tafiti bila kukata tamaaa..

Tatu viongozi wetu waache mara moja kuwatumia vijana kama mitaji ya kisiasa na kujitafutia umaarufu badala yake wawe njia, dira na taa kwa vijana wa tanzania tuache kuwageuza vijana kuwa chawa(tabia inayomea kwa kasi sana nchini kwetu sasa hivi) badala yake wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wawashe switch on kwa vijana kuweza kuona fursa zinazowazunguka na namna ya kuzifikia fursa hizo..

Kwa Wajamii vijana wasomi waaminiwe nawahakikishia vijana wengi wasomi hapa nchi wana majawabu ya matatizo mengi yanayotuzunguka kwenye jamii zetu tatizo jamii haiwaamini na hawapi fursa hizo badala yake wanaonekana ni ovyo au usomi wao hauna maana hasa pale inapotokea kijana msomi amekosa ajira..

Wadau karibuni kwa mjadala huu huku tukiendelea kuadhimisha kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kumbukizi ya baba wa taifa.

baba wa taifa.jpg
 

Sam mirror

JF-Expert Member
Sep 29, 2018
980
1,000
Mchawi elimu inayotelewa ni copy and paste ya wazungu, haimuandai kujiajili elimu ibadilishwe elimu ya ufundi iwe kipaombele kutokana na mazingira ya kitanzania.
 

Misss Chuga

Senior Member
Oct 6, 2021
129
250
Mchawi elimu inayotelewa ni copy and paste ya wazungu, haimuandai kujiajili elimu ibadilishwe elimu ya ufundi iwe kipaombele kutokana na mazingira ya kitanzania.
Sijasoma alichoandika ila nadhani umefupisha maandishi yake.


Hata elimu ya darasani wanafunzi wajitaidi kuifahamu kwa vitendo sio mi theory tu. Mfano Chemistry ni zaidi ya uchawi mtu akilimaster na kulifahamu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom