Mchangiaji kuhusu katiba mpya jina MJUNI GEORGE na sauti ni PIUS MSEKWA

Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,327
2,000
Mungu nisamehe mie. Mchangiaji wa mwisho kwenye maada iliyokuwa inaendeshwa na STAR TV kwa kujitambulisha kwa jina la MJUNI GEORGE NA HUKU SAUTI YAKE NI KAMA ILE YA PIUS MSEKWA hapa nimekoma. Ninamshauri pia atambue hao wanaopiga simu ndo wanamchi wenyewe na haingewezekana wote kupata nafasi ya kupiga simu kwa wakati mmoja. THANKS YAHAYA KWA KUSHTUKIA HILO PIA JAPO BUSARA ZIMEKUTANGULIA NA UKAUCHUNA.
 

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Unapoanzisha mada ni vyema utambue kuwa wana JF wengine hawakusikia hayo majadiliano. Ni vema ukatoa muhtasari wa kilichotokea ndipo ukatoa mawazo yako.
 

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
195
Ni kweli tulikuwa tunasikia mjadala wa star tv kuhusu katiba mpya -mchagiaji wa mwisho aliyejimbulisha kwa jina la mjuni goerge tulitambua kuwa sauti na utambulisho ilikuwa tofauti-pius msekwa tunamfahamu hata kwa sauti -ila alishindwa kujitambulisha wala kubadili sauti yake -lakini hii haitushazi ni yaleyale tunasema moral authority na harakati za kulinda maovu yao.

Hata yahya mhoza alichanganyikiwa kusikia sauti ya mtu anayemfahamu akitambulisha kwa sauti nyingine ambaye alisema wanaochangia mada za katiba watoe maoni yao sio waseme maoni ya wananchi lakini akasahau kuwa yeye ni tabaka lingine na sisi ni tabaka lingine tunaongea tunajua kilio chetu -bahati yake mjadala ulikuwa umekwisha ningepiga na kumwambia saa imefika kuwaweka hadharani na hujuma zao -wamekosa moral authority
 

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,555
1,170
hao siku zao zilishaisha wajiandae tu kubeba virago, walidhani watz wataendelea kuwa mavuvuzela siku zote
 

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Pamoja na kutojua huyo Mjuni alias Msekwa alichangiaje, lakini haina budi ikumbukwe Pius Msekwa ndiye aliyekuwa katibu wa Tume iliyafanya maandalizi ya katiba ya sasa; katika hali hiyo, bila shaka itakuwa vigumu kwake kukaa kimya wakati umma wa watanzania wanaonyesha dalili za wazi za kuihusisha katiba hiyo na kudumaa kwa Tanzania.
 

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
1,750
Kwa hiyo alichangia kitu gani? was he for or against it?..tupashe habari iliyokamilika ndugu zetu..hii thread imekaa kijuu juu sana, malizia
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,353
2,000
...na hasa hasa alikuwa anataka kuwapiga madongo Jeneral Ulimwengu na Mzee Cheyo wa mapesa kutokana na kauli zao kwamba wananchi sasa wako tayari kwa katiba mpya. matokeo yake kwa kutojiamini maana hata yeye alikuwa haamini anachosema akaishia kutaja jina la Uongo sijui akifikiri anamdanganya nani! Hii ndio aina ya Viongozi tulio nao. Anaogopa kutaja jina lake la kweli maana haya yeye mwenyewe ndani ya Moyo wake haamini anachokisema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom